Bosco Ntaganda
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 1,636
- 2,020
Ndugu zanguni, katika kipindi cha hivi karibuni sote tumeshuhudia matukio ya KUOGOPESHA yakiendelee nchini. Kwa uchache tu, kupotea kwa vijana walioonekana kuikosoa serikali kama Ben Saanane na wengineo, kuchapwa mvua za risasi Lissu mchana kweupe (tena katika makazi ya viongozi), viongozi wa baadhi ya vyama kushambuliwa, ofisi kuchomwa moto n.k
Kushamiri kwa matukio ya namna hii kwa kweli kunatupa mashaka makubwa sana sisi wananchi wa kawaida. Inaleta UKAKASI kuona serikali ikijikita kwenye ununuzi wa MADEGE MAKUBWA, ujenzi wa madaraja na mabwa ya kufua umeme n.k huku ikipuuzia usalama wa wananchi wake na mali zao.
Kwa muktadha huu, ni kweli tuna serikali INAYOWAJIBIKA kwa raia wake? Ama tuna KIKUNDI tu kinachotwala kwa maslahi yake binafsi? Kushindwa kudhibitiwa kwa UFEDHULI HUU unaoendelea nchini, lawama zimuendee nani? Nani ameshindwa kutimiza wajibu wake IPASAVYO?
Tumekuwa tukiaminishwa kwamba haya matukio ya KIFEDHULI yanayoendelea na njama za kupangwa na wahusika wenyewe. Kwa kuwa tuna aminishwa kwamba wahusika WANAFAHAMIKA (kutokana na upangwaji huo wa matukio), serikali imechukua hatua gani kuwakabili hao WAPANGAJI WA MATUKIO YA KIFEDHULI ili kutujengea imani, kutuondolea hofu na kutuhakikishia usalama wetu sisi wananchi wa kawaida?
Serikali imeishiwa mbinu na maarifa ya kukabiliana na haya matukio ya kifedhuli ama imeamua tu kuwaachia WAPANGAJI MATUKIO YA KIFEDHULI watambe watakavyo?
Nani anayepaswa kuwajibika kwa uonevu huu unaoendelea nchini kutokana na haya MATUKIO YA KIFEDHULI?
Kama haijulikani anayepaswa kuwajibika kwa UHUNI, UHALIFU WA KIBINADAMU na MATUKIO YA KIFEDHULI ambayo yanaendelea kufanyika nchini, Kuna haja ya kuendelea na kuvumilia MACHUNGU ya namna hii kwa miaka mingine mitano tena? TUJADILI..