Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Katika jamii yetu, ongezeko la watoto yatima na wanaokataliwa na baba zao limekuwa changamoto kubwa. Hali hii inawaumiza watoto wasio na hatia na kuathiri mustakabali wao.
Niliguswa sana na tukio lililomkuta dada yangu, ambapo mume wake aliamua kupima DNA kwa watoto wake watatu na kugundua mmoja tu ndiye alikuwa wake. Tukio hili lilileta maumivu makubwa na kuyumbisha familia.
Kutokana na hili, napendekeza tuanzishe chama cha wanaume wanaokubali kutunza watoto bila kujali matokeo ya DNA.
Lengo ni kuwalea watoto wote waliozaliwa katika mazingira ya ndoa au mahusiano kwa upendo na uwajibikaji.
Huu ni mwito kwa wanaume kujenga jamii yenye maadili bora kwa kukubali na kulea watoto kwa moyo mmoja, bila kujali changamoto za kihisia au ukweli wa DNA.
Tukiwalea watoto kwa upendo, hatutasaidia tu kupunguza idadi ya watoto wa mitaani bali pia tutasaidia kuunda kizazi chenye heshima na maadili mema.
Haya mambo ya kukimbilia DNA yamewaponza wengi, na mwisho wa siku, kinachoathirika ni maisha ya mtoto.
Tunawapongeza wanaume wote wanaotimiza majukumu yao bila kuzingatia DNA. Mungu awabariki na kuwalipa kwa mema mnayoyafanya. Ni wakati wa kuonyesha utu wetu kwa vitendo.
Tunaingia Ibadan kwa Chief Prof Suguye!