Serikali ilikosea kujenga uwanja wa Mkapa Temeke. Hongera KMC kwa uwanja mpya, mpira umesogezwa kwa wastaarabu



Mtazamo wako ni wa kibaguzi. Tanzania haina sera ya kupendelea maeneo yoyote.

ndio maana hata mwendokasi ilianza kujengwa mbagala, gongo la mboto, njia ya manzese kote uswahilini


na makao makuu ya nchi yakapelekwa Dodoma sehemu ambayo kiasili ni masikini na kame,

hiyo ndio Tanzania tunayojua sisi, haipendelei, hainyimi, kulikobarikiwa kunabaki na baraka zake (mfano kaskazini, zanzibar, dar, mwanza, mbeya)
kwenye ufinyu kunanyanyuliwa (mfano dodoma, mtwara etc)

na hapo tanganyika packers panajengwa arena, unataka nini tena
 
hawakujui hawa temeke, wala hawajui jinsi chang'ombe kunavyofanana na upanga, wala hawajawahi paona kijichi kulivyo ushuani. hata uswahilini za temeke zinatengeneza pesa, mfano mbagala na tandika ni masoko makubwa ukitoa kariakoo, pesa inatengemezwa uswahilini temeke
 
Weka kumbukumbu sawa,mwendokasi ilianza morogoro Road 2012
 
Kiwanja kizuri ila kipo uswahilini sana hapo ukikaza tako ukatandika mkwaju wa nguvu mpira lazima uende chumbani/ chooni kwa mtu kazi inaanza kuutafuta.
 
Mkuu umeongea ukweli yani tuna viongozi wajinga kweli. Mfano Azam sijui nani aliwashauri wakajenga uwanja uswahilini uko, wangeongea na Serikali naamini wangepewa eneo mjiji maana serikal ina maeneo mengi ya wazi mfano uwanja wa kinesi. Viwanja Ukwamani, Biafra Kinondoni
 
Maeneo yapo tu kwa kweli inafikirisha sana,tena hapi biafra pako centre kabisa,panafikika kirahisi toka pande zote za mji,mtu hawezi toka kibaba kwenda chamazi kuangalia mechi
 
Hili ndio swali la msingi analotakiwa kusema

Utakwambia masaki.
 
Hivi siku hizi wahindi wanajenga bongo?
Maana nasikiaga wao wanapangaga Nyumba za NHC au Apartment kujenga no!!!
Si nyumba peke yake. Hata viwanda hawajengi. Viwanda wanajenga wabongo. Wabongo ndiyo wawekezaji wakubwa wa viwanda. Just confirm na TIC!
 
Ona hili nalo hivi kwanini wanajamii forum mnapenda sana kufake life hili linasema halipo Tanzania kwamba lipo Washington DC lakini linavyochati tu linaonesha lipo tandale
Ha ha ha ha. Tandale ni mji gani tena? Kuna sehemu inaitwa Tandale karibu na Sinza. Watu wa Tandale hawatakiwi kwenda Washington DC. Wakienda huko wanatakiwa wasahau mambo ya kule Tandale walikozaliwa kwa sababu ya Uzungu wao siyo! Hata wale waliozaliwa pale kama Diamond.
 
Nakubali Wakorowaitu Rutashobya.
 
Mechi ya mwisho kutazama live kwa mkapa ni ile Simba alimfunga Yanga 5-0.
 
Ni kweli mkuu.

Changombe ili kuwa planned kuishi watu wa middle class.

Mpaka leo panaonekana palivyopangika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…