Serikali imekosa ubunifu, inachofikiri ni kuongeza kodi tu

Artifact Collector

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
6,617
Reaction score
10,205
Ukimuangalia Mpango na Mwigulu wote akili zao zinafanana, wanachofikiri kila siku ni kuongeza kodi. Kwa akili hizi hatuwezi kwenda mahali popote.

Tanzania ili iendelee lazima tuwe na ubunifu na lazima tutumie pure capitalism ili nchi iendelee kivipi;-
  • Kushusha corporate tax kutoka asilimia 30 mpaka 8
  • VAT kwa corporate iwe asilimia 4 na kwa bidhaa asilimia 2
  • Income tax iwe asilimia 3 hii itawafanya watu wengi walipe kodi
  • Interest rate kwa central bank kwenda commercial bank asilimia 2, na commercial bank hawaruhusiwi kuomtoza mtu Zaid ya asilimia 5 kwa kampuni na mtu aliyeko Tanzania
  • Ili kufungua kampuni Tanzania haihitaji kuwa mtanzania
  • Kuondoa tax holiday kwa sababu tayari Kodi zimeshashushwa maradufu
  • Kuondoa minimum wages kwenye private sector muajiri na mwajiriwa wataelewana na soko ndo litakaloamua
  • Transit duty asilimia 2
  • Sales tax asilimia 3
  • Mtalii akija Tanzania alipa dollar 500 tu hio ndo kama kibali Cha yeye kutembelea vivutio vyote bila ya usumbufu kwa mda usiozidi mwezi mmoja
Na pia ilikuvutia uwekezaji lazima mfumo wa mahakama uwe huru asilimia mia 100 kivip;-
Jaji mkuu, na majaji wote wanachaguliwa na mahakama, mahakimu wote wanaajiriwa na mahakama- Rais hausiki na serekali haihusiki kwenye kuwachagua kwa namna yeyote Ile

Kufanya serekali kuwa ndogo kwanza kuwaondoa wakuu wa wilaya wote, mkuu wa mkoa anachaguliwa na wananchi na analipwa msharahara kulingana na mapato ya mkoa husika. Kazi nyingi za serekali sio zote zinakua outsource kwa private sector

Wabunge mishahara na posho zitabaki kama zilivyo, kama wananchi wengine lazima watozwe Kodi, na hawatanunuliwa zile V8, mbunge akitaka kufanya ziara jimboni kwake usafiri na mafuta atagharamikiwa na mkoa wake, kwenda kwenye vikao vya binge ni gharama zake

NOTE;- Baada ya haya mabadiliko Tanzania itakuwa ni kitovu cha contract manufacturing barani afrika na ajira nyingi zitazalishwa. Na pia uchumi utapanda maradufu kwa sababu uchumi utakua kwa asilimia 12-15% na ukiendelea hivi kwa miaka 10 tu itakua ni habari nyingine umaskin utapungua

Lugha iliyotumika sio nzuri sana
 
Ilitakiwa uitwe "Corporate au Tax Priest", na sio Science Priest.

Excellent Vision Mkuu.[emoji1534]

Ubaya zaidi ni kwamba serikali yetu haina planned vision ya mbali kwa taifa, kwamba mikakati yetu baada ya miaka 50 tuwe hatua gani. Kila kiongozi akishika madaraka anaelekea anapojua yeye na akili yake.

Serikali haina stages ilizojipangia kimkakati ili taifa kuelekea kwenye mode ya kuwa developed. Kila Waziri akiteuliwa anakwenda na akili yake inapotaka aende.

 
Shida ya Wanasiasa na viongozi wa Bongoland huwa wanajiona wenye akili Sana kushinda watu wengine.
 
Ni kweli viwango vinatakiwa kushuka but haviwezi kushushwa ghafla na kwa figures ulizozitaja overnight.

Ukifanya hivyo lazima kuwe na pesa ya kuziba pengo litakalojitokeza maana elasticity yake haiwezi kutokea kwa haraka kiasi cha kuziba nakisi kwa haraka.

So kama wanaamua kufanya hivyo lazima serikali iwe na uhakika wa mapato na njia ya haraka ni kukopa tena sio ndani bali nje kwa wastani wa miaka 3 hivi.

Nahisi Serikali inaogopa mikopo au mikopo ya bei nafuu haipatikani kirahisi kwa hiyo wanachelea kutumia hiyo mbinu.

Mwisho hiyo mbinu lazima ujue itapush inflation haraka Sana but wachumi hawana uhakika wa viwango vinavyoweza kufikiwa kwa kuwa uchumi wetu sehemu kubwa ni informal ndio maana unaona wanaongeza kodi .

Binafsi napendekeza kupunguza viwango vya kodi ila kwa awamu na kwa rates za wastani sio kama hizo zako maana ni ndogo Sana
 
Ni kweli haiwezi kutokea Mara moja, Ila kwa kupitia niliyopendekeza ni rahisi sana kutransform informal sector kuwa formal sector sababu hawataona burden kulipa Kodi tofauti na Sasa hivi Kodi ni kubwa sana
 

Sifa ya kuwa mbunge ujue kusoma na kuandika.ila dereva umalize form 4 na ufaulu usio zidi div 4.

[emoji23] ccm na katiba ndio imetufikisha huko
 
Ni kweli haiwezi kutokea Mara moja, Ila kwa kupitia niliyopendekeza ni rahisi sana kutransform informal sector kuwa formal sector sababu hawataona burden kulipa Kodi tofauti na Sasa hivi Kodi ni kubwa sana
Hata hivyo serikali imeanza kufanyia kazi ndio maana kuna ile wanaita blue print japo inajivuta sana.Nezt fy utaona mabadiliko makubwa zaidi.

Hilo la Rais sijui Ma DC nk halitekelezeki kwa sasa ila hayo mambo ya kodi na kisera yanatekelezeka ila kwa njia niloyosema japo ni kwa kujikongoja sana
 
... kwa suggestions hizo hebu nenda hatua moja mbele utuambie Serikali itaingiza billions ngapi. Hii itatupa picha kamili kama ubunifu huo ni faida au ni hasara.
Ndio maana nimemjibu hakuna serikali itafanya hayo overnight never? Huku sio Ulaya Ili muwekezaji aje kuna factors nyingi wanaangalia ,by the way mitaji hakuna,demand hakuna na sababu kadha wa kadha.

Hivyo hayo mambo yatafanyika taratibu taratibu,hilo jambo hawezi kukupa jibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…