DOKEZO Serikali iko wapi masoko yanakuwa machafu kiasi hiki? Kipindupindu kitatuacha?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hali ya masoko kwa kweli ni mbaya sana, yaani unaweza kununua bidhaa ukaharibu viatu na ukapata magonjwa mazingira ya masoko yetu. Kila mfanya biashara analipa ushuru wa kuwepo sokoni, hata hivyo inashindwa kubainika hela zinatumikaje? Mbona masoko machafu hadi yanatia kinyaa, na mengine hutoa harufu mbaya kabisa.

Leo nimetembelea soko la Tegeta Nyuki aisee, sijui kama kipindupindu kimetuacha au kinatuvutia kasi tu. Maeneo machafu hata kutembea ni shida. Angalia kama hali ya wauzaji matunda hapa na hayo maji machafu ya pembeni.

Fikiria uchafu huo halafu bado tupo comfortable kununua bidhaa bila kujali afya zetu. Mimi nadhani ni wakati kwa wafanyabiashara kudai matumizi ya fedha za ushuru zinazolipwa kila siku.

Kwa sasa kasi ya magonjwa yasiyoambukiza pia iko juu, kwa uchafu huu magonjwa ya upumuaji yanakosekanaje maana kutakuwa na hewa nzito mfanyabiashara anaivuta kutwa nzima.
Hebu angalia kama hapo, mtu unapitaje, yaani unatoka sokoni kama umetoka shamba miguu imechafuka matope matupu.

Ni kweli tumeshindwa kutumia hela za ushuru kutengeneza mitaro vizuri ili mvua zisilete athari kwa kiasi hiki cha kuhatarisha afya za watu.

Tunasubiri kupindupindu?
Halafu unakuta wafanyabiadhara wanalipia ushuru wa taka.

CCM wapo bize kusaka dola kwa mtutu. Mambo ya maendeleo si kipaumbele chao
 
Mtu mchafu… hasafishi alipo Halafu tunaita serikali

This is too much

Kuna anahitaji serikali imfundishe usafi?
Tatizo Kuna ushuru unachukuliwa kwaajili ya kazi hiyo Sawa unaweza safisha mahali ulipo vipi kuhusu miundombinu ya maji taka iliyobomoka?
 
Wafanya biashara inabidi wajiongeze tuu kwa sababu ni wao watakao anza kupata madhara kutokana na huo uchafu masokoni, kusubiria serikali ya mboga mboga iliyojaa machawa na wapenda sifa ije ifanye jambo watajikuta wamekufa wote
 
Aiseee sio kwa uchafu huo. Hapo ukienda sokoni inabid uvae gloves, gumboot na mask. Na ukishanunua uloweke vitu uoshe na vinegar. Looh kweli jiji la dar linanuka
 
Hi nchi Chafu, na kitovu Cha uchafu ni Dar.

Pita mitaani utaona viroba vya uchafu, vinavyo kusanywa Kwa mwezi mara Moja, what do you expect!

Mitaani barabarani kula kwenye Kona, nguzo ya umems utaona mama ntikie, muuza matunda, au kakibanda uchwara, Hawa usafi huwa hauwahusu wanatupa kila kitu kwenye mtaro au barabara iliyombele Yao, what do you expect!

Juzi nimeenda Temeke Stereo, soko ni Chafu nikasema rabda ntarudi msimu wa kiangazi. Na watu wako na Furaha tu kuwa na uchafu hapo hapo anafaya biashara yake, utafikiri hawatoi ushuru.

Ni shida sana,
 
Aiseee sio kwa uchafu huo. Hapo ukienda sokoni inabid uvae gloves, gumboot na mask. Na ukishanunua uloweke vitu uoshe na vinegar. Looh kweli jiji la dar linanuka
Hiii sasa ni utumwa wa akiri kipindupindu haiwezi tuacha aslani😄
 
Serikali inakusanya kodi kila siku, na ni pesa nyingi sana; wana wajibu wa kurekebisha lile soko! Kwa hali ilivyo, hata kama wafanya biashara wangesema wasafishe hawawezi, miundo mbinu ni mibovu sana, panahitaji ukarabati wa uhakika, kisha viwekwe vifaa vya kuhifadhia taka, na wazoaji wapite mara mbili au tatu w siku kuzoa taka!
 
Soko la mabibo na ilala ndio balaa kwa mwezi haya masoko yanakusanya zaidi ya milioni 200 za ushuru wa soko na usafi ila ukifika utakuta taka zilizolundikwa zaidi ya siku tatu, matope mwanzo mwisho. Viongozi wa masoko wanaongoza kwa upigaji wa kodi za ushuru wa masoko zinazotolewa na wafanyabiashara. Utakuta kila siku wanatakiwa wapeleke gari 4 au tano za taka ila cha ajabu wanapeleka gari mbili tu,zile pesa za gari mbili wanafinya mpk kesho/kesho kutwa
 
Hali ya masoko kwa kweli ni mbaya sana, yaani unaweza kununua bidhaa ukaharibu viatu na ukapata magonjwa mazingira ya masoko yetu. Kila mfanya biashara analipa ushuru wa kuwepo sokoni, hata hivyo inashindwa kubainika hela zinatumikaje? Mbona masoko machafu hadi yanatia kinyaa, na mengine hutoa harufu mbaya kabisa.

Leo nimetembelea soko la Tegeta Nyuki aisee, sijui kama kipindupindu kimetuacha au kinatuvutia kasi tu. Maeneo machafu hata kutembea ni shida. Angalia kama hali ya wauzaji matunda hapa na hayo maji machafu ya pembeni.

Fikiria uchafu huo halafu bado tupo comfortable kununua bidhaa bila kujali afya zetu. Mimi nadhani ni wakati kwa wafanyabiashara kudai matumizi ya fedha za ushuru zinazolipwa kila siku.

Kwa sasa kasi ya magonjwa yasiyoambukiza pia iko juu, kwa uchafu huu magonjwa ya upumuaji yanakosekanaje maana kutakuwa na hewa nzito mfanyabiashara anaivuta kutwa nzima.
Hebu angalia kama hapo, mtu unapitaje, yaani unatoka sokoni kama umetoka shamba miguu imechafuka matope matupu.

Ni kweli tumeshindwa kutumia hela za ushuru kutengeneza mitaro vizuri ili mvua zisilete athari kwa kiasi hiki cha kuhatarisha afya za watu.

Tunasubiri kupindupindu?
Vipaumbele vyetu vipo wapi? Afya ya Watanzania ni moja ta kipaumbele chetu au upigaji kila mahali?

Mbona masoko yanaweza kuwekewa mazingira mazuri tu kama machinga complex.
 
Kwanini inawatoza kodi kama wanataka wafanye usafi wao? Hizo tozo wanazipeleka wapi? Kununua ma V8?
Mfumo wA uongozi wa soko ndio shida,Kodi wanakula na hawapangi watu ,wakupanga usafi,na Hilo soko linafaa livunjwe lote lijengwe kisasa,na pia serikali inatakiwa iwasimamie Viongozi wa mazingira bwana afya,na wizara ya ofisini ya makamu wa raisi na mazingira , kuhusu , kuweka sera ya usafi,.,... kiukweli majiji yetu ni machafu ,sanaa ,na Viongozi wetu wapo hii ni aibu Kwa taifa wakati wasomi wetu wa mazingira wapo wakutosha ,tunapaswa watanzania tuitunze nchi yetu na tutunze mazingira yetu yatutunze!!!!!
 
Hali ya masoko kwa kweli ni mbaya sana, yaani unaweza kununua bidhaa ukaharibu viatu na ukapata magonjwa mazingira ya masoko yetu. Kila mfanya biashara analipa ushuru wa kuwepo sokoni, hata hivyo inashindwa kubainika hela zinatumikaje? Mbona masoko machafu hadi yanatia kinyaa, na mengine hutoa harufu mbaya kabisa.

Leo nimetembelea soko la Tegeta Nyuki aisee, sijui kama kipindupindu kimetuacha au kinatuvutia kasi tu. Maeneo machafu hata kutembea ni shida. Angalia kama hali ya wauzaji matunda hapa na hayo maji machafu ya pembeni.

Fikiria uchafu huo halafu bado tupo comfortable kununua bidhaa bila kujali afya zetu. Mimi nadhani ni wakati kwa wafanyabiashara kudai matumizi ya fedha za ushuru zinazolipwa kila siku.

Kwa sasa kasi ya magonjwa yasiyoambukiza pia iko juu, kwa uchafu huu magonjwa ya upumuaji yanakosekanaje maana kutakuwa na hewa nzito mfanyabiashara anaivuta kutwa nzima.
Hebu angalia kama hapo, mtu unapitaje, yaani unatoka sokoni kama umetoka shamba miguu imechafuka matope matupu.

Ni kweli tumeshindwa kutumia hela za ushuru kutengeneza mitaro vizuri ili mvua zisilete athari kwa kiasi hiki cha kuhatarisha afya za watu.

Tunasubiri kupindupindu?
Uchafu Sokoni utaisha vipi wakati mnachagua viongozi waliokuwa wakichora kuta za vyoo vya shule kwa mavi ?.
 
Back
Top Bottom