Serikali imetosheka na walimu wa arts hawaitajiki tena

Poleni sana walimu mnaosubiri ajira, hata mwaka jana yalisemwa mengi sana lakini mwisho wa siku tuliajiriwa.. Chamsingi ukipata ajira popote wewe nenda.Ukweli ajira ni ngumu sana. I feel your pain
 
Hao walimu wa Arts hawaitajiki kwa Mwaka upi na nchi ipi? Na kama ni Tanzania sio kweli...Maana tayari walishajaza form za ajira Mwezi wa 6 na Wale waliohitimu vyuo vikuu tayari walishapewa form zinazoonesha kiasi gani cha mkopo wanadaiwa na Muda ambao mkopo huo wanapaswa kuanza kuurejesha umewekwa kwenye zile form,na waliopewa hizo form ni watu wa faculty ya education tu,faculty nyingine hawajapewa,sasa jiulize kwa nini wamepewa walimu tu wakati kuna watu pia wa faculty zingne hawajapewa wakati walikuwa na mikopo? Isitoshe Naibu waziri TAMISEMI Aggrey Mwanry Alishasema kuna upungufu wa walimu 43,000.
 
Mwaka huu Wa uchaguzi tutasikia mengi mnoo mala kufuta ada duhhh,,,, tunaombwe la viongozii
 
Hivi nyie walimu kwa nini mnapenda sana serikalini badala ya private schools? ningesomaga ualimu ningeendaga Laureate International School kufundisha sio mnaendekeza ulele mama
 
Hivi nyie walimu kwa nini mnapenda sana serikalini badala ya private schools? ningesomaga ualimu ningeendaga Laureate International School kufundisha sio mnaendekeza ulele mama

Huko kuna mafao ya uzeen ndo maana
 
Rais amesema ya kuwa hakuna tatizo la walimu wa masomo ya arts na hajasema kuwa walimu wa arts hawahitajiki so nadhani hapa kuna tatizo la uelewa Kwa mtoa mada
 
Hivi nyie walimu kwa nini mnapenda sana serikalini badala ya private schools? ningesomaga ualimu ningeendaga Laureate International School kufundisha sio mnaendekeza ulele mama

tatizo lako ndugu yangu hujataka kuelezwa faida za kufanya kazi serikalini. Tafuta mtu akuelimishe kidogo kuhusu hilo. Na ndio mana unaweza kukuta mtu anafundisha private lakini ajira za serikali zikitoka anaacha private na kwenda serikalini hata kama mshahara ni mdogo kuliko private,na mazingira ni mabaya lakini ataenda tu. Jiulize ni kwa nini??kazi ya serikali ina raha yake hta kama ujira wake ni mdogo.
 

Tumebakiwa na upungufu wa walimu 45,223 yaani 26,946 wa shule za msingi na 18,277 wa shule za sekondari hususan wa masomo ya sayansi. Hivi sasa hatuna tatizo la walimu wa masomo ya sanaa katika shule za sekondari.Hivi mwanzisha thread aliisoma hii statement na kuielewa kweli au vip maana hapa rais alimaanisha kwamba bado pengo la waalimu lipo ila hususani kwa waalimu wa sayansi maana waalimu wa arts wapo tayari sokoni ila waalimu wa sayansi wenyewe hawapo kabisa so ndo maana akaelezea hatua zilizochukuliwa na serekali juu ya upatikanaji wa waalimu wa sayansi na sio kwamba serekali hawahitaji tena walimu wa arts nb tusipende kuongezea chumvi kwenye thread tunazozianzisha maana zinapotosha taarifa !!!!!
 
Ninacho jua waalimu wote huandaliwa kwa kutokana na ufaulu wa masomo anayo somea lakin tathimini zinaonesha masomo ya sayansi ufaulu wake toka kidato cha 4 mpaka Chuo Kikuu ni mdogo mno hivo msingi wa sayansi ni mbovu katika shule nyingi hivo inatakiwa mpango madhubuti kukabiliana na hili tatizo
 
Walimu wengi tu wa Arts bado wanaendelea kuajiriwa kila wakati. Ishakuwa kama taratibu kutangaza kila wakati na kusema wametosha.
 
Hivi nyie walimu kwa nini mnapenda sana serikalini badala ya private schools? ningesomaga ualimu ningeendaga Laureate International School kufundisha sio mnaendekeza ulele mama

Uko private unafkir wanaingia tu kama choo cha shule?
 

tatizo eti serikali haina fungu la kuajiri.
 

Ulikua wap toka mwanzo! mana vijana wameangamizwa kisaikolojia kwa kukosa maarifa... well said mkuu i like it..
 
Ajira zitakuwepo such as self employment as well as private schools, usi cremishe maisha sio kila msichana ni bikra
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…