Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Naibu Waziri wa Fedha, Mwanaidi Ali Hamis ameliambia Bunge leo Ijumaa Februari 12, 2021 Jijini Dodoma kuwa hakuna mfanyabiashara aliyekimbia biashara yake kwa sababu ya kodi.
Ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Stella Fiyayo (Chadema) ambaye amehoji upi mkakati wa Serikali katika kufanya marekebisho ya kodi iweze kuendana na hali ilivyo.
Naibu Waziri huyo wa fedha, amesema Serikali haitozi kodi kandamizi na wala haifikirii kufanya hivyo kwa wananchi na wafanyabiashara wake.
Majibu ya Naibu Waziri yamekuja wakati wabunge wamekuwa wakipiga kelele kwa wiki nzima wakilalamikia kodi kubwa wanazotozwa wafanyabiashara na Mamlaka ya Kodi (TRA).
Kwenye michango yao, wabunge hao walisema mfumo unaotumika kukadilia na kudai kodi siyo rafiki kwa wafanyabiashara na wawekezaji.