#COVID19 Serikali imeanza kulazimisha watu kuchanja chanjo za COVID-19?

Shida ya vitu vya bure ndio hiyo, hapo unaweza kukuta aliambiwa lazima ziishe ndio apewe msaada mwingine
 
Huyu amechemsha kabla ya kuanza!! Ila anasema watahamasisha, hajasema watalazimisha!! Akitaka aiombe serikali itoe waraka rasmi wa kulazimisha!! Kitu ambacho hakiwezekani!! Huo mtiti hauwezekani kabisa!! Mkuu wa mkoa si mtunga sera, bali ni msimamizi mkuu wa sera zinavyotekelszwa katika mkoa wake na anapimwa kwa hilo!!
Kwa hiyo anapaswa ahakikishe uchanjaji wa hiari unafanyika mkoani mwake!! Watu wasipochanjwa kwa hiari aachie ngazi au Raix amtumbue!! Akijaribu kulazimisha pia atumbuliwe!!
 
Bi mkubwa.kule UN alihimiza chanjo asije kuwa katoa magizo watumishi wachanjwe??

Mi nshatangaza na narudia tena SICHANJWI!!!!
 
Ila hali ngumu, maana juzi Msigwa kasema laki 4 tu ndiyo wamechanja, lakini dsm tu kuna watu karibia laki 5.....bado mwamko ni mdogo sana
Johnson Unachoma Mara Moja Inakaribia Kuchacha Kutokana Muda. Sasa Mzigo Mpya Kutoka China Million 2
Naona Viongozi Wanatweta Wamekosa Ubunifu


Baadaye Tutaambiwa Kuchanja Kwa Virungu
Jiwe Alisema Bwana Bure Hayupo
Sasa Mabeberu Wametoa Cash Wanataka Mrejesho
 
Msihofu Mungu yupo imewashinda kulazimisha barakoa,watu kujazana ije kulazimisha kuchanjwa?
Nani huyo Yuko wapi? Kwa Sheria ipi? Maana mgonjwa mwenyewe Ana haki zake,sembuse mzima?
 
MKUU wa MKOA wa MBEYA ametangaza Chanjo ni Nyumba kwa Nyumba
 
Ikibidi iwe lazima kuchanja Ili tusiambukizane na tusiendelee kuwa kwenye red line afu uchumi wa nchi unaanguka.
 
Huyu pumbavu anaropoka nini? Matibabu Ni hiyari ya mgonjwa siyo lazima,mbona viongozi wetu mnatutia Shaka juu ya uadilifu wenu.tukisema Kuna kitu kinaendelea nyuma ya pazia tutakosea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…