Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Hivi sasa mabenki wanatutumia sms wakitushauri tuache utaratibu wa kufanya miamala kwa kutumia cash money na badala yake tutumie huduma za kielektroniki(mobile banking) kufanya miamala hiyo kama njia mojawapo ya kupambana na ugonjwa wa corona.
Binafsi naupokea ushauri huo ila nawashauri kwanza wao wenyewe(mabenki na makampuni ya simu za mikononi) wajiongeza kwa kupunguza gharama za kufanya miamala husika ili kui-encourage watu kutumia huduma hizo na sio wao ku-focus tu katika kufanya kibiashara i wakati hili tatizo kwa sasa ni jambo la dharura hivyo nao wao wanapaswa kuli-handle kidharura ikiwa ni pamoja na kushusha gharama za kutumia huduma hizi za kimtandao.
Vile vile,katika kuhamasisha matumizi ya simu za mikunoni kufanya miamala hii,nawashauri watazame upya vigezo na mashari vilivyopo, mfano kukatwa hela hata kama huduma ulioomba imefeli/haijafika mwisho lakini wao wanakata tuhela kwenye simu yako na kwenye akaunti yako ya benki bila kujali huduma uliohitaji imekamilika(hili jambo huo nalliona ni kama kuibia wateja).
Mwisho,napenda kuishauri serikali kuwa huu ndio wakati muafaka wa kupeleka miswaada/sheria Bungeni kwa hati ya dharura ili kutunga sheria au kurekebisha sheria zinazoweza kusaidia kupambana na janga hili endapo ugonjwa huu utageuka tishio humu nchini na mojawapo ya mabadiliko nayopendekeza(iwapo kutakuwa na huo ulazima kulingana na hali ya huu ugonjwa) ni kupunguza kodi ya kufanya miamala kwa njia za kieletroniki.
Hivyo, Serikali kupitia BOT,TCRA na Wizara ya Fedha, huu ni wakati wa nyie ku-monitor hii situation na kufanya kile kilicho katika mamlaka yenu katika kupambana na janga hili na mojawapo ni kutazama pendekezo hili iwapo hali ya ugonjwa huu kweli italazimisha hatua kama hizo kuchukuliwa.
Kila mtu kwa nafasi yake ni mdau katika hili janga kwani linagusa karibu kila eneo mbali na kugusu karibu kila mtu kiuchumi na kijamii.