Ungeuliza badala ya kutoa opinion zako.
Ni hivi mwaka wa fedha wa serikali unaanza tarehe 01/07 na kuisha 30/06 kila mwaka.
KINACHOTOKEA
kwa kuwa mwaka wa fedha unaanza tarehe 01/07 na kwa kuwa mfumo wa malipo wa serikali hasa LGA's yaani Epicor 9.05 upo centralized kinachofanyika kwa muda huo kuanzia tarehe 01/07 linafanyika zoezi la ku-upload budget za LGA's zote na kumbuka ni karibu 185. utaona mwenyewe ni namna gani zoezi hili lilivyokubwa na lenye kuhitaji umakini, kumbuka baudget inaingizwa kwa govenment financial statistics code (GFS code) yaani kila Tshs inaingizwa kwenye kifungu husika.
Kwa sababu hiyo ndio maana malipo kwa sasa kwa LGA's yamesimama lakini pia kumbuka yamesimama kwa zile hatua zinazohitaji kufanya kwa mfumo na kwa sababu malipo ni process, bado kuna hatua nyingine za malipo kama vile kuinitiate madokezo kunafanyika wakati wakisubiri budgeti iwe uploaded kwenye mfumo wao wa epicor 9.05.
Kuhusu Lawson na mifumo mingine inayotumia infrastructures za Epicor 9.05 inaweza kuathirika kwa namna moja au nyingine kwa kuwa wakati huu pia TAMISEMI inaweza ikawa inafanya maboresho au marekebisho kwenye miundo mbinu ya mifumo mfano Servers updating, upgrading....etc
Zoezi hili huwa ni la kila mwaka hivyo halina uhusiano na utawala uliopo.
TATIZO LINAWEZAJE KUEPUKIKA
Tatizo kama hili linaweza kuepukika ikiwa kunaweza kukawa na mifumo miwili inayofanana but tofauti in physical device katika hatua za mwanzo kama stand alone system them zinaweza pandishwa kwenye server usiku wa tarehe 30/06 Kila mwaka ili tarehe 01/07 asubuhi kusitokee namna yoyote masuala ya malipo yakasimama.
Nadhani Mtoa thread utakuwa umepata japo kwa kiasi.