Serikali imeamua kuua huduma za miamala ya simu

Mama kamsikiliza Lameck.. Itakula kwake.. Angejua ana magoli ya mbali kamwe asingekubali huu ujinga
 
Ni miezi 4 imepita tangu tulipolalamika bando kupanda na serikali ikaingilia kati. Leo hii serikali hiyo hiyo, inabariki makato makubwa bila kujali maumivu anayopata mtumiaji.

Yaani kutoa Tsh 10,000 unakatwa 1,800? kuna haja gani sasa ya kutumia mobile money? Serikali imechemsha big time[emoji2959][emoji2959][emoji2959][emoji2959]
 
Tufanyaje mkuu kuepuka hilo?
Ni kuongea na wakala akutumie pesa yako moja kwa moja kwa wakala mwenzie wa mahali unapotaka pesa yako ifike mkatie wakala anaetuma 500 na yule wakala anaetoa cash mwambie akate 700 mchezo unaisha kwa makato ya 1200
 
Takukuru wawachunguzi wamiliki wa mabenk na Mwigulu

Hu sasa ni mwaka wa 15 tokea tuanze kutumia mobile money mbona hayo mabenk hayajakufa?

Mbona mwaka Jana NMB walitangaza wamepata faida kubwa sana

Bank kuu haiwezi kufa hata hizo pesa za mobile money zinakaa bank kuu watumiaji wanakaa na namba tu katika simu zao na ndio maana kuna magawio huwa yanatolewa kwa wanao tumia mobile money

Yani bank kuu wamezifanyia biashara hizo pesa faida iliyopatikana ndio wanagawa gawio



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Subiri bi mkubwa atoke safarini atafanya kama kwenye mabando mkuu
 
Ni umbwaaa kabisa huyu jamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…