Fidel80
JF-Expert Member
- May 3, 2008
- 21,947
- 4,470
WALIMU 20 wamewasili jijini Dar es Salaam kutoka Mbeya wakiwa katika lori lililosheheni mikungu ya ndizi kwa ajili ya kudai mishahara yao ambayo hawajalipwa tangu Februari mwaka huu mpaka sasa.
Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti jijini Dares Salaa jana, walidai kuwa wamekuwa wakifuatilia malipo ya mishahara yao bila mafanikio na badala yake wamekuwa wakiambiwa na maafisa wa mkoa huo kuwa ni watumishi hewa, waliajiriwa kihalali na wana nyaraka zote za ajira.
Walidai kuwa kitendo cha kuitwa walimu hewa, kiliwachukiza hivyo kuamua kusafiri kwa shida kwa kupanda lori la ndizi na kulala njiani hadi Dar es Salaamu kuja kudai haki zao.
Walisema mbali na wao kuna wenzao 40 ambao wamekosa nauli ya kufika Dar es Salaam hivyo wanawawakilisha.
Unaona nguo yangu, madoa haya ni utomvu wa ndizi kwani tumelala juu ya ndizi, na wengine hatujui tutakula wapi na hatujui sehemu ya kulala, alisema Godfrey Mhelela ambaye ni mmoja wa walimu hao.
Walipofika jijini walienda moja kwa moja katika ofisi za Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kutoa taarifa za kuwepo kwao na kuomba msaada kwa kusindikizwa katika ofisi husika serikalini ili suala lipatiwe ufumbuzi.
Baada ya kutoka ofisi za CWT waliandamana hadi Ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kueleza matatizo yao na kujua hatima yao huku wakisema kwamba kama hayatatatuliwa watakwenda Ikulu kumona Rais ili awasaidie.
Rais wa CWT, Gration Mukoba, alikiri kutokea tatizo hilo na kwamba yeye ndiye aliyewapokea na kuahidi kuwa atahakikisha walimu hao wanapata haki zao.
Mukoba aliongeza kwamba, wakati umefika wa serikali kuumbuka kwani ilikuwa na visingizio vya kwamba kuna watumishi hewa na kushindwa kutekeleza madai yao sasa hili linaonyesha wazi kwani walimu hao wana kila kitu, lakini wamekuwa wakiambiwa ni watumishi hewa.
''Serikali imekuwa ikisema visingizio vya kwamba kuna watumishi hewa je hili la walimu hawa wanalionaje na tukizungumza wanasema eti tunachochea migomo. Huu ni wakati mwafaka wa kutafuta haki kwa hali na mali na maafisa wa serikali wajisahihishe,'' alisema Mukoba.
Msemaji wa Ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Zamaradi Kawawa, alikiri kupokea malalamiko ya walimu hao na kwamba kuna ambao waligundulika kutokuwa katika vituo vyao vya kufanyia kazi hali iliyowapelekea kufutwa katika ulipaji wa mishahara.
Kawawa alifafanua kwamba, uchunguzi uliofanywa na ofisi hiyo ulibaini kuwa kuna walimu waliokuwa hawaonekani katika vituo vyao vya kufanyia kazi zaidi ya miezi miwili, hivyo hatua zichukuliwe ikiwa ni pamoja na kuwafuta katika orodha ya malipo ya mishahara.
Tulifanya utafiti na kubaini kuna walimu waliokuwa wakifundisha shule nyingine za binafsi huku wakiendelea kupata mishahara kama wafanyakazi wa serikali na kwenda kupokea mishahara bila kufanya kazi hivyo tulisimamisha mishahara yao kwa kuwa serikali haiwezi kulipa watumishi hewa, alifafanua Kawawa.
Alisema katika tatizo hilo, wanaotakiwa kutoa maelezo ni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwani walimu hao wako chini ya wizara hiyo na kwamba wao kama utumishi wanategemea taarifa kutoka Wizara ya Elimu.
Madai ya walimu hao yamekuja wakati kukiwa na kitisho cha kufanyika mgomo wa wafanyakazi wote kutoka Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi (Tucta), kudai maslahi yao. Hata hivyo mgomo huo ulisitishwa baada ya hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, aliyotoba bungeni wiki mbili zilizopita akiwataka kutofanya hivyo.