Serikali imechelewesha mishahara au haina pesa?

Hela za kulipa mishahara zitatoka wapi!, Wakati zinaelekezwa Zanzibar kupitia kuilipia mikopo yake inayokopwa bila utaratibu.
 
TUCTA wao ni akina nani hadi watubadilishie tarehe ya mishahara yetu?
Hawa si ndo walituletea kikokotoo? Toka tarehe 23/05 hadi tarehe 309/06 ni siku 38 badala ya siku 30 za mwezi
 
Watumishi mmezidi sasa kulalamika. Subirini mtalipwa. Kwanza hata hivyo shukuruni serikali inawasaidi kupunguza matumizi kwa kuendelea kuwahifadhia hela zenu.
We hujui watu walivyo pambano hadi kupata sifa za kuajiriwa! Siyo upendeleo. Wengine tumeajiri wa kipindi ikikataa kwenda kufanya kazi serikalini, unashitakiwa kwa kukiuka mkataba!
Leo akina Madelu wanatuwekea tu vikokotoo na kutufanya wapendavyo!
Hadi tunajuta kuajiliwa na serikali kipindi hicho!
 
Awamu hii majizi yanakwiba bila ya hofu.Hakuna wa kuwagusa.
 
Hapo usikute wewe ni mwandishi wa gazeti la The Guardian ambao hamjalipwa kwa miezi 3 mfululizo, lkn hamuuandiki habari aenu
 
Mwezi huu tutawakopa..tutawalipa mwezi ujao..
 
Niliacha kulala na mafaili Nina stress
 
Wenye akili hata hawawazi kuhusu mshahara kwasababu wanajimudu hata bila mshahara
 
Dah mshahara kuchelewa imekuwa nongwa, na kazi mngekuwa mnapiga kwa bidii hivi hivi tungekuwa mbali sana
 
Wenye akili tulijua Serikali ya Awamu ya Sita itakwamia hapa!!

Nchi imekabidhiwa Kwa wezi ambao Kila jambo wanapiga!!

Sakata la Sukari limewavua nguo. Hela hakuna tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…