Serikali imetenga Trilioni 1 kwa ajili ya safari za ndani na nje kwa mwaka wa fedha 2026/27. Bilioni 833 kutumika katika safari za ndani ya nchi na Bilioni 149 kutumika katika safari za nje.
Ni katika bajeti ambayo imewasilishwa Juni 11, 2026.
Trilioni moja zatengwa kwa ajili ya safari za nje na ndani ya nchi. Serikali imetenga bajeti ya trilioni moja kwa ajili ya safari za ndani na nje ya nchi kwa mwaka wa fedha 2026/2027. Katika fedha hizi, bilioni 883 zimetengwa kwa ajili ya safari za ndani wakati bilioni 149.2 zimetengwa kwa ajili ya safari za nje ya nchi. Fedha hizi zinakaribiana na zile zilizotengwa 2025/2026 ambazo zilikuwa takriban trilioni 1.04.
Kwa ujumla, kumekuwepo na ongezeko la fedha zilizotumika kwa ajili ya safari ambapo kwa mwaka 2020/2021 fedha zilizotumika zilikuwa bilioni 299. Kwa mwaka 2021/2022 fedha hizi ziliongezeka kufikia bilioni 397. Kwa mwaka 2022/2023 fedha zilizotumika kwenye safari ziliendelea kuongezeka na kufikia bilioni 686.7. Kwa mwaka 2024/2025 fedha za safari ziliongezeka kwa kasi zaidi hadi kufikia bilioni 993.
Kwa ujumla, ndani ya miaka mitano takriban trilioni 2.87 zimetemika kwenye safari za ndani na nje ya nchi. Fedha hizi ni zaidi ya fedha zilizotumika kujenga reli ya SGR kati ya Dar es Salaam mpaka Morogoro. Ni fedha sawa na kujenga daraja kama la Kigongo-Busisi walau madaraja matano.
Pia soma: Wizara ya Mambo ya ndani yaomba kuidhinishiwa sh. Trilioni 2.44 Kwa mwaka wa fedha 2026/2027