DOKEZO Serikali ikichunguze Kituo cha Afya Optimisim Dispensary cha Mwanza, mazingira ni machafu na huduma zake mmmh!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Katika Mkoa wa Mwanza, Kata ya Kirumba, kuna kituo cha afya kinachoitwa Optimisim Dispensary ambacho kinakabiliwa na malalamiko makubwa kutoka kwa wananchi na hata baadhi ya wafanyakazi wake.

Inadaiwa kuwa hakijasajiliwa rasmi, na baadhi ya watumishi wanaotoa huduma hawana leseni hai za kufanya kazi za afya. Hali hii imeibua wasiwasi mkubwa juu ya usalama na ubora wa huduma zinazotolewa kwa wagonjwa.
photo_2026-06-01_12-46-44.jpg

photo_2026-06-01_12-46-43.jpg

photo_2026-06-01_12-46-42.jpg
Aidha, kituo hicho kinatajwa kuwa na utaratibu usio halali wa utoaji wa huduma, ikiwemo kutoza fedha kwa baadhi ya vipimo ambavyo vinapaswa kuwa na utaratibu maalum, kama vile kipimo cha VVU (HIV) kinachodaiwa kutozwa shilingi 5,000. Pia, kuna madai kuwa majibu ya vipimo vinavyotolewa si sahihi, kwani wagonjwa wanaopima tena katika hospitali kubwa kama Bugando Medical Centre hupata majibu tofauti na yenye uthibitisho zaidi.

Kwa upande wa rasilimali watu, kituo hicho kinadaiwa kushindwa kuwalipa wafanyakazi wake kwa wakati, hali inayosababisha wengi wao kuacha kazi. Kutokana na hilo, inasemekana kuwa kituo kinaajiri watu wasio na vigezo stahiki, wakiwemo wahitimu wapya au watu wasio na taaluma ya afya, na kuwapa majukumu makubwa kama ya udaktari au maabara. Pia, kuna malalamiko dhidi ya baadhi ya watumishi, akiwemo muuguzi anayetajwa kwa jina la F... A..., kwa madai ya kuwafokea na kuwanyanyasa wagonjwa.

Soma Pia; Kituo cha Afya cha Manda, Wilayani Ludewa (Njombe) kina mazingira machafu kama vile kimetelekezwa

Vilevile, mazingira ya kituo hicho yameelezwa kuwa machafu na hatarishi kiafya. Inadaiwa kuwa kuna chemba ya choo inayovuja na kutoa harufu mbaya inayosambaa hadi ndani ya vyumba vya wagonjwa. Aidha, taka za hospitali kama sindano zilizotumika huhifadhiwa vibaya kwenye mifuko bila uwepo wa kichomea taka (incinerator), jambo linaloweza kusababisha maambukizi. Pia, maji yanayotumika si salama vya kutosha, yakitajwa kuwa ni ya kuhifadhiwa kwenye mipira badala ya mfumo wa maji tiririka.

Kwa ujumla, wananchi wa eneo hilo wanaendelea kulalamikia ubora duni wa huduma, gharama kubwa za dawa, na ukosefu wa uwajibikaji wa uongozi wa kituo hicho, ambapo inadaiwa kuwa msimamizi hana taaluma ya afya lakini anajiita daktari. Wananchi wanaomba mamlaka husika zichukue hatua za haraka kuchunguza na kushughulikia changamoto hizi ili kulinda afya na usalama wa jamii.
 
Poleni sana, hapo hakuna afya
 
Nini kinawafanya wagonjwa waendelee kwenda- pale au ni fitina za Kibiashara hizi!!!?tu
 
Back
Top Bottom