Qa people
Member
- May 8, 2020
- 54
- 34
Nakazia. Pesa sio zao, kwanini iwaume? Mungu ndie atupaye nguvu za utajiri.....Sisi tunatoa sadaka kwa hiari ninyi mnaumia nini?,wivu tu.
Kum 8:17-18
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nakazia. Pesa sio zao, kwanini iwaume? Mungu ndie atupaye nguvu za utajiri.....Sisi tunatoa sadaka kwa hiari ninyi mnaumia nini?,wivu tu.
ni watu waliokata tamaa ya maisha wenye ufukara wa kutisha.
tunalo tumaini la kesho yetu nzuri ndani ya yesu!
Ogopa sana haya makanisa feki ya mitume manabii na makuhani hayo makanisa huwa siingii hata kidogo kuna nguvu za giza sana yani ukifika humo unakuwa mjinga wa akili na mpumbavu mpaka ufilisike kabisa ni waganga wa kienyeji haoWanabodi
Kama kawa kila nipatapo fursa huja na makala zangu elimishi za kwa maslahi ya taifa. Topic ya leo, ni kutoa wito kwa Serikali yetu kuingilia kati kitu kinachoendelea kwenye baadhi ya makanisa ya wakovu yanayojinasibu kufanya miujiza, kutoa mapepo, kutoa uchawi na kufanya miujiza ya uponyaji?.
Baadhi ya wahubiri hawa wanatumia nguvu za giza za kiini macho kwa kitu kinachoitwa auto suggestion kwa Watanzania Masikini wa Kutupwa, kuaminishwa umasikini wao ni kwasababu wamelogwa, hivyo ili kuuondoa uchawi wa umasikini, unatakiwa kufanya appointment kumuona Mtumishi, ambapo utapangiwa kiwango cha fedha kumuona mtumishi.
Kwenye matangazo yao kupitia redio na TV, unaambiwa njoo na sadaka yako bila kuambiwa kiwango. Ukifika kanisani,
utaandikishwa na kuambiwa kiwango cha kumuona mtumishi akueleze jinsi ulivyologwa na ni nani amekuloga. Kiwango kilianzia 10,000, baadae ikawa 20,000, ikapanda kuwa 50,000, 100,000 sasa ni 200,000.
Unatakiwa kuitafuta hiyo pesa popote ulipe ndipo umuone mtumishi. Hivyo ni waumini wenye pesa tuu ndio watamuona mtumishi!.
Baada ya kuingia kumuona, mtumishi atakuambia prophesy yako na ku conclude matatizo yako yote, ya kiuchumi, umasikini, maradhi, au majanga yoyote, ni umelongwa na watu wa jijijini kwako!.
Baada ya hapo sasa ndio utapewa bili ya sadaka. Mtumishi atajifanya anamuuliza Mungu, then unaambiwa Mungu amesema njoo na sadaka ya milioni 2, 5, 10, 20, kutegemea na ukubwa wa tatizo lako, ya kuleta hiyo sadaka ndipo Mungu atalimaliza tatizo lako!.
Kutokana na wewe kuwa ni tayari umesha pigwa ganzi, utakwenda kuzitafuta hizo pesa na kuzileta cash!.
Watanzania masikini wa kutupwa, wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli, na baadhi ya hawa ma Pastor, huku hao ma Pastor na wahubiri wakineemeka na kuageuka mamilionea na mabilionea huku wakivuta mi ndinga ya nguvu!.
Kuna Mama mmoja alifiwa na mtoto wake, the only son, amedanganywa mtoto wake hajafa, amechukuliwa tuu kichawi, mama kaambiwa akatafute sadaka kiasi fulani, arejeshewe mwanae!, huyo mama ana haha kusaka hiyo pesa ili kumrejesha mwanae!.
Japo haya ni mambo ya imani, na waumini wanakwenda wenyewe kwa hiyari yao na wana toa fedha kwa ridhaa zao, na serikali yetu imetoa uhuru wa kuabudu, lakini ikifikia kiwango Watanzania wanatapeliwa, serikali ina wajibu wa kuingilia kati wananchi wake wasiendelee kutapeliwa!.
Namalizia kwa ile hoja ya msingi jee kuna haja ya serikali iingilie kati shughuli za haya makanisa ya wakovu ya miujiza ili Watanzania masikini wa kutupwa, wasiendelee kukamuliwa mamilioni kwa utapeli, huku wahubiri wakizidi kunona kwa kuwa mamilionea!.
Naomba kuwasilisha.
Paskali
Update
Mkuu Mywangu, usimwingize Mtumishi kweli wa Mungu, Kuhani Mussa, kumuona Kuhani Musa ni bure ila unaweza kuleta sadaka yako yoyote.
Kazi ya ujenzi wa Ngome ya Yesu pale Kimara Temboni, inafanyika kupitia kadi zinaitwa Partnership, hupangiwi kiwango, unajifanyia personal assessment ndipo unajaza!.
Watumishi matapeli kumuona ni lazima utoe 200,000, kuna watu walikuwa na 100,000 walitoa na zikapokelewa, watu wa 200,000 walipoongezeka, wale wa 100,000 walirudishiwa fedha zao, wakaambiwa wakadundulize mpaka zitimie 200,000 ndipo warudi.
Ukimuona Kuhani Mussa anakuombea na kukupatia vifaa vya kiroho bure extra utalipia lakini kuwaona matapeli hawa, unatakiwa kwenda kuleta kwanza sadaka, with the amount, from 6 figures ndipo uombewe!.
P
Nimemuona Nabii mmoja kwenye TV saa nane mchana akiwaambia kondoo wake kwamba watapokea dola toka USA na kwa mamlaka aliyopewa na Yesu wa Nazareth yule "Mbabe" atafungua mikoba yake na dola zitiririke mifukoni mwa hao kondoo! Kondoo walikuwa na furaha ya ajabu kama mazuzu kwa kuahidiwa dola. Kumbuka ni saa nane, watu badala ya kuchacharika wapo kanisani wanaomba dola ziteremke kama mana toka mawinguni. Ama kweli "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa". BTW, hapo mbele linaonekana kapu kubwa ambalo kondoo wanaweka shilingi za kitanzania kama sadaka...,Ndio maana Tapeli ' Kiboko ya Wachawi' aliwaingiza Wengi Mkenge!!!....na badohawakomi. 'Watu wangu wanaamhamia Kwa Kukosa Maarifa' !....Kweli.
DuhNimemuona Nabii mmoja kwenye TV saa nane mchana akiwaambia kondoo wake kwamba watapokea dola toka USA na kwa mamlaka aliyopewa na Yesu wa Nazareth yule "Mbabe" atafungua mikoba yake na dola zitiririke mifukoni mwa hao kondoo! Kondoo walikuwa na furaha ya ajabu kama mazuzu kwa kuahidiwa dola. Kumbuka ni saa nane, watu badala ya kuchacharika wapo kanisani wanaomba dola ziteremke kama mana toka mawinguni. Ama kweli "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa". BTW, hapo mbele linaonekana kapu kubwa ambalo kondoo wanaweka shilingi za kitanzania kama sadaka.
Kwa ufupi tu ukisikia mtume nabii sijui apostle kwa sasa ni kama waganga wa kienyeji tu usiende huko wana uchawi wa mvutoDuh
Ova
Na matapeli----wakiongozwa kwa sasa na huyo kutoka kaweKwa ufupi tu ukisikia mtume nabii sijui apostle kwa sasa ni kama waganga wa kienyeji tu usiende huko wana uchawi wa mvuto