Serikali imeishiwa haina pesa za mishahara

WALIMU 20 wamewasili jijini Dar es Salaam kutoka Mbeya wakiwa katika lori lililosheheni mikungu ya ndizi kwa ajili ya kudai mishahara yao ambayo hawajalipwa tangu Februari mwaka huu mpaka sasa.


Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti jijini Dares Salaa jana, walidai kuwa wamekuwa wakifuatilia malipo ya mishahara yao bila mafanikio na badala yake wamekuwa wakiambiwa na maafisa wa mkoa huo kuwa ni watumishi hewa, waliajiriwa kihalali na wana nyaraka zote za ajira.


Walidai kuwa kitendo cha kuitwa walimu hewa, kiliwachukiza hivyo kuamua kusafiri kwa shida kwa kupanda lori la ndizi na kulala njiani hadi Dar es Salaamu kuja kudai haki zao.


Walisema mbali na wao kuna wenzao 40 ambao wamekosa nauli ya kufika Dar es Salaam hivyo wanawawakilisha.


“Unaona nguo yangu, madoa haya ni utomvu wa ndizi kwani tumelala juu ya ndizi, na wengine hatujui tutakula wapi na hatujui sehemu ya kulala,” alisema Godfrey Mhelela ambaye ni mmoja wa walimu hao.


Walipofika jijini walienda moja kwa moja katika ofisi za Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kutoa taarifa za kuwepo kwao na kuomba msaada kwa kusindikizwa katika ofisi husika serikalini ili suala lipatiwe ufumbuzi.


Baada ya kutoka ofisi za CWT waliandamana hadi Ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kueleza matatizo yao na kujua hatima yao huku wakisema kwamba kama hayatatatuliwa watakwenda Ikulu kumona Rais ili awasaidie.


Rais wa CWT, Gration Mukoba, alikiri kutokea tatizo hilo na kwamba yeye ndiye aliyewapokea na kuahidi kuwa atahakikisha walimu hao wanapata haki zao.


Mukoba aliongeza kwamba, wakati umefika wa serikali kuumbuka kwani ilikuwa na visingizio vya kwamba kuna watumishi hewa na kushindwa kutekeleza madai yao sasa hili linaonyesha wazi kwani walimu hao wana kila kitu, lakini wamekuwa wakiambiwa ni watumishi hewa.


''Serikali imekuwa ikisema visingizio vya kwamba kuna watumishi hewa je hili la walimu hawa wanalionaje na tukizungumza wanasema eti tunachochea migomo. Huu ni wakati mwafaka wa kutafuta haki kwa hali na mali na maafisa wa serikali wajisahihishe,'' alisema Mukoba.


Msemaji wa Ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Zamaradi Kawawa, alikiri kupokea malalamiko ya walimu hao na kwamba kuna ambao waligundulika kutokuwa katika vituo vyao vya kufanyia kazi hali iliyowapelekea kufutwa katika ulipaji wa mishahara.


Kawawa alifafanua kwamba, uchunguzi uliofanywa na ofisi hiyo ulibaini kuwa kuna walimu waliokuwa hawaonekani katika vituo vyao vya kufanyia kazi zaidi ya miezi miwili, hivyo hatua zichukuliwe ikiwa ni pamoja na kuwafuta katika orodha ya malipo ya mishahara.


“Tulifanya utafiti na kubaini kuna walimu waliokuwa wakifundisha shule nyingine za binafsi huku wakiendelea kupata mishahara kama wafanyakazi wa serikali na kwenda kupokea mishahara bila kufanya kazi hivyo tulisimamisha mishahara yao kwa kuwa serikali haiwezi kulipa watumishi hewa,” alifafanua Kawawa.


Alisema katika tatizo hilo, wanaotakiwa kutoa maelezo ni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwani walimu hao wako chini ya wizara hiyo na kwamba wao kama utumishi wanategemea taarifa kutoka Wizara ya Elimu.


Madai ya walimu hao yamekuja wakati kukiwa na kitisho cha kufanyika mgomo wa wafanyakazi wote kutoka Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi (Tucta), kudai maslahi yao. Hata hivyo mgomo huo ulisitishwa baada ya hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, aliyotoba bungeni wiki mbili zilizopita akiwataka kutofanya hivyo.
 
Hundi za mishahara katika idara mbali mbali za serikali zimeaanza kuingia. Lakini kwa mshangao na masikitiko ya wengi hakuna jipya katika mishahara hio. Hakuna cha mshahara mpya, wala cha malimbikizo. Je huku kungoja kote kulikuwa kwa nini kama hakuna kilochobadilika? Huu kusema kweli ni unyanyasaji wa hali ya juu. Moja, mtu haki yako ya kupata mshahara imecheleweshwa; Pili huku ukiwa na mategemeo kutakuwa walau na mabadiliko yatakayo ondoa maumivu za kusubiri, unakuta yale yale.

Nasema sasa Serikali yetu na Raisi Wetu wamekuwa WAONGO. Kwenye hili la mishahara Raisi Kikwete kwa makusudi kabisa AMEUDANGANYA umma wa watanzania. Je kuna sababu gani ya kumwamini katika jingine lolote atakalokuja nalo? Au ambalo ameshatuambia?

Kiongozi yeyote ambaye kwa makusudi kabisa anapotosha wale anao waongoza hafai kabisa katika Uongozi. Na wote waliomuunga mkono asilimia 100% kwenye hotuba yake nao wako kundi moja.
 
Watanzania mmeliwa! Rais kasema hatembei na fuko la pesa, bali anatembea na bakuli na kopo kuombaomba!
 
Mzee Wangu unajua wafanyakazi wa serikali hawajalipwa leo mwezi wa pili, sasa hiyo nyongeza inaongezewa wapi?

Jamani acheni kamba hizo nani kawaambia serikali haijawalipa watumishi wake kwa miezi miwili mfululizo?. siwezi kuamini hadithi hizi mpaka data ziwekwe hapa.

Itachekesha sana kama hili ni kweli. Ndege ya gharama tunayo, pesa za EPA zipo, mgodi wa kiwira upo. Kwanini tukose mishahara ya watumishi wa serikali?
 
hii kweli jamani mishahara tusidanganyane mpaka leo tarehe 33 haijatoka huku nilipo tumeambiwa imepelewa bank ila haman kitu tukiongea tunaonekana wakorofi tukigoma tunambia sio wavumilivyu. hivyi sisi watanzania tumelisha nini.

hebu fikiri kwa kawaida mishahara hutoka tarehe 26-29 ukienda bank unakuta mambo poa. mwezi uliopita haman kitu sisi huku nilipo wakatuwekea matangazo kuwa mishahara itachelewa kwa sababu wanafanya marekebisho ya mishahara mpya. tukawa waungwana tukasubiri hatimaye leo wanaleta tangazo mishahara mipya mpaka mwenzi wa 9 tuendelee kuvumilia hii inakwenda akilini. watu tumekopa tukijua kuna mishahara mipya na haman mkopo bila riba sik hizi hata kwa rafiki utasikia nakukopesha kwa riba.
inamaana hii serikali ya ccm inataka tuwe ombaomba kama yenyewe inavyo omba omba tunatengeneza taifa la nama gani
kwa ushauri wangu we mtanzania uliolala kwa kuambia tupo kwenye amani hakuna amani nashindwa kuendelea kwa sababu naona itaharibu key board yangu hasira nazipeleka huko
 
wewe unayesea serikali haijaishiwa unataka ujitangaze ndio uamini,kama haijaishiwa si itoe mishahara mipya. na hayo madai yetu. jamani hebu tuache kupotoshana
 
WALIMU shule za vijijini wilayani Iringa mkoani hapa kwa wameshinda siku tatu mfululizo katika benki ya NMB tawi la Iringa kusubiri foleni ipungue ili wachukue mishahara yao katika mashine ya kuchukulia fedha (ATM).

Mwandishi wa habari hizi jana asubuhi alishuhudia foleni hiyo ambapo baadhi ya walimu waliokutwa katika benki hiyo barabara ya Iringa-Dodoma ambao hawakupenda majina yao yaandikwe gazetini, walisema baada ya kupata taarifa na walimu wenzao wa mjini juzi, kuwa mishahara yao imetoka, walifunga safari kuja kuchukua fedha za matumizi.

Hata hivyo, baada ya kufika juzi saa sita mchana, walikuta foleni katika benki hiyo ikiwa ndefu na hivyo walilazimika kusubiri hadi saa moja usiku, ili ipungue, lakini bado idadi ya walimu iliongezeka.

Walisema walimu hao kwamba hadi saa nne usiku, bado foleni katika mashine hiyo ya ATM iliendelea kuwa ndefu hali iliyosababisha baadhi yao kuondoka na kwenda kutafuta vyumba vya kulala katika nyumba za wageni.

Walimu hao walisema hata hivyo baadhi yao walilazimika kurudi katika maeneo yao ya kazi huku baadhi yao wakitafuta hifadhi kwa ndugu na jamaa zao, ili kusubiri foleni ipungue katika mashine hiyo.

Kwani walisema mbali ya foleni, pia wakati mwingine fedha katika mashine hiyo zimekuwa zikiisha na hivyo kulazimika kusubiri na kama tatizo hilo limetokea baada ya muda wa kazi wa watumishi wa benki hiyo kumalizika, suala hilo husubiriwa mpaka asubuhi.

Pamoja na kuulalamikia utaratibu wa benki hiyo kushindwa kuongeza matawi katika maeneo mengine ya vijijini, pia walisema ni vyema Serikali kurudisha utaratibu wa zamani kwa walimu kupata mishahara yao kuliko utaratibu wa sasa ambao unaweza kurudisha maendeleo ya elimu kwa wanafunzi kutokana na walimu kushinda benki kufuata mishahara yao.

Pia alisema wapo baadhi ya walimu ambao wamekuwa wakilazimika kujiingiza katika vitendo visivyo vizuri ili kupata kuishi mjini, wanaposubiri foleni ipungue katika benki hiyo.

Pamoja na walimu hao kulalamikia benki hiyo kwa kuwa na mashine moja ya kuchukulia fedha, baadhi ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani wakiwamo askari Polisi na Magereza mjini hapa, jana kufungua akaunti ikiwa ni sehemu ya mchakato kuingia katika utaratibu wa kuwekewa mishahara yao katika akaunti zao kama walimu, utaratibu ambao umepokewa kwa shingo upande wa askari hao.
 
Sijui lini serikali yetu itawakumbuka walimu wetu kuwawaishia mishahara yao sijawahi sikia POLISI na wanajeshi kama wanapata usumbufu kama huu kwa walimu.......
 

Sijui lini serikali yetu itawakumbuka walimu wetu kuwawaishia mishahara yao sijawahi sikia POLISI na wanajeshi kama wanapata usumbufu kama huu kwa walimu.......

Jibu angalia hapo juu... nao soon wataingia kwenye kimbembe hicho..!

Cha msingi Hii ya kukaa kwenye foleni kwa siku tatu, ingefaa kuwataarifu Guinness book of records na kujua foleni ndefu katika ATM ilichukua muda wa siku ngapi na ilikuwa na urefu gani... Hii ni njia mojawapo ya kujitangaza duniani.

Huyo mwandishi wa habari next time at latest mwezi ujao aende na tape measure yake ili kupima urefu wa foleni hiyo tayali kuingizwa kwenye rekodi ya foleni ndefu duniani.
 
Kuanzia mwezi huu Polisi nao wameingia katika adha hii ya NMB. Tusubiri na jeshi (JWTZ) sasa.
 
Watu wanasubiri nini kuandamana?

Unajua kati ya wafanyakazi waoga kama kunguru ni walimu.........wapo wengi sana lakini waoga sana na hawana mshikamano na nguvu ya pamoja.......mishahara wanalipwa kiduchu mazingira ya kazi ni magumu sana kuliko mfanyakazi yeyote wa serikali lakini wao wanakomaa tu na nidhamu za woga...wanatakiwa kugoma na kuandamana nchi nzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…