Serikali ikikosea kesi ya Mbowe, naamini Ujerumani watafunga ubalozi

Lini mahakama imeacha kuingiliwa na CCM?
Na lini ilikuwa huru?
Tuache kujipendekeza kwenye mambo ata mtoto wa form one anayajua,ni ujinga,ni unprofessional
 

Nakazia: Akikusikia kwa maneno tu huyu:



Usiache kutuletea mrejesho.
 
Miaka yote hiyo ndani ya JF bado unaandika ujinga-jinga tu! Huwezi kupanga maelezo, unaleta hoja mfu, unaadika kiswahili kibovu, n.k. kwa nini usirudi shuleni kwa miaka hata miwili?
 
Wasepe tuu kwani nani anawahitaji? Hao wakoloni wametusaidia nini toka wametutawala
 

Weka mengine yote pembeni kwa maneno ya bwana Kasekwa mahakamani, hii nchi hatuna polisi bali tuna majambazi!

Ni aibu kuwa rais katika nchi ambayo Kingai, Mahita na timu yao iliyowafanyia unyama huu watuhumiwa eti ni walinzi wa jamhuri.

Kwamba Kasekwa na wenzake hata walikuwa wamelitumikia taifa kwa kiwango kile na kuwa malipo yao ndiyo hayo sasa wamepata toka kwa kina Kingai?

No wonder hata jumatatu kuingia mahakamani ni mpaka yatamkwe haya:

"No entrance no case."
 
Hapo amesite tu kwa kesi ya mbowe kama case study. Ila upuuzi wa police ni mwingi sana, wanagandamiza haki za watu kufanya mikutano, huku ccm wao wakijiachia. Usije ukafikir watafunga kwa ajili ya kesi ya mbowe tu ni mengi yanaendelea haswaa kuminya haki ya kimekrasia.
Akili yako pascal umeiacha wapi? Unashindwa king'amua hata jambo dogo kiasi hicho!!
Shame on you pascal.
 
Wewe msaliti sana wa Erick Kabendera. TENA BAHATI YAKO MBAYA MSUKUMA MWENZIO KAFA KABLA YA KUKUPA CHEO.
 
Acha upumbavu wewe. Unafikiri ujerumani wajinga wafunge ubalozi kwa ajili ya mbowe? Wao unafikiri ni kweli wanajali demokrasia zaidi ya maslahi yao ya kibiashara na tanzania? Yote kufuatilia hii kesi ni kufanya ubabe tu kuitisha nchi yetu. Kama wanajali utawala bora kuliko maslahi yao kiuchumi wasingekua na mahusiano na nchi kama saudi arabia. Tz inaendesha kesi ya mbowe kwa mujibu wa sheria zake wala sio kwa sheria ya ujerumani.
 
Binadamu wote wameumbwa na aibu kasoro Watanzania wachache!
 
inawezekana Mbowe kaonewa au hajaonewa..

ili la kufunga ubalozi eti kwa sababu ya kesi ya mtu fulani wakati yako mengi ambayo yameshatokea Tanzania zaidi ya hili, inatufanya tufikilie kiundani kidogo maslahi ya Ujerumani vs CDM au Mbowe... ni mtazamo tu..
 
Kwa kesi ya Mbowe, hakuna ishu ya "sheria kufuata mkondo wake".
1) Sheria ya "UGAIDI" iliyotumika kumfungulia kesi hii Kamanda Mbowe ni sheria mbovu. Hata kwenye hii kesi jaji aliyejitoa alikiri mapungufu. Pia inamnyima dhamana. Kwa ujumla, kanuni kuu ya INNOCENT UNTIL PROVED GUILTY " inakiukwa sana tu, maana mpaka hukumu ije kutolewa, mtuhumiwa tayari ameumizwa, amedhalilishwa, na haki zake kukiukwa.
2) Mazingira ya Mbowe kufunguliwa mashitaka haya yanatia mashaka makubwa. Mbowe ni nani, mahusiano yake na serikali, historia ya miaka 7 iliyopita, kuna kila dalili ya nia ovu.
3) Uzoefu wa kesi zilizoendeshwa dhidi ya wapinzani unaonesha kwamba kumekuwa na MALICIOUS INTENT. Lema alishitakiwa kesi ambayo Dhamana iko wazi. Lakini alikaa gerezani miezi 4 kutokana na malicious intent, mpaka majaji walipoamua awe nje kwa dhamana, walitoa karipio kwa waendesha mashitaka. Kesi wala haikuwa na mashiko. Nia ovu ya serikali ni kumwadhibu Lema kwa KIFUNGO CHA MIEZI 4 BILA KUTIWA HATIANI NA MAHAKAMA.
4) Kesi za "ugaidi" ni uchochoro wa serikali kuwaadhibu wapinzani . Hoja ni kwamba ccm haina uwezo wa kupambana na wapinzani katika "level field ya kisiasa. Huko Tabora mahaksma iliwahi kuionya serikali matumizi mabaya ya "kesi za ugaidi". Paskali, sisi siyo watoto wadogo
 

Naona uliruka hii kuhusu kuwapenda Mbowe!

P,

Sheria ifuate mkondo ni vema kama mahakama kweli ni huru. Lakini kwenye nchi ya kidemokrasia kumshitaki mwenyekiti wa chama cha upinzani kwa ugaidi sio kitu kidogo kama tunavyofikiria. Lakini vilevile historia inatusuta. Mpaka leo hakuna hata shitakiwa mmoja kwa kesi ya Lissu kupigwa risasi na ndiyo maana Lissu alivyoenda ubalozi hawajampuuza. Kuna wanasiasa wengi wapo magerezani bila kesi, Lissu mwenyewe ana kesi tano nyingine!!. Lakini mikutano imekatazwa hata ya ndani! sasa kama ni balozi ni lazima uangalie mbali na kujiuliza je hii ni nchi ambayo inakuwa kidemokrasia au inarudi nyuma?

Lakini vilevile wawekezaji wanaangalia miaka 20 mbele. Je Tanzania yenye 70% chini ya miaka 27 itakuwaje miaka 20 ijayo kama sasa upinzani ambao pamoja na mambo yote ulipata zaidi ya 30% ya kura 2015 lakini waangalizi wa kimataifa wameona uchaguzi wa 2015 ulivyokuwa. Tujue Tanzania ni nchi inayoendelea hivyo mabadiliko yatakuwepo lakini kwa wawekezaji hasa wa nchi hizi za magharibi mazingira ya uwazi na demokrasia ni muhimu sana kwao. Ukweli ni kwamba hao wajinga wajinga walikuwa wanamshauri Magu awe Raisi kama wa China. Maana yake hakuna demokrasia na yeye ni kama mtakatifu

Watanzania tusije tukajidanganya kama vile hawa wazungu wanawapenda wakina Mbowe na Lissu si kweli ufuatiliaji ni kupima wawekezaji wao wa sasa na ambao wanafikiria kuwekeza baadae. Vilevile usalama wao.

Lakini kuna mambo mengi sana nilishasema huko nyuma watu wakachukuwa miaka mingi kunielewa

1. Vitambulisho vya taifa nilisema miaka ya zamani sana
2. mikopo ya bank kuwa juu sasa ndiyo bank kuu imeamka
3. Niliongelea kwamba Magufuli akiondoka bandari ya bagamoyo itarudi
 
Mkuu Paskali, kwa andiko lolote lile unaloliandika hapa jukwaani, huwa nafarijika mno pale unapokuwa "objective" zaidi ya kuwa "subjective" pale unapojenga hoja zako. Katika watu ambao kila wakichangia humu jukwaani, wewe ni mmojawapo katika ya watu wachache wenye kuvutia "attention" ya hadhira kwa kiwango cha juu sana.

Naomba sana usimamie ukweli mchungu unaoutambua kuwa ni kweli tupu, zaidi ya kuwa na ushabiki wenye kujitoa ufahamu hata ukiwa na dalili zote za kutothamini haki ama uelekeo wenye kudhihirisha dhuluma juu haki za msingi za binadamu. Wewe unapothubutu kuonyesha hisia za kushabikia ama kuwa upande wa udhalimu na wadhalimu, hii ni sifa ambayo inaondoa ama kushusha "credibility" kubwa uliyokuwa nayo.
 
hawa chadema wana akili za kushikiwa, ni shida juu ya shida kwa wenyewe kwa wenyewe. wamewatoa kina halima mdee ambao walikuwa na hekima kidogo, sasa wamebaki mazuzu watupu. tupa kuleeeeee
Tangu Mdee atoke CDM hawezi kujenga hoja tena. Cha muhimu anaweza kuendesha maisha yake na ' mkewe'.
 
Pamoja na Yote Polisi wetu ni hatari sana mimi binafsi siwaamini tenaaaa.
Wewe waamini pasipo na shaka ndiyo maana umeweza hata kuandika huo mstari wa maneno ya kubeza.Maadamu tunawalipa kwa Kodi zetu hawataacha majukumu ya kwa kutishiwa nyau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…