Tusiwe na rigid mind kiasi hiki. Eti tuogope kuzuia bodaboda kuingia mijini kisa tu vibaka wataongezeka, kuna shughuli nyingi sana binafsi za kufanya sema tu sisi hatuna akili na akili zetu ni mgando sana kuwa bila kuuza mitumba , bila kuingia mjini na boda, bila kuuza chips hakuna kingine cha kufanya.
Halafu sio kila kitu Serikali inahusika kuandaa maana naona kila changamoto ni kuilaumu Serikali, HATA MWANAO AKIVUTA BANGI UNAILAUMU SERIKALI.
Tujiulize Diamond, Ali Kiba, Mwijaku, Ndaro , Steve, Dr Cheni, Samata , Msuva, Mzize waliandaliwa mazingira gani na Serikali. Huo ni mfano tu, lakini wapo wafanyabiashara, wakulima na wasomi ambao wamejibeba wenyewe . KUNA MAMBO YA SERIKALI KWELI LAKINI MENGI NI AKILI NA STRUGGLING YA MTU BINAFSI.
SASA TUKIWA NA RIGID MIND KAMA HIZO TUNAZIDI KUDUMAZA WATU WETU HASA VIJANA NA KUCHELEWESHA MAENDELEO.