KERO Serikali imekisahau Kijiji cha Olchoronyori - Wilaya Simanjiro, huku hakuna Vodacom, Yas wala Airtel

KERO Serikali imekisahau Kijiji cha Olchoronyori - Wilaya Simanjiro, huku hakuna Vodacom, Yas wala Airtel

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mdau kutoka Kijiji cha Olchoronyori Wilaya Simanjiro, Serikali imepasahau tunaomba itembelee huku ione changamoto zilizopo.

1. Tunaomba kujengewa mnara wa Mtandao wa Vodacom, TIGO au Airtel maana huku tunatumia TTCL unaotegemea jua tu na kukatika mara kwa mara na kusababisha ukosefu wa mawasiliano.

2. Wazawa wa eneo hili hawataki kutoa ardhi kwa ajili ya wageni (watumishi wa umma) hali inayofanya mtumishi kusafiri mara kwa mara kwenda kuangalia familia yake, hiyo inasababisha kufanya kazi katika mazingira magumu, wizara husika iingilie kati suala hili.

3. Watumishi wa Umma wanapoitwa halmashauri hawapewi stahiki zao kama posho za nauli na mwishowe kusababisha Wafanyakazi kuona utumishi ni mzigo kwao na unakuta halmashauri iko mbali sana na kituo cha kazi.
 
Back
Top Bottom