Wajasiriamali Wadogo
Nimekuwa ninapekuwa na kusoma hizi nyuzi humu bila kuona hata mmoja unaogusia hali ilivyo mbaya mtaani haswa kwa wafanyabiashara wadogo. Biashara nyingi zinafungwa kutokana na mzunguko wa pesa. Biashara tamu pale uchumi wa nchi unapokuwa unashamili lakini unapoyumba wafanyabiashara haswa wadogo huwa wanaathirika sana. Hili ndio linalotokea sasa. Na kwa wale waliokuwa na mikopo kweli hali inatisha. Nasoma magazeti yamejaa matangazo ya kupigwa minada kwa dhamana mbali mbali. Je haijafika wakati serikali ikaingilia kati hili kuwanusuru wafanyabiashara wadogo haswa ukizingatia wamejikuta katika hali hii si kwa uzembe bali kwa mtikisiko wa uchumi wa nchi??!!