Serikali iingilie Kati - Wafanya Biashara Wadogo Tunalia!!

Kokola

Senior Member
Joined
Sep 5, 2015
Posts
135
Reaction score
78
Wajasiriamali Wadogo
Nimekuwa ninapekuwa na kusoma hizi nyuzi humu bila kuona hata mmoja unaogusia hali ilivyo mbaya mtaani haswa kwa wafanyabiashara wadogo. Biashara nyingi zinafungwa kutokana na mzunguko wa pesa. Biashara tamu pale uchumi wa nchi unapokuwa unashamili lakini unapoyumba wafanyabiashara haswa wadogo huwa wanaathirika sana. Hili ndio linalotokea sasa. Na kwa wale waliokuwa na mikopo kweli hali inatisha. Nasoma magazeti yamejaa matangazo ya kupigwa minada kwa dhamana mbali mbali. Je haijafika wakati serikali ikaingilia kati hili kuwanusuru wafanyabiashara wadogo haswa ukizingatia wamejikuta katika hali hii si kwa uzembe bali kwa mtikisiko wa uchumi wa nchi??!!
 
Kibaya zaidi TRA wanapandisha kodi bila kuangalia hali halisi ya mzunguko.wkt mwingine unalipa kodi ambayo haiendani na mtaji au mzunguko wako wa biashara...kwakweli serikali iliangalie hilo..
 
Ndio mtuombee turuhusiwe kusafiri nje ya nchi, kutengeneza wafanyakaz hewa, makontena hewa,semina kwenye mahotel binafsi,miradi hewa nakadhalika bila hivyo mtalia sana uchumi umeyumba maana uhalisia ndio huo kwamba 30% ya bajet ya serikali ilikua inafisadiwa kuingia mtaani hence uchumi hewa uliokua......
 
Kibaya zaidi TRA wanapandisha kodi bila kuangalia hali halisi ya mzunguko.wkt mwingine unalipa kodi ambayo haiendani na mtaji au mzunguko wako wa biashara...kwakweli serikali iliangalie hilo..
Kibaya zaidi TRA wanapandisha kodi bila kuangalia hali halisi ya mzunguko.wkt mwingine unalipa kodi ambayo haiendani na mtaji au mzunguko wako wa biashara...kwakweli serikali iliangalie hilo..
Hamna namna kodi lazima ilipwe tu awamu hii hamna cha mfanyabiashara mdogo wala nn namba tuisome wote
 
Hakuna anaekataa kulipa kodi.,tatzo ni pale wanapotaka kufikia malengo au kuvuka kwa kumkamua zaidi mtu wa chini bila kuangalia hali halisi..ikumbukwe pia kuwa serikali ina wajibu wa kutengeneza mazingira rafiki na mfanya biashara ili alipe kodi endelevu sio kumkoa ili afunge biashara..
 
Wacha tuisome Namba...maana kama kosa mlishalifanya siku ya Election
 
Wajasiriamali Wadogo
Nimekuwa ninapekuwa na kusoma hizi nyuzi humu bila kuona hata mmoja unaogusia hali ilivyo mbaya mtaani haswa kwa wafanyabiashara wadogo. Biashara nyingi zinafungwa kutokana na mzunguko wa pesa. Biashara tamu pale uchumi wa nchi unapokuwa unashamili lakini unapoyumba wafanyabiashara haswa wadogo huwa wanaathirika sana. Hili ndio linalotokea sasa. Na kwa wale waliokuwa na mikopo kweli hali inatisha. Nasoma magazeti yamejaa matangazo ya kupigwa minada kwa dhamana mbali mbali. Je haijafika wakati serikali ikaingilia kati hili kuwanusuru wafanyabiashara wadogo haswa ukizingatia wamejikuta katika hali hii si kwa uzembe bali kwa mtikisiko wa uchumi wa nchi??!!
Kasikilize mkutano wa BOT wanatoa majibu rahisi kwa maswali magumu.....sijawa na uhakika kama hawaoni hii hali au wamejitoa ufahamu kama mtu alievuta bangi.
 
Nahisi kufa biashara ni kwamba wateja hakuna kwa sababu kodi ilikuwepo enzi hizo mifuko ikiwa imetuna na biashara zilikuwa zinaendelea kama kawaida ila kwa huyu jamaa ukitaka kutoa hela mfukoni lazima utafakari kwanza kama unachotaka kununua ni muhimu.
 
Nimeenda kununua maandazi kwa Mama muuza kitafunio mtaani ananiambia leo hajapika yako ya jana. Namuuliza kulikoni anasema sikuhizi kapunguza kipimo na hata hivyo vitafunio haviishi siku ile ile wateja wamekauka!! Kuna mifano mingine kama hii au ni huu mtaa wetu tu jamani...?
 
Inawezekana kweli maanake mimi nimeacha kunywa chai,bajeti iko tight.
 
Back
Top Bottom