- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu
Nimekutana na hii baua ikionesha kuwazua watumishi wa serikali wasijihusishe na post za wanasiasa kama vile Sativa, Mange Kimambi na Maia Sarungi. Je una uhalali kiasi gani?
Nimekutana na hii baua ikionesha kuwazua watumishi wa serikali wasijihusishe na post za wanasiasa kama vile Sativa, Mange Kimambi na Maia Sarungi. Je una uhalali kiasi gani?
- Tunachokijua
- Kumekuwa na tangazo linalosambaa katika mitandao ya kijamii likiwa na utambulisho wa taasisi za serikali (Wizara) likieleza kuwa imebaini kua watumishi wanaendelea kufuatilia na kushadadadia baadhi ya akaunti zinazosambaz chuki dhidi ya serikali ikiwemo akaunti ya Sativa, Mange Kimambi, pamoja na Maria Sarungi.
Uhalisia wa Tangazo hilo
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejiridhisha na kubaini kuwa tangazo hilo ni la kughushi.
JamiiCheck imebaini baadhi ya mapungufu kadhaa katika tangazo hilo ikiwemo kuchanganya wizara. Mathalani rejea aya ya kwanza ambayo inataja ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora kisha chini inaonekana imetolewa na TAMISEMI.
Aidha anayeonekana kusaini taarifa hiyo kama mkuu wa kitengo cha mawasiliano Ofisi ya Rais-Tamisemi, Nteghenjwa Hosseaah hayupo katika wizara hiyo. Ambaye alisema kuwa;
"Hiyo barua siyo halisi na wala sijaandika mimi na haijatoka kwangu, nipo Wizara tofauti na hiyo iliyoandikwa hapo.”
Mbali na hilo wizara ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa kwa sasa imehamishiwa ofisi ya Waziri Mkuu kutoka ilipokuwa awali kwenye ofisi ya Rais.
Hata hivyo si ukurasa Wizara ya utumishi wa umma wa TAMISEMI zilizowchapisha taarifa hiyo ama yenye kufanana na hiyo.