Serikali imesema TRA haitozi kodi kwa wasafiri kati ya Zanzibar na Tanzania bara wanaobeba vitu kwa matumizi binafsi

Serikali imesema TRA haitozi kodi kwa wasafiri kati ya Zanzibar na Tanzania bara wanaobeba vitu kwa matumizi binafsi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Serikali imesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) haitozi kodi kwa wasafiri kati ya Zanzibar na Tanzania bara wanaobeba vitu kwa matumizi binafsi.
1.JPG

Hayo yameelezwa bungeni, jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Danie Silo (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Konde, Mhe. Mohamed Said Issa, aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itawaondolea usumbufu wa kikodi wananchi wanaobeba vitu vya matumizi binafsi wanaposafiri kati ya Zanzibar na Tanzania Bara.

‘‘Changamoto hujitokeza wakati wafanyabiashara wengine wasiokuwa waaminifu kubeba vitu vya biashara na kutokutaka vitozwe kodi, Wafanyabiashara hao wanavipitisha bandarini wakiwa wamevigawanya kwa abiria au kutumia wabeba mizigo wa hapo bandarini ili kuvitoa’’, alifafanua Mhe. Silo.

Mhe. Silo alisema kuwa baada ya bidhaa hizo kupita maeneo ya bandari mfanyabiashara husika anakabidhiwa vitu vyake bila kuvilipia kodi ambapo kutokana na utaalamu na weledi wa maofisa wa forodha mazingira kama haya ya wafanyabiashara hao hugundulika.

Mhe. Silo aliongeza kuwa mchezo huo ukigundulika wafanyabiashara hutelekeza mizigo hiyo bandarini na kuanza kutoa lawama kwa TRA kwamba wanashikilia bidhaa za wasafiri kitu ambacho hakina ukweli wowote.
 
Wanachekewa sana wazanzibari matatizo wanatengeneza wenyewe halafu wanalalamika.

Wao ndio walitaka waachiwe mamlaka ya kuamua mambo ya forodha bila ya kujali movements za raia wa bara na visiwani.

Wameenda weka kodi zao chini ili kivutia mizigo ishuke kwao wakidhani itaweza ingia bara kirahisi tu.

Personal tabia za hawa watu zimenifika kweli vunjilia mbali ili limuungano na mijitu ambayo aina shukran. Utaratibu wao ‘changu ni changu, chako ni changu’.
 
Wafanyabiashara na wenye viwanda wanapaswa kulipa kodi stahili kwa uhai wa Taifa letu.

Kodi zinazolipwa zinapaswa kutumika vema,Kulindwa na kusimamiwa vema na si kufujwa.

Mchakato wa kukusanya kodi stahili unapaswa kufanyika kwa kuzingatia uhalisia wa kibiashara na kulinda mazingira bora ya uendelezaji wa biashara.

Wigo wa walipa kodi bado ni mdogo mnoo ukizingatia idadi ya raia wa nchi ama wanufaika wa matunda husika.

Tunakopa kufadhiri miradi lukuki..Tutalipa,Lazima tulipe..Kwa miaka mingi ijayo..Lazima tukuze shughuri mbalimbali za kiuchumi sasa na baadae..

Hatupaswi kuua biashara kwa msingi wa kukusanya mapato ili kuvunja rekodi..Hatupaswi kunyanyasa wafabiashara na wenye viwanda kwa kivuli cha kufurahisha wanasiasa..Hatupaswi kuziba masikio lundo la biashara likifa kwa sababu ya ukatiri wa maafisa kodi..

Dunia inapita ktk changamoto nyingi za kibiashara kimataifa..Tujifunze na kuchukua hatua stahiki kuchukua hatua stahiki kulinda sekta binafsi na wenye viwanda..

TUACHE:-
UBABE
KIBURI
DHARAU
UKATIRI
 
Back
Top Bottom