Serikali ikikosea kesi ya Mbowe, naamini Ujerumani watafunga ubalozi

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Kama tulivyosema kuna watu wanajaribu kumwaribia Raisbkwa kuweka hizi kesi za kijinga. Ubalozi wa German ndiyo Lissu alikimbilia baada ya kutaka kutekwa baada ya uchaguzi na walimpeleka mpaka Airport. Kwasasa watu kwenye kesi ya Mbowe na wanapima kuona kama Tanzania inabadilika au iko vilevile kwenye haki za binadamu na demokrasia.

Lakini Rais hajui kwamba wabaya wake wanataka hizi Balozi ziondoke ili kumpunguzia nguvu lakini wanamdanganya kwamba kuwabana wapinzani ni kuwasaidia CCM na hii haina ushahidi wowote. Serikali isikoweka viongozi wazalendo ambao hanawa njama itaingizwa kwenye matatizo. Leo hii Rais badala ya kushangiliwa New York sifa zimeenda kwa Rais wa Zambia kwasababu tu ya hii kesi.

Serikali kuweni makini nawapa ukweli huu.
 
Duh...!, Mkuu Kamundu, yaani Tanzania iachane na utaratibu wa kuruhusu sheria kufuata mkondo wake kwasababu tunaigopa Mjerumani atafunga ubalozi wake nchini?!. Mwenzetu umejuaje haya au kumbe na wewe mwenzetu uko ubalozini Ujerumani ?.
Kesi ya Mbowe si naendelea kusikilizwa, kwanini kuingilia uhuru wa mahakama yetu kwa kututishia nyau kuwa watafungasha virago vyao watimke?. Hivi hao wanabalozi wa Ujerumani, hicho ndicho kilichowaleta nchini ?!.

Acheni kuwasingizia wana Balozi mambo ya ajabu. Acheni mahakama itimize wajibu wake bila kuingiliwa au kupewa mashinikizo.
P
 
Wafunge tu maana kama tunakosa ubinadamu kisa kukomoa wapinzani
 

Una hoja lakini imekaa kiumbeya zaidi..

Wewe unaona wivu rais wa zambia kushangiliwa= hii ni roho mbaya sana.
 
[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419]



Pascal umeua
 
Pamoja na Yote Polisi wetu ni hatari sana mimi binafsi siwaamini tenaaaa.
 
Tanzania kuna sheria? Tangu lini? 😳😳😳


 
Naona ufahamu wako umeanza kurejea Kama mwanzo.Maana tangu ulipoitwa Bungeni,ukatia Nia kule Kawe,ulikuwa siye Yule tuliyemujua.
 
hawa chadema wana akili za kushikiwa, ni shida juu ya shida kwa wenyewe kwa wenyewe. wamewatoa kina halima mdee ambao walikuwa na hekima kidogo, sasa wamebaki mazuzu watupu. tupa kuleeeeee
 
Nyie ndio washauri wa Rais mnaomdangaya mkifikiri kujipendekeza kwa Wazungu inalipa. Mgejifunza na yatokanayo na hotuba ya pale UN jana usiku ili mbadilike. Kupiga picha na da mange kulizuia mabango?
Ijapokuwa JF hatufahamiani personally, lakini kwa posts zako inaonesha wewe jamaa ni MSHAMBA sana
 
Lini mahakama za Tanzania tangu enzi ya Mwendazake ilikuwa huru?
Sihitaji kukumbusha Jaji wa Kimkakati aliyekataliwa na Mbowe vituko vyake (rejea:Sauti Kubwa kwa in depth analysis ya uteuzi na hukumu zake)
Kangaroo courts haziwezi kutoa hukumu ya haki popote duniani
 
Tangu lini Serikali ya Tanzania ilifuata sheria? Si unawasikia akina Kingai wanavyofanya kazi? Ni sheria ipi wanayofuata?

Vyombo vya serikali vinafanya kazi kama magenge ya majambazi.
 
Sihitaji kukumbusha Jaji wa Kimkakati aliyekataliwa na Mbowe vituko vyake


Elezea mzee
 
Kada wa ccm katika ubora wako
Safari hii ukurugenzi utakufuata mlangoni kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…