nasrimgambo
JF-Expert Member
- Jan 10, 2017
- 1,902
- 2,488
Mpaka leo sijui nani alisema uwanja wa Mkapa ujengwe Temeke jirani na uwanja wa Uhuru zamani Taifa.
Haikuwa sahihi kurundika viwanja viwili vikubwa sehemu moja, hatuna uhaba wa ardhi nchini,
Uwanja wa Mkapa ungejengwa Tanganyika Packers kwa Mwamposa.
Mimi binafsi huwa naenda uwanja wa Mkapa kwa matukio muhimu ya kiserikali, mechi ya mwisho na mwanzo kwenda ilikuwa Simba na Yanga ile sare ya 3-3 miaka takribani kumi.
Temeke kuna wahuni wengi sana na hawana uwezo kiuchumi, siwezi kutoka Ununio eti niende Taifa kuabgalia mechi ya Simba na Namungo.
KMC wametufungua macho, mpira sasa unapendwa na kada zote,wastaarabu na wasomi.
Uwanja wa KMC hata mechi ndogo ukiweka kiingilio cha 10000 unajaa.
Pia soma: Mapato ya uwanja wa Benjamini Mkapa ndiyo kikwazo kikubwa kwa mapacha wa Kariakoo kujenga uwanja wao
Jimbo la Kawe na Kinondoni ndio majimbo ya watu wenye uwezo hapa Daslam na Tanzania kwa ujumla. 10,000 kwa wakazi wa Temeke ni hela nyingi mno.
Hongera KMC, nawasihi Simba msirudi kwa Mkapa labda kwenye derby tu.huo ndio uwe uwanja wenu, kwanza Mwenge na Bunju sio mbali.
Haters mpooo
Mtazamo wako ni wa kibaguzi. Tanzania haina sera ya kupendelea maeneo yoyote.
ndio maana hata mwendokasi ilianza kujengwa mbagala, gongo la mboto, njia ya manzese kote uswahilini
na makao makuu ya nchi yakapelekwa Dodoma sehemu ambayo kiasili ni masikini na kame,
hiyo ndio Tanzania tunayojua sisi, haipendelei, hainyimi, kulikobarikiwa kunabaki na baraka zake (mfano kaskazini, zanzibar, dar, mwanza, mbeya)
kwenye ufinyu kunanyanyuliwa (mfano dodoma, mtwara etc)
na hapo tanganyika packers panajengwa arena, unataka nini tena