Serikali iitishe kura ya maoni Wazanzibari waamue upya kama wanautaka muungano ili isionekane tunawalazimisha

Naunga mkono hoja. Na baada ya hiyo kura ya maoni, ikiwezekana waendelee tu na Taifa lao kama ilivyo kwa Comoro, nk.
Halafu tukutane nao EAC.

Kitakachotokea:

1. Kama Samia atakuwa bado madarakani, italazimu Tanganyika kuongozwa na Rais wa mpito kwa mara ya pili.

2. DPW itabidi iende kue desha bandari za Zanzibar, maana imekuja Tanzania kama deal la wazanzibari.

3. Zanzibar litakuwa taifa la kwanza la kigeni kuuziwa umeme na TANESCO.

4. Mchele na ndizi toka Tanganyika zitaanza kuuzwa Zanzibar kwa kutumia sarafu ya Marekani.

5. Itakuwa patashika Tanganyika itakapotangaza wahamiaji toka Zanzibar kutakiwa kukamilisha taratibu za uhamiaji, huku wengi wakiamua kuukana uraia wa Zanzibar ili kukidhi sheria ya uhamiaji ya Tanganyika!!

Katika porojo ni rahisi sana kusema Muungano uvunjike, lakini kiuhalisia, hilo likitokea, inaweza kuchukua hata miaka 50 mpaka Zanzibar kutengamaa kama Taifa.
 
Tatizo ni kwamba waliotuunganisha ni CIA na MI6! Wala hatukuwa sisi! Sababu ilikuwa ni kuzuia uislam kuenea Tanganyika! Mnaona sababu yenyewe ya muungano? Ina mantiki au ni ya kibwege?
 
Mkuu, we ni mzanzibari pia?

Nipe rejea za visiwa vinavyomiliki ukanda wa pwani wa bara fulani ili nijifunze huwa inakuaje!
Mimi sio mzanzibar ila ukanda wa pwani wote ni sehemu ya zanzibar .Pia usiwe na wasiwasi kwa sababu hata muungano unapovunjika yoyote anaweza kuishi popote kwa kufuata sheria.

Mzanzibar anaweza kuomba uraia wa huku na huku akapta kule ,juzi tu hapa wapemba wamepewa uraia huko kenya.
 
Una hoja nzuri lakini mpango sio mzuri


Kwa upande wa kura hauwezi kuleta majibu sahihi, wamasai waliofukuzwa Ngorongoro walitafutwa wamasai uchwara ambao walikuwa wanasapoti kuondolewa na kuipongeza serikali.


Hata katika hilo hawashindwi kufanya figisu ili ionekane muungano unapendwa
 

Ukanda wa pwani hawawezi kuupata.

Haijawahi kutokea mahali popote Duniani, kisiwa kumiliki inland, ila kuna inland countries nyingi zinazomiliki visiwa.
 
Wakishajitenga na kuunda Taifa lao huru, Rais Samia atakosa sifa ya kuwa Rais wa Tanganyika.
 
Muungano ulifanyika kwa usiri mkubwa Kati ya Mwl na Mzee. Hvyo watu hawakushirikishwa.
 
Over their dead bodies.
Chama tawala hawako tayari kabisa kukubaliana na hoja hii. Kama wanaiba matokeo ya kura toka 1995, uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, unadhani watakubali hio kura?
 
Mtakuwa tayari kupambana na mujaheedin upenuni mwenu ?

2035 inabidi wapelekewe rais mlokole kutoka Morogoro.
 
Wanalia lia sana hawa watu ifike wakati maamuzi magumu yachukuliwe wenyewe wamejaa kuuza samaki hadi vichochoroni huko bara lakini hawataki wabara wakafanye kazi,na kazi zenyewe wawe wanaweza sasa kufanya,huku wanapewa URC,DC na nyadhifa mnalimbali kwao ni wao kwa wao bado hawaoni hayo yote
 
Bara wanautaka Muungano kwa nguvu zote kwa maslahi ya Kanisa Katoliki. Rejea maneno ya Lukuvi kupinga wazanzibari kujitoa ktk Muungano.
Kanisa haliko tayari Muungano uvunjike
Kama kawa. Lawama zote kwa John.
 
Tatizo ni kwamba waliotuunganisha ni CIA na MI6! Wala hatukuwa sisi! Sababu ilikuwa ni kuzuia uislam kuenea Tanganyika! Mnaona sababu yenyewe ya muungano? Ina mantiki au ni ya kibwege?
Lawama zote kwa John.
 
Ata mikoa mingi iliungwanishwa kwa kanda zake vipi nazo kanda tuzipe uhuru?.
 
Zanzibar ingekuwa huru, ingepinga hatua kubwa kimaendeleo na ingepata fursa nyingi kuliko kuendelea kukaliwa na mkoloni Tanganyika
Zanzibar ni kisiwa pekee barani pembezoni mwa hili bara?

Maendeleo ya visiwa vingine yapoje? Nielimishe kuhusu Comoro!
 
Cc Mohamed Said una maoni gani.

Tugawane mbao tu kila mmoja ajenge kwake. Nilimsilikia mbunge mmoja anasema Watanganyika wakija Zanzibar wanatakiwa kuwa na passport.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…