Pre GE2025 Serikali imetangaza kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Soni - Bumbuli - Korogwe kwa kiwango cha lami

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Serikali limetangaza imetangaza kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Soni - Bumbuli - Korogwe kwa kiwango cha lami.

Ujenzi huo utaanza rasmi baada ya kufunguliwa kwa zabuni ya mkandarasi mnamo Machi 6, 2025, ambapo awamu ya kwanza itahusisha kilomita 20 kutoka Soni hadi Bumbuli, hatua inayotajwa kuwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha miundombinu na kufungua wilaya ya Lushoto na Mkoa wa Tanga kiuchumi.

Soma pia: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema hayo leo Jumatatu Februari 24, 2025 akiongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara wilayani Lushoto mkoani humo.

Rais Samia amepongeza juhudi za wananchi wa Lushoto katika utunzaji wa mazingira na kuwaagiza wawafundishe wengine ili kuhakikisha mazingira yanaendelea kuhifadhiwa kote nchini.

“Niwape wana Lushoto maua yenu katika utunzaji wa mazingira, ukiingia Lushoto hata uvutaji wa hewa unakuwa ni wa tofauti zaidi. Naomba muwafundishe wengine na muendelee kuweka mazingira vizuri.”

Akizungumzia lengo la ziara yake , Rais Samia ameeleza kuwa, ni kuwaona wananchi na kujiridhisha na matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo.

“kwa siku mbili hizi, nimefurahi kuona kuwa fedha zinazotolewa na serikali zimetumika vizuri kwa maendeleo ya wananchi,” alisema.

Mara baada ya kuzindua jengo jipya la Halmashauri ya Bumbuli, Rais Samia amebainisha kuwa, serikali yake imejenga majengo 122 ya Halmashauri ndani ya kipindi cha miaka minne ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kuimarisha utawala bora.

Aidha, amesisitiza kuwa serikali inaendelea kuboresha huduma za kijamii kama elimu, afya, maji, na umeme, huku akifurahishwa na barabara zilizofunguliwa ndani ya wilaya ya Lushoto kama sehemu ya mpango wa kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi.
 
  • Thanks
Reactions: Tui

Lakini hii haizui mbunge wa chama kingine kuchaguliwa au inazuia
 
. Ki ujumla tu, Tanga barabara inabidi ziboreshwe maana ni finyu sana..

. Leo mama samia alikuwa tanga, foleni ilikuwa kubwa sana.. Kwa sababu ya ufinyu wa barabara.
 
Miaka 60 ya Uhuru bado RAISI ndiyo anatupangia juu ya ujenzi wa barabara? Ina maana asingefanya ziara barabara isingejengwa?
 
Serikali limetangaza imetangaza kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Soni - Bumbuli - Korogwe kwa kiwango cha lami.

Ujenzi huo utaanza rasmi baada ya kufunguliwa kwa zabuni ya mkandarasi mnamo Machi 6, 2025, ambapo awamu ya kwanza itahusisha kilomita 20 kutoka Soni hadi Bumbuli, hatua inayotajwa kuwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha miundombinu na kufungua wilaya ya Lushoto na Mkoa wa Tanga kiuchumi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema hayo leo Jumatatu Februari 24, 2025 akiongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara wilayani Lushoto mkoani humo.

Rais Samia amepongeza juhudi za wananchi wa Lushoto katika utunzaji wa mazingira na kuwaagiza wawafundishe wengine ili kuhakikisha mazingira yanaendelea kuhifadhiwa kote nchini.

“Niwape wana Lushoto maua yenu katika utunzaji wa mazingira, ukiingia Lushoto hata uvutaji wa hewa unakuwa ni wa tofauti zaidi. Naomba muwafundishe wengine na muendelee kuweka mazingira vizuri.”

Akizungumzia lengo la ziara yake , Rais Samia ameeleza kuwa, ni kuwaona wananchi na kujiridhisha na matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo.

“kwa siku mbili hizi, nimefurahi kuona kuwa fedha zinazotolewa na serikali zimetumika vizuri kwa maendeleo ya wananchi,” alisema.

Mara baada ya kuzindua jengo jipya la Halmashauri ya Bumbuli, Rais Samia amebainisha kuwa, serikali yake imejenga majengo 122 ya Halmashauri ndani ya kipindi cha miaka minne ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kuimarisha utawala bora.

Aidha, amesisitiza kuwa serikali inaendelea kuboresha huduma za kijamii kama elimu, afya, maji, na umeme, huku akifurahishwa na barabara zilizofunguliwa ndani ya wilaya ya Lushoto kama sehemu ya mpango wa kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi.
Sa 100 kilomita 20 ni za kuwalaghai watu wa Bumbuli wampe Kura makamba maana hamna cha maana ambacho mpaka sasa kimefanyika huko Bumbuli licha ya Makamba kukaa bungeni kwa zaidi ya miaka 15
 
Back
Top Bottom