... eti mtu na akili zake anauliza waende wapi! Uholela huo ukiachwa maana yake yeyote popote alipo ana haki ya kujifanyia biashara popote mijini bila kuzingata sheria zilizopo. Kila mwaka maelfu kwa maelfu ya vijana wanahamia mijini na kama kimbilio la walio wengi ni kufanyia biashara mabarabarani hali itakuwaje huko tuendako?
La muhimu sheria zisimamiwe kikamilifu vinginevyo linatengenezwa tatizo la kudumu kwa kisingizio cha wanyonge! Ni aibu kwamba ilifika mahali wakajihalalishia maeneo hayo kinyume cha sheria na taratibu za mipango miji kwa kisingizio cha kulipia 20,000! Aliyebuni hili ni sehemu ya tatizo na mvunja sheria namba moja kwa suala hili la umachinga.