Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 524
- 829
Tarehe 24 Steptemba 2026, Mbunge huyo alitembelea Kijiji cha Mbesa ambapo wananchi walimfikishia changamoto kadhaa, hasa tatizo kubwa la wafugaji kuwaingilia wakulima kwa kufuga mifugo yao kwenye mashamba na kuharibu mazao. Wananchi hao wamelalamika kuwa hakuna juhudi za kutosha kutoka kwa serikali kuwakabili wafugaji hao na kusuluhisha mgogoro huo unaoendelea kuwaathiri.
Akizungumza na mbunge huyo, wananchi watatu, akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, walieleza kero zao. Mwenyekiti huyo alidai anachelewa kulala kutokana na kusikiliza malalamiko ya wananchi wa eneo lake kuhusu ng’ombe za wafugaji. Aliongeza kuwa hata yeye mwenyewe ameathirika na tatizo hilo baada ya wafugaji kuingia katika eneo lake.
“Sasa nimezoea watu wanakuja kwangu kuniletea malalamiko, lakini na mimi yamenifika japo ni kiongozi wa serikali na sijui nitamfikishia nani kero zangu,” alisema mwenyekiti huyo.
Kwa upande wake, Mbunge Ado Shaibu Ado aliwaahidi wananchi wa Mbesa kuwa atalifikisha jambo hilo Bungeni. Alitoa msimamo wake kwa kusema anaamini kuwa serikali ikiamua kulimaliza tatizo hilo, linaweza kutatuliwa hata leo.
Ziara ya mbunge huyo inaendelea katika vijiji mbalimbali vya jimbo lake kwa lengo la kusikiliza sauti za wananchi na kuyashughulikia masuala yanayowakabili.