Serikali ikinusuru Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere-Kigamboni

Uzalendi

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2013
Posts
221
Reaction score
15
Ndugu wadau sisi wanafunzi wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere-Kigamboni tunaomba mtufikishie ombi letu kwa Serikali kupitia Wizara ya Elimu ili iinusuru Chuo hiki.

Tunakaribia kurudi chuoni mwezi augusti mwaka huu bila kujua hatma ya chuo itakuwaje kwani kuna walimu pale hawani sifa na ushahidi ulishatolewa kwenye tume. Tulichangishwa fedha za bima ya afya (NHIF) kinyume na utaratibu na hatujarudishiwa. Kuna wanafunzi walifeli wakapewa vyeti na ushahidi pia ulitolewa kwenye tume.

Kuna ufisadi wa kila aina pale Chuoni unaotishia hatma ya elimu yetu. Tunaomba mamlaka husika zichukue hatua mapema kuisafisha chuo hiki ili kirudi kwenye mstari wa kutoa elimu bora. Nawasilia kwenu great thinkers.
 

Poleni kwa mikasa hiyo, naamini serikali imesikia na hatua iko mbioni kichukuliwa kuirekebisha chuo hicho.
 
Mimi nafikiria chuo hicho kingekuwa mfano wa kuigwa kwa kutumia jina la mwalim jk. Nyerere kumbe ni ubabaishaji tu ,jamaan wadau nusur elimu ya wanachuo hao
 
Mimi nafikiria chuo hicho kingekuwa mfano wa kuigwa kwa kutumia jina la mwalim jk. Nyerere kumbe ni ubabaishaji tu ,jamaan wadau nusur elimu ya wanachuo hao

Yaani muuliza mwanafunzi yeyote aliyesoma pale hiki Chuo ni balaa, sasa sisi tunaorudi tena pale sijui itakuwaje kama hapajarekebishwa.
 
hiki chuo hakina uongozi wa maana pale ni makada tu wamejaa na vyeti feki. Wapeleke mtu makini pale kama Prof. Maboko uone mabadiliko ndani ya kipindi kifupi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…