Serikali imeanza kuhakiki mkataba wa bandari ya Bagamoyo


JF Ina watu wengi sana tunafanya kazi sehemu mbalimbali na usiongee kitu kama hujui tafadhali. Wengine wapo kwa AG wengine ni wanasheria wa makampuni binafsi hivyo huwa tunapata access ya hizi documents Ila hatuwezi kuongelea kila kipengele. Wanaojua wamekaa kimya maana mlishaamua kuongea Ila mradi itajengwa tu.

Kimsingi, mkataba upo stage ya negotiation na hizo ni proposed clauses za wachina na kiufupi Ila draft contract Ina page zaidi ya 1000 kijana usiandike kitu hujui.

Pia fahamu kwamba hizo propositions ni kawaida kwa mfanyabiashara maana hajaja kutangaza dini hapa kwetu yeye anatumia hela apate faida so mianya kama hii akipenya anajua ana uhakika wa kumaximize profit.

Wao walitaka mambo mengi mno nashindwa hata kuelezea ikiwemo suala la tax holiday sio wasilipe Kodi acha kudanganya. Hata hiyo ilishakataliwa wakati wa majadiliano sababu hata kisheria tax holiday ilishafutwa.

Walitaka pia kuwa na port charges zao kitu ambacho kilikataliwa kwakuwa Bandari zote nchini wanatumia tarrif rate moja tu za kwenye bahari kuna tarrif zake na maziwa Wana tarrif zao.

Pia walitaka Bandari nyingine isijengwe kuanzia pangani hadi Mtwara ili waweze kurudisha pesa yao kwa wakati uliopangwa kwa kuwa Ile Bandari tumeingia concession agreement kwa miaka 33 na ikiisha wanatuachia ingali bado watakuwa wanatupatia gawio kwa kuwa tunaform kampuni yetu itakayoingia ubia katika uendeshaji wa Ile Bandari hivyo tutagawana mapato kulingana na share capital tuliyoinject.

Haya mengine hayapo ni wazimu wa Magufuli tu hii nakueleza mie sipendi tudanganye sana kuhusu huu mradi maana kila mtu anakaza shingo sana tunasahau huu mradi utaajiri watu zaidi ya 12,000 direct employment na watu zaidi ya 200,0000 watapata indirect employment kwa kuajiriwa kwenye mahoteli yatakayojengwa kule ili watu wanaotoa mizigo wapate malazi, chakula transportation nk.

Mradi utaunga na kuzindua special economic zone (SEZ) ambayo Kuna eneo limetengwa la viwanda kwa sababu ya Ile Bandari itakuwa free port. Tafuta maana ya free port sio kwamba hulipi.

Kuna airstrip itajengwa, reli itajengwa kuiunganisha Bandari na reli ya Kati pamoja na Tazara hivi kwa nini mnapinga huu mradi????????? Hawa watu wana shida gani? Kisa Magufuli aliukataa??? Yule alikuwa na ishu zake ndio maana aliuchafua na wajinga wanamuona kama Mungu.

Magufuli aliukataa sababu kwenye kutengeneza kampuni inabidi serikali itoe hela kama share capital ili tuchangie sababu wao walitaka waendeshe wenyewe sisi tukasema hapana tukisubiri Kodi pekee siku tukikabidhiwa huu mradi tutashindwabsababu tutakuwa hatujajiweka tayari kuendesha so tukaamua iwe formed kampuni ili tuweke watu wetu nao waingie kwenye management.

Magufuli aliona pesa inayotakiwa ni nyingi akaamua kutoa visingizio vya kijinga sana na alikataa alisema sisi tuna ardhi kwa nini tutoe hela

Sasa ndugu zangu hata kama una ardhi ukitaka kukodisha hakuna shida Ila ukitaka na kuingia ubia upate gawio lazima utoe pesa otherwise subiri Kodi ya pango.

Mambo ni mengi sana Ila kuna watu tunaufahamu vizuri huo mchezo wa hapo sehemu.
 
Hela uliyowapiga wachina uje kutetea bandari yao hapa ni bora uwarudishie tu maana hakuna unachofanya.

Ujinga mtupu
 
Kimsingi, mkataba upo stage ya negotiation na hizo ni proposed clauses za wachina na kiufupi Ila draft contract Ina page zaidi ya 1000 kijana usiandike kitu hujui.
Unaposema "proposed clauses" ndiyo hiyo niliyoita/ inayoitwa Framework Agreement... huu sio mkataba!

Kwamba "Hizo ndo proposed clauses" unatakiwa kutaja ni zipi!!

Mimi nimezungumzia KODI, na nime-specify aina ya kodi ambazo Wachina and any other businesses huwa wanaomba kusamehewa lakini SIO KODI ZOTE... HAKUNA KITU KAMA HICHO!
Pia fahamu kwamba hizo propositions ni kawaida kwa mfanyabiashara maana hajaja kutangaza dini hapa kwetu yeye anatumia hela apate faida so mianya kama hii akipenya anajua ana uhakika wa kumaximize profit.
Sasa si ndicho nilichosema, au?
Wao walitaka mambo mengi mno nashindwa hata kuelezea ikiwemo suala la tax holiday sio wasilipe Kodi acha kudanganya. Hata hiyo ilishakataliwa wakati wa majadiliano sababu hata kisheria tax holiday ilishafutwa.
Hivi ulikuwa unanijibu mimi, au?!

Nimesema wasilipe kodi au nimesema Wachina kama ilivyo kwa other businesses, WANA KAWAIDA ya kuomba Msamaha wa Income Tax? Na suala lingine la kodi, nikasema kuna kodi zingine hadi kesho huwa tunasamehe kwa sheria zetu wenyewe!
Walitaka pia kuwa na port charges zao kitu ambacho kilikataliwa kwakuwa Bandari zote nchini wanatumia tarrif rate moja tu za kwenye bahari kuna tarrif zake na maziwa Wana tarrif zao.
Nimezungumzia masuala ya kodi na sio charges!!

Hata hivyo, hivi sasa kuwa na rate moja haiwezi kuwa hoja ya msingi kwa sababu as of now, operator ni mmoja! A moment tukishataka kuwa na multiple operator, hatuwezi tena kuwabana kuhusu same charges kwa sababu hapo inakuwa ni biashara huru!
Halafu hivi tangu taifa lipate uhuru miaka zaidi ya miaka 60 iliyopita, TZ tumewahi kujenga bandari ipi?! As far as I know, hata bandari tulizokuta zingine zimeshakufa na zingine zinapumulia mashine lakini leo hii suala hili linaongewa sana... all in all, it's just a proposal, na hakuna mjinga anayeweza kusema we'd accept all proposals!

Only the dead can do that!
Na kwa mchumi hayo ndo ya msingi zaidi kuliko hoja nyingi ambazo zimekuwa zikitolewa kama vile ardhi wakati tayari kuna watu wamemilikishwa ardhi kwa miaka 99 wakati tija kwa taifa toka kwenye ardhi husika hakuna!
Yote hayo nishaeleza sana huko nyuma ndo maana nikahoji hivi unaniuliza mimi, au?!
Hivyo ni visingizio vyake tu.. hivi unadhani Bagamoyo ingekuwa ndo Chato hayo ya share capital yangetokea?! Tatizo lingine la Magu ndo ile ya kutaka kujifanya yeye tu ndio msafi lakini wenzake wote ni wezi!

Matokeo yake, ndo kama ilivyokuwa SGR! Mwanzoni kawapiga chini Wachina, watu wakashangilia kwelikweli! Sie wengine tukasema wazi hapa Mturuki HANA pesa iliyo available kwa mradi mkubwa kama huu, na hasara yake ni kwamba mradi unaweza ku-delay!

What happened... baadae tukarudi kwa Mchina yule yule ambae plan ya mwanza ilikuwa ni more strategic kwa sababu a huge SGR Investment ingekuwa utilized na bandari! Leo hii sijui tunaratajia kui-utilize na nini!
 
Mkataba upi tena jamani? si kuna mheshimiwa alisema hapakuwa hata na mkataba?!!!
 
 
Mchina anajenga Isaka - Mwanza na Mturuki anajenga Dar - Tabora
 
Huyu mama tangu aseme wale kwa urefu wa kamba zao simwamini tena, labda kama alikuwa anamaanisha kitu kingine na sio ninachofikiria
Kama umefungiwa kamba ya mita mbili kuzungukia chumbani mwako tu, acha wenzio waliofungwa na kamba za kilomita elfu na mia tano watakula shamba lota toka dar mpaka Bukoba na kuzungukia nchi nzima. Il kamba ya mama mwenyewe ndiyo hatujui ina urefu gani.
 
[emoji1787][emoji1787]
 
Commercial base ndiyo nini?
 
WATANZANIA tutafika mbinguni ama jehanamu tumechoka Sana [emoji31]

hivi nani alisema au kuleta neno lawanadamu kwenda mbiguni hakuna binadamu atakaenda mbinguni mambo yote tutahukumiwa hapahapa
 
Kabudi lazima atoe mimacho yake kwenye mapitio ya huo mkataaba..mana ndio kiongozi wa timu ya mikataba.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app

sasa nimeelewa kabudi kawekwa kwa ajili ya mkataba wa bandari ya bagamoyo utaukubali na kuusapoti na nafikiri atajitoa ufahamu kuelezea kuwa makufuli alipotoshwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…