Serikali imefanya kweli kwenye kilimo, Vijana waanza mafunzo

Serikali imefanya kweli kwenye kilimo, Vijana waanza mafunzo

kalacha mateo

Senior Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
119
Reaction score
240
Baada ya kuchaguliwa vijana 812 wa awamu ya kwanza kwenda kwenye mafunzo ya kilimo, Leo kazi imeanza kwa mafunzo ya uandaaji na uzalishaji wa miche katika kituo atamizi cha Bihawana jijini Dodoma. Serikali inakusuidia kutengeneza ajira milioni tatu za vijana na wanawake kupitia kilimo ifikapo mwaka 2030.

Aidha serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu inaboresha sekta ya kilimo na kutatua changamoto za kilimo ili kuwavutia zaidi vijana kwenye kilimo. Serikali inatoa umiliki wa ardhi kwa kipindi cha miaka 66 ikiwa ni sehemu ya mtaji baada ya kumaliza mafunzo hayo.

Imani ya serikali nguvu kubwa ya vijana na wananwake ikienda shambani basi Taifa litazalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya taifa, Afrika na Dunia.
Fr5mhPDWYAAbR3x
Fr5mhO5WIAEq3ds
 
Mabadiliko makubwa katika kilimo yatatokea kwa uboreshaji wa miondombinu ya barabara za lami na umwagiliaji vijijini.
 
Ili kutengeneza hizo ajira 3,000,000 hadi kufikia 2030 inabidi kila baada ya miezi 6 waajiriwe vijana walau 214,000. Serikali imeanza na 812.

Nitaandika tena nikikumbuka jambo.
 
Hapo bado sana maana naona hao vijana sio wahusika, si wapite hata huko sehemu mbali mbali kuna vijana wenye mioyo ya kilimo na wana idea kubwa zaidi uwezeshaji tu hawana
 
Vijana wa uvccm hao,project imekaa kisiasa zaidi,soon wahuni watagawana mbao,ikitoboa 2024,muje muongee.
 
Back
Top Bottom