Serikali imeishiwa haina pesa za mishahara

Mzee Wangu unajua wafanyakazi wa serikali hawajalipwa leo mwezi wa pili, sasa hiyo nyongeza inaongezewa wapi?

Mzee ES, hizo habari umezitoa wapi mwenzetu?? Wafanyakazi wa serikali wanatoa nje!!!
 

Maneno hayo hapo juu niliyaweka katika ile thread ya majambazi wa Arusha, hivi haina uhusiano na ongezeko hilo la Mishahara? Tukumbuke hata polisi nao walikua wakisubiri ongezeko la mishahara. Sasa wameridhika?

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=3935&page=2
 
...JF ni baraza haswa!

...maneno ya kizushi kibao!

...si hoja lakini,baada ya siku ukweli utafahamika!
 
Vijana mwishoni mwa mwezi wa Tano, serikali ilitoa waraka katika Government Gazzette, kusitisha uajiri mpya ndani serikali, mishahara, na uhamisho kwa wafanyakazi wake hadi itakapofikia mwezi huu wa nane, baada ya bajeti kupita, kwa mfano katika kipindi hicho ni maofisa wa UN ndio walioruhusiwa kuhama kutokana na umuhimu wao huko nje, lakini wengine wote ndio kwanza wameanza sasa kuhama,

Wizara na mashirika ya umma, hupewa mgawo wake wa mwaka mwezi wa sita, ambao unategemewa kuwaendesha hadi mwezi wa sita mwingine, sasa serikali ikisema haina hela haina maana wizara hizo na mashirika yote yatakuwa yameishiwa pesa, NO! kutakuwepo na hela za hapa na pale, kama hazikuibiwa ndizo zitawashikiza kwa mishahara hadi serikali itakapotoa hela za mwaka, lakini yes kutakuwa na wizara ambazo zitakuwa zimeamliza kabisaa mgawo, na this time moajwapo ya wizara hizo ilikuwa ni foreign, in the last two moths karibu all financial movemments zilikuwa frozen,

Wakati wa enzi za Mwalimu, na Mwinyi, haya yalikuwa ni mambo ya kawaida, tena enzi za Mwinyi, kuna wakati ilikuwa inaweza kwenda hadi miezi sita bila mshahara, sasa kipi cha ajabu this time around?
 
Kuna habari za kutia moyo, ila sijui ni kwa kiwango kipi.. tafadhali soma hapa chini:
Source link: Daily News.

Je, habari hizi zimetolewa hivi sasa kwa ajili ya kutuliza vuguvugu lililopo nchini, haswa kuhusiana na Buzwagi?!

SteveD.
 
Kuna habari za kutia moyo, ila sijui ni kwa kiwango kipi.. tafadhali soma hapa chini:

Source link: Daily News.

Je, habari hizi zimetolewa hivi sasa kwa ajili ya kutuliza vuguvugu lililopo nchini, haswa kuhusiana na Buzwagi?!

SteveD.

Hilo mojawapo na jingine ni kwamba wafanyakazi walikuwa wameshatoa tishio la mgomo wa nchi nzima. Kwa maoni yangu kima cha chini inabidi kiwe uniform nchi nzima kama ni shilingi 350,000 basi ni nzima ili kuwawezesha kumudu gharama za maisha. Sijui reaction ya chama cha wafanyakazi itakuwaje kufutia tangazo hili la sirikali.
 

Kima cha chini kwa mwezi miye nafikiri kinamaanisha kuwa: ni kima cha pesa ambacho Mtanzania yeyote inabidi awe nacho ili kukidhi maisha ya chini. Maisha mengine yoyote yale yatakayo tegemea kiasi chini ya hicho ni "maisha ya chini ya kima cha chini". Bubu, 350,000/= kama unavyosema ni lazima iwe ya Watanzania wote, na juu ya hapo basi itagemea wale wasemayo, kama vile utaalam, uzoefu, umaridadi, sekta n.k.

SteveD.
 
Admin,
Samahani, naona kuna alert ilishawekwa na Mkjj kuhusiana na hili, sikuweza kuona wakati naanzisha thread, hivyo basi naomba uinganishe hii kwenye ile kama hilo litafaa. Ahsante,

SteveD.
 
Mimi nadhani kuna haja ya wachumi kufanya utafiti kuhusu athari za kiuchumi. Kupandisha mishahara kwa kuwalazimisha sekta binafsi without creating the right business environment ni bure. Owner wa daladala atawalipa kweli kila dereva na konda 200,000 tshs each?! Kwa hela na faida gani anayopata? Result itakuwa nini? Kupandisha nauli! So we can expect massive inflation. Mimi siyo mchumi lakini naomba msaada wa mchumi ambaye pia anaweza kueleza zaidi kuhusu free market economy and how market forces work. Let us be realistic badala ya kushabikia! The business community in Tanzania is primarily made up of middle and small scale businesses who have to make a profit! By saying that they should dole out more money in salary it will result in people being fired and the remaining working 2 or 3 times more! Mi naona serikali hii imepanic kwa sababu ya kutishiwa mgomo, but they just looking at a very short term solution. Kama ni hivyo wapunguze corporate tax from 30% to 20% kama Uganda na Kenya! Also provide more conducive environment for businesses siyo TRA wanakuja wanataka hongo, customs wanataka kitu kidogo! Come on! Pushing responsibility to the private sector is not the solution!
 
Mimi sielewi kitu, please nielewesheni. Hapa salary iliyotangazwa inahusu private sector, vipi kuhusu serikalini?
Mi nilidhani wanapandisha kima cha chini kwa wafanyakazi wote hata serikalini ndo iwe hiyo 350000. So walimu, madaktari nk wataendelea kusota?
 
viongozi wa type hii,mie sijui tutafika wapi?huku ndio kujikosha kwa fisadi namba moja aliyemaliza safari zake juzi hapa,
mbona kima cha chini cha serikali hakiongezwi..?
 
kwanini karamagi bado anaendele akuwa WAziri?
kwanini Msolla Bado hajang'oka?
kwanini batlida Burtiani hajafukuzwa ofisini,
Kwanini EL anendelea kutuibia?
Kwanini Balali anaendelea kukaa Madarakani?
kwanini bei za matuta ziko juu?
Kwanini mafisadi hawajachukuliwa hatua?
kwanini Takukuru wanag'ang'ania kuchunguza tuhuma za buzwagi?
kwanini maisha ni magumu?
kwanini nchi inaongozwa na Wasanii??
why?
why?
tafakari ,chukua hatua
 

Na nnji hii inakuwa nyuma kwa sababu kila kitu ni wao wao wao wao, serikali, serikali serikali, siasa, siasa, siasa! hakuna siku unasema mimi,mimi, mimi, au sisi, sisi, sisi, sisi!!!

Nalinganisha na vita zidi ya Ukimwi, kila mtu anamunyooshea kidole mwenzake, yeye hapana,,, hili ni tatizo letu sote, maisha magumu ni matokea ya mambo mengi kwa miaka 40-50 iliyopita sio JK na EL, sitakiamini hivyo hata siku moja hadi nitakapozikwa kaburini!

Having said so!

Sitetei Uharamia!
 
Posted Date::10/9/2007
Nyongeza mishahara yaibua mjadala wananchi wahoji vigezo
Na Waandishi Wetu
Mwananchi

ONGEZEKO la mishahara kwa wafanyakazi wa sekta binafsi lililotangazwa na serekali juzi, limezua mjadala mkubwa miongoni mwa wananchi na vyama vya wafanyakazi wakihoji utelekezaji wake.

Wameshangaa hatua ya serikali kupandisha kima cha chini ya wafanyakazi wa ndani kuwa Sh65,000 huku wafanyazi wa serikali wakilipwa Sh84,000, kwa mwezi.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafanyakazi Nchini (Tucta), Nestory Ngula alisema ni hatua nzuri kwa serikali, lakini ana wasiwasi na utekelezaji wa ongezeko hilo la mishahara.

"Hatuna uhakika kama serikali itaweza kutekeleza sheria hiyo, kwa sababu kila mwajiri anajipangia gharama ya kumlipa mfanyakazi, hivyo kutokana na hali hiyo wafanyakazi wengi wa baa na majumbani watakosa ajira," alisema.

Alisema pia serikali ingeonyesha ni jinsi gani utekelezaji wa ongezeko hilo utafanyika, hasa kwa wale wa majumbani na kwenye baa za mitaani.

Rais wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, alisema kima kilichowekwa na serikali na hasa kwa wafanyakazi wa majumbani kitawapa changamoto ya kuangalia kima cha chini kitakachowekwa kwa ajili ya wafanyakazi wa serikali hususani walimu.

"Kama mfanyakazi wa nyumbani atalipwa Sh 65,000 kwa mwezi, ili mwalimu aweze kumudu gharama ya kumlipa ni lazima awe na kipato kikubwa zaidi," alisema Mukoba.

Alisema kwa kuwa serikali imeanza na sekta binafsi, bado wanasubiri vikao vya Kamati Ndogo iliyoundwa na serikali hivi karibuni kwa ajili ya kuangalia mishahara ya wafanyakazi wa kima cha chini wa serikali.

"Baada ya serikali kutangaza kima cha chini kipya kwa walimu, tutapata mwanga wa wapi kuna mapungufu na wapi kunatakiwa kurekebishwa..." alisema.

Nalo Baraza la Habari nchini (MCT) limesema hatua ya serikali kutangaza kima kipya cha mishahara kwa sekta hiyo, huenda ikaviyumbisha baadhi ya vyombo visivyo na uwezo kifedha.

Pamoja na mtazamo huo, Baraza hilo limesema hatua hiyo bado ni nzuri kwa ajili ya kuangalia maslahi ya wafanyakazi wa sekta hiyo, lakini limeitaka serikali kuchukua hatua zaidi za kuviwezesha vyombo hivyo kwa kuvipa ruzuku ili viweze kutekeleza agizo hilo.

Akizungumza na Mwananchi jijini jana, Katibu Mkuu wa MCT, Anthony Ngaiza, alisema pamoja na nia nzuri ya serikali kuboresha vipato vya watu katika sekta binafsi, hatua zilizochukuliwa zinaweza kusababisha kufa kwa baadhi ya vyombo vya habari.

Ngaiza alisema kiwango hicho kipya kwa mishahara ya kima cha chini hasa kwa sekta ya habari ni vigumu kutekelezeka kwa kuwa vyombo vingi vya habari nchini bado ni vichanga.

Ni kiwango kizuri, lakini nadhani ni vyombo vichache sana vyenye uwezo wa kuwalipa wafanyakazi wake kima hicho kilichotajwa na serikali, kinachoweza kutokea ni mzigo kwa serikali kwa kuwa vyombo hivi vinaweza kufikia hatua kuamua kupunguza wafanyakazi ili kubaki na wachache kutokana na uwezo wa chombo kumudu hitaji hili,� alisema.

Ngaiza aliitaka serikali kuacha kuviita vyombo vya habari binafsi kuwa vya kibiashara kwa kuwa hata vya umma vinafanya biashara pamoja na kupewa ruzuku na serikali.

Wanatangaza kupanda kwa mishahara kwa sekta binafsi, kwa nini hawataji vya serikali ambao nao wamekuwa na malalamiko kwa muda,� alihoji Ngaiza.

Alisema kuwa serikali ina uwezo wa kuweka kodi maalum ya habari inayoweza kulipwa na makampuni, ili kuimarisha miundombinu ya sekta ya habari kwa kuvipatia ruzuku vyombo hivyo ili viweze kujiendesha kwa uhakika.

Pia wadau wa sekta ya habari ambao ni waajiriwa katika baadhi ya vyombo vikubwa nchini walisema kima cha chini kilichotangazwa na serikali bado hakiwezi kukidhi mahitaji kyao, hasa kutokana na mazingira magumu ya kazi yao.

Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti, walidai kuwa licha ya kutotosheleza mahitaji, pia ni vigumu kwa agizo hilo kutekelezeka hivyo kuitaka serikali kuweka mkakati maalum kuhakikisha kuwa kila chombo cha habari kinatekeleza kwa vitendo tangazo hilo la serikali.

Katika hatua nyingine, baadhi ya wafanyakazi wa mujumbani wamesema kima cha chini kilichowekwa na serikali kama kitatekelezwa na kusimamiwa ipasavyo kitawezakupunguzia ukali wa maisha.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa mashalti ya majina yao kutoandikwa gazetini, walisema tatizo lipo kwa waajiri wao ambao huwa ni wagumu kuwalipa mishahara yao kama inavyotakiwa inapofika mwisho wa mwezi.

"Kiasi hicho si kikubwa sana, lakini kimeonyesha uhai na dhamana ya wafanyakazi wa majumbani ambapo awali tulikuwa hatudhaminiwi hasa kutokana na mshahara tunaolipwa, "alisema moja wa wafanyakazi hao.

Alisema kwa sasa wanalipwa Sh10,00 na mara nyingine hawalipwi kwa wakati, hivyo ni vema serikali ikaandaa mkakati wa kunusuru hali hiyo.

Naye Rose Maungu alisema kuwa kiwango kilichowekwa na serikali hawataweza kukimudu kwasababu ni kikubwa ukilinganisha na kipacho cha Watanzania wengi kuwa duni.

"Mimi binafsi sitaweza kumlipa mfanyakazi wangu Sh65,000 kwa mwezi kwa sababu mfanyakazi wangu ni sawa na mwanangu, ninamnunulia nguo na pia ninampeleka hospitali akiugua," alisema.

Juzi serikali imetangaza rasmi kima cha chini cha mshahara katika sekta binafsi huku wafanyakazi wa majumbani wakipangiwa Sh65,000, wafanyakazi wa sekta ya madini Sh 350,000 na wahudumu wa baa na nyumba za kulala wageni wakipangiwa kiwango cha Sh 80,000 kwa mwezi, kuanzia mwezi ujao.

Viwango hivyo vipya vimetokana na utafiti uliofanywa na Bodi ya Uchunguzi wa Mishahara katika sekta binafsi, ambayo iliteuliwa Aprili mwaka huu na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, John Chiligati, kufuatia Sheria mpya ya Kazi namba 7 ya 2004, kifungu namba 35 (1).

Serikali imetoa onyo kwa mwajiri ambaye hatalipa viwango vipya kwamba atachukuliwa na hatua kwa mujibu wa sheria Kifungu 41 (1) cha Sheria ya kazi Namba 7/2007.
 

Susuviri,
Kwanza kabisa karibu jamvini!
Hapo kwenye kukurupuka mimi pia nafikiri ni hivyo, Waziri Ghasia (kama sijakosea) alikanusha miezi kadhaa iliyopita kuhusiana na jambo mojawapo la ongezeko la mishahara na wafanyakazi mbalimbali hasa Dar waliandamana. Kama malengo, sera na maamuzi haya yangelikuwepo muda mrefu si yangetaja nia ya kufanya hivi wakati ule wa vuguvugu lililo husika zaidi?..

Lakini mambo yale yametulia kidogo na kuepuliwa na wapinzani ambapo safari hii yamechanganyika na Buzwagi, basi serikali imeamua kutoa tamko la ongezeko katika sekta binafsi. Kama ongezeko hili halikupangwa miezi minne iliyopita, basi katika mambo ya uamuzi hili swala ni sawa na kukurupuka baada ya kukurupushwa, na kwa maana hiyo kama unawauliza miezi minne ijayo watafanya nini kuhusu mishahara ya waalimu watakuwa hawajui. Mpaka pale walimu watakapo andamana na kugoma kufundisha kwa siku 4!

Na hapo pengine kwenye responsibility kushinikiziwa sekta binafsi, kwa kweli mimi mwenyewe jibu makini moja sina... labda:
- bidhaa kama cement na mafuta viwe capped
- kuwe na subsidy katika bidhaa za mahitaji muhimu
- kiwango cha kima chini kiwe 'kiwango cha tamati' chini ya hapo mtu hahesabiki tena kama ni kima cha chini, maana atakuwa 'anaishi chini ya kima cha chini', hivyo kila kitu kwake kiwe cha kugawiwa/token.
.... mengi ya kufikiria hapa, lakini majibu ni magumu, hata hivyo haimaanishi kuwa majibu yote yaliyotelewa kama vigezo vya kuongeza mishahara ni sahihi.

SteveD.
 

Kili, kwanza kabisa heshima yako mkuu.

Kwenye hilo la uharamia, kwa hiyo unakubali upo au?! Kama upo ni nani wa kulaumiwa ambaye yupo kwa niaba ya wananchi? Nafsi ngapi zipo ambazo zinaweza kusema 'ni sisi' msimsumbue mwingine yeyote maana maharamia ni sisi.

Kama haupo, kwanini uchunguzi unaendelea kufanywa BoT hivi sasa? Wahusika walifanya nini kabla ya uchunguzi?

SteveD.
 

SteveD,
Angalizo langu la kusema sitetei maharamia, nilikuwa namaanisha wapo, lakini nasema hata maharamia wangekuwa hawapo, na sisi tusipofanya kazi nchi haitaenda popote!!!

Maharamia nnji hii ni wengi, ni kuanzia wale wanalipwa laki 300,000/- kwa mwezi ambao ni graduates, wanaendesha gari, wanajenga nyumba, kisa wizi kupitia semina, kusema nitakufanyia mpango hata pale ambapo service inatakiwa kuwa kawaida...
 
Posted Date::10/24/2007
Mishahara mpya sekta binafsi yazua balaa
*Wafanyakazi 553 waachishwa kazi viwandani
*Viwanda vyakutana Dar kuomba kipunguzwe

Na Gebo Arajiga, Arusha
Mwananchi

BAADA ya serikali kutangaza ongezeko jipya la mishahara wa kima cha chini katika sekta binafsi, Oktoba mwaka huu, makampuni mbalimbali ya watu binafsi vikiwamo viwanda vya nguo jijini Arushwa vimeanza kupunguza wafanyakazi.


Tayari viwanda viwili vya nguo vimepunguza wafanyakazi 553 katika kipindi cha wiki mbili zilizopita ikiwa ni baada ya ongezeko hilo la mishahara katika sekta ya viwandani ambapo sasa wanatakiwa kulipwa Sh 150,000 kwa mwezi. Kabla ya ongezeko jipya la mishahara, kima cha chini katika sekta binafsi kilikuwa Sh48,000.

Viwanda hivyo ni Sunflag (T) Ltd na A TO Z vyote vya jijini Arusha vimechukua hatua ya kupunguza wafanyakazi kutokana na kudai havina uwezo wa kulipa kiasi hicho cha fedha kutokana na wingi wa wafanyakazi ilionao.

Viwanda hivyo vinadai kuwa vimelazimika kuchukua hatua hiyo ya kuwapunguza kutokana na kushindwa kuwalipa mishahara hiyo mipya iliyotangazwa na serikali kuanza kutumika Novemba mwaka huu.

Msaidizi Mkuu wa Mkurugenzi wa kiwanda cha nguo cha A TO Z, Godwin Obed alisema kiwanda hicho ambacho kimeajiri wafanyakazi 3200 tayari kimeshapunguza wafanyakazi 133 na bado kitaendelea kupunguza hadi kufikia idadi ya wafanyakazi ambao wataweza kuwalipa mishahara hiyo mipya.

Kiwanda cha A TO Z kinamiliki viwanda vya kutengeneza plastiki, vyandarua, juisi, magodoro, nguo na maji.

Alisema tayari wenye viwanda vya nguo nchini wameshapeleka mapendekezo serikalini ya kutaka viwango hivyo vibadilishwe kutoka Sh150,000 hadi Sh 72 ,000 kwa mfanyakazi kwa mwezi.

Obeid alisema kuwa mazungumzo hayo yanaendelea jijini Dar es Salaam kati ya serikali na wamiliki wa viwanda vya nguo kufuatia pendekezo hilo." Iwapo viwango hivyo vya mishahara havitabadilika basi kuna uwezekano mkubwa wafanyakazi wengi wakapoteza ajira zao kiwandani hapa, " alisisitiza Obed.

Alisema kuwa viwango vipya vimepanda sana ukilinganisha na nchi za China, Nepal, Bangladesh, ambako wafanyakazi wa viwandani wanalipwa mishahara chini ya hii iliyoamriwa na serikali.

Alitoa mfano kuwa China mtu hulipwa dola za Marekani 43, Sirilanka dola za Kimarekani 38, Pakistan dola za Kimarekani 50 na Nepal dola za Kimarekani 27.

Katika kiwanda kingine cha nguo cha Sunflag (T) Ltd ambacho kina viwanda viwili vya nguo kilichopo Unga Limited na Themi Njiro ambacho kina watumishi zaidi ya 2000 tayari kimeshapunguza wafanyakazi 420 na bado kinaendelea na zoezi hilo
 
Finally! I am seeing news that is looking at the other side of the coin! I had a bad feeling that this will lead to massive job losses and also wakishindwa wenye viwanda wataenda Sri Lanka na India! I mean we need industries, siyo kuwapa masharti magumu! This will lead to recession (double it with inflation, fuel prices etc).... Again I am not an economist but it's obvious that more than 300% increase of salary is not a good strategy! Battle the inflation instead!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…