Serikali imeamua kuua huduma za miamala ya simu

Serikali imeamua kuua huduma za miamala ya simu

Kutuma Tshs 300000
Ada ya mtandao Tshs 1500
Tozo za serikali Tshs 3500
JUMLA TSHS 5000

Kutuma Tshs 300000 mtandao tofauti
Ada ya mtandao Tshs 2300
Tozo za serikali Tshs 3500
JUMLA TSHS 5800

Kutoa Tshs 300000
Ada ya mtandaoTshs 6500
Tozo za serikali Tshs 3500
JUMLA TSHS 10000

Ukweli ni Kwamba hapa serikali imeamua kuua miamala ya kuweka na kutoa kupitia makampuni ya simu Kwa sababu inakuwa haina faida Kwa mlaji ila ni hasara

Na pia inasikitisha Kama viongozi wanao ongoza serikali yetu pendwa ya CCM wanaamua kutuletea wananchi wao kitu Kama hichi Kwa kweli inasikitisha sana

Au Kwa sababu wanatumia kodi zetu kununulia magari mazuri ya kutembelea na kulipana mishahara na malupulupu ya kiwango kikubwa ndio Wanahisi Kwamba Watanzania wanaishi maisha mazuri

Sitaki kuamini Kama viongozi wetu ndio wameishiwa mbinu za kuongoza nchi kiasi hiki
Mama kamsikiliza Lameck.. Itakula kwake.. Angejua ana magoli ya mbali kamwe asingekubali huu ujinga
 
Ni miezi 4 imepita tangu tulipolalamika bando kupanda na serikali ikaingilia kati. Leo hii serikali hiyo hiyo, inabariki makato makubwa bila kujali maumivu anayopata mtumiaji.

Yaani kutoa Tsh 10,000 unakatwa 1,800? kuna haja gani sasa ya kutumia mobile money? Serikali imechemsha big time[emoji2959][emoji2959][emoji2959][emoji2959]
 
Tufanyaje mkuu kuepuka hilo?
Ni kuongea na wakala akutumie pesa yako moja kwa moja kwa wakala mwenzie wa mahali unapotaka pesa yako ifike mkatie wakala anaetuma 500 na yule wakala anaetoa cash mwambie akate 700 mchezo unaisha kwa makato ya 1200
 
Mkuu..wenye mabank walienda ililia serikal kwamba makampun ya simu yamechkua kaz yao ya kuhifadh pesa...maana weng skuhiz kuanzia 5m kushuka chini wanahifadh kwenye simu....na ndo asilimia karib 90 ya wa Tz wanacheza humo...

Bank zilikua zinakufa...na bank zikifa manake bank kuu kwisha...

So watu wa mabank walilia vyakutosha kuwa kama maamuz magum hayatofanywa basi bank zinakufa zote....

Ndo ikabid ichezwe karata hyo

Hahahaha
Takukuru wawachunguzi wamiliki wa mabenk na Mwigulu

Hu sasa ni mwaka wa 15 tokea tuanze kutumia mobile money mbona hayo mabenk hayajakufa?

Mbona mwaka Jana NMB walitangaza wamepata faida kubwa sana

Bank kuu haiwezi kufa hata hizo pesa za mobile money zinakaa bank kuu watumiaji wanakaa na namba tu katika simu zao na ndio maana kuna magawio huwa yanatolewa kwa wanao tumia mobile money

Yani bank kuu wamezifanyia biashara hizo pesa faida iliyopatikana ndio wanagawa gawio



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Subiri bi mkubwa atoke safarini atafanya kama kwenye mabando mkuu
 
Sikuwahi kutegemea kama jamaa ni kilaza kiasi hichi

Eti na yeye ndio alikuwa anataka uraisi

Hivi kama ni kweli alisoma uchumi na akaelewa ina maana yeye anaamini kweli kwa makato haya miamala itakuwa mingi ili na serikali ipate hayo mapato mengi

Maana Leo tu mamilioni ya wananchi wameshaacha kutumia mobile money

Inawezekana amepokea fungu kutoka kwa mapepari wa mabenk na huo ni ufisadi

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni umbwaaa kabisa huyu jamaa
 
Back
Top Bottom