Wakuu habari,
Tufuatilie live ya Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Boniface Mwabukusi akitoa tamko Muda huu
View: https://www.youtube.com/live/u4jupslBLE8?si=gvSCRvis826W9uvQ
Wakili Boniface Mwabukusi: Sisi kama TLS tunawajibu wetu wa kisheria na katika kutekeleza wajibu wetu wa kisheria tulijiwekea utaratibu kwamba ni vizuri tufanye sana engagement kwa njia ya mazungumzo na kukuta uso kwa uso na wadau wetu au mamlaka mabalimabali. Lengo letu kubwa ni kuhakikisha kila mmoja anaheshimika, tunatambua nafasi yake, tunaikubali nafasi yake na tunampa nafasi ya kujua, kuelewa na kufanyia kazi kile ambacho TLS inashauri.
Chama cha wanasheria Tnganyika (TLS) ni taasisi iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria ambayo ni Tanganyika Law society Act sura 307 ilivyorejelewa mwaka 2019 na moja ya wajibu wake ni kulinda, kusimamia maadili ya taaluma ya sheria, kulinda utawala wa sheria, haki za biandamu na demokrasia na vilevile kushauri kushirikiana na bunge pamoja na serikali ili kuhakikisha utawala wa sheria, utawala bora unatamalaki katika taifa letu.
Ndugu watanzania tupo kwenye kipindi cha uchaguzi. Uchaguzi wa mwaka huu ni uchaguzi ambao umekua na changamoto kidogo na hii inatokana na yale yaliyojiri kwa hali ya muendelezo ya kukua au kutandaa ambayo dalili na viashiria vilianza mwaka 2018, 2019 wakati wa uchaguzi wa serikali za mtaa, tukaviona mwaka 2020 vikajirejea 2024, ambapo iliuwa trend ya ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi katika taifa letu.
Kwasababu 1995 tulivyoanza tulikua tumeanza chini lakini tunakua gradualy. Hakuna uchaguzi katika uliofanyika nchi hii ukakosa changamoto hata zile za chama kimoja zilikua na changamoto, kwaiyo hatuwezi kuwa na uchaguzi fully insulated isiwe na changamoto, changamoto zinakuwepo lakini lazima ziwe changamoto zionekane changamoto zinazotokana na uchaguzi wenyewe siyo cghangamoto zinazosababishwa kwa kukusudiwa na wale wanaotakiwa kufacilitate zoezi la uchaguzi.
Uchaguzi wa mwaka huu tofauti na mika mingine katika hali ambayo si nzuri kumekuwa hali kitaifa ambayo inaleta mgawanyiko wa kisiasa, kidini na kikabila. Haya mambo hatutakiwi kuyaonea aibu kuyakemea na kuyasema wazi ili tutafute suluhisho. TLS muda wote na wakati wote tutakuwa daraja la haki ili kuweza kutafuta muhafaka kwa njia ya mazungumzo na maelewano bila kumuonea mtu, kumpendelea mtu, kutishwa au kubabaishwa, tutafanya wajibu wetu wa kisheria tukiwajibika kisheria na kwa katiba ya nchi yetu.
Uchaguzi wa mwaka huu umekumbwa na changamoto mbalimabali na moja ya changamoto hizo zimepelekea hata kauli mbiu zetu siyo zile tulizozoea ni kauli mbiu ambazo hazileta afya katika ushindanin wa kidemokrasia , kuna wanaosema 'Oktoba tutatiki' hatuuziana sera kwaiyo yeye atatiki tu, mwingine anakwambia 'no reforms no election na mwingine anakwambia Piga kura, Linda kura. Kauli hizi zinaonyesha changamoto katika mfumo wetu wa kiuchaguzi.
Ndugu wananchi hatukatai kwamba kulikuwa na mabadiliko, mabadiliko wamefanyika kwenye sheria za uchaguzi lakini tuwe wa kweli unapobadilisha unataka kutibu nini. Hata makaburu walikua na sheria, Hitler alikuwa na policy zake alikuwa na sheria. Tunapoangalia zoezi la uchaguzi maana yake lazima liwe lenye kuwajibika, lenye uwazi, lenye kutoa heshima ya thamani na kura, lenye kutabirika na lenye usawa, haya ni mambo tunayoyaangalia katika uchaguzi.
Katika hatua zote za qualitative; yaani hatua zinazoanza uteuzi wa wagombea, mawakala, elimu ya mpiga kura, kituo cha kupiga kura, usimamizi, utangazaji wa matokeo, ujimuishaji wa matokeo na upingaji wa matokeo, haya ni maeneo muhimu mno katika kuthibitisha uthabiti wa mfumo wetu wa uchaguzi.
Katika hali tuliyoiona kama TLS tuliona mgawanyiko huu ni mkubwa sana na hauna afya. kwaiyo tulianza mchakato kwanza kujaribu kukutana na pande zote kila upande ambao una changamoto zake na tulikutana katika maeneo kila upande na eneo lake na baadae tukakutana nao pamoja kama taasisi. Kwenye taasisi za dini tulikutana na baadhi ya taasisis kama TEC, BAKWATA, CCT NA SHULE YA MA IMAM. Nia yetu ilikua kupata mtazamo wao kama viongozi wa dini wameona nini.
Pili tulijaribu kupata mawazo na kuonana vyama vya siasa vilevile lakini hivi tulienda kwenye vyama ambavyo ni member wa TCD ambao ni CUF, ACT WAZALENDO, CHADEMA, NCCR MAGEUZI na CCM. Katika vyama vya siasa kwa bahati mbaya wenzetu wa CCM hawakupata nafasi ya kushirikiana nasi japo tuliwaalika na tukasogeza hata mbele tena ili tuweze kukutana nao lakini walitujibu kwamba ofisi ya katibu wao mkuu haijateua mtu wa kuja kwa sababu wapo katika shughuli za uteuzi wa wagombea kwaiyo hawatoweza kufika.
Lakini vilevile tulikutana na watu mashuhuri, wenye heshima ana ushawishi katika masula ya kijamii, kisheria, kisiasa na kiuchumi. N atulikuatana nao ni muendelezo toka Aprili tunafanya iyo kazi kwa kutumia gharama na kiasi kidogo cha pesa tulichonacho lakini nia yetu ni kuhakikisha tunakua na Tanzania yenye haki, amani na yenye kuthamini utu.
Vilevile tulikuatana na asasi za kiraia katika michakato hiyo ya majadiliano kama legal human and huma rights centre, Tanzania human rights defender coalition, Tanzania women lawyer association, Tanznaia media women association, MCT Jukwaa la katiBa, Shirika la vijana la bridge for change, TWAWEZA pamoja na wengine. Wote hawa tulikuwa tunakutana ili kujaribu kuangalia mchakato na hali nzima ya kidemokrasia na namna ambavyo tuweze kuingia kwenye uchaguzi tukiwa wamoja, tufanye uchaguzi tukiwa wamoja asiwepo wa kuachwa nyuma.
Lengo kuu ya majadiliano haya yalikuwa ni kujadili masuala ya haki, amani na utulivu. Kwa sababu kumekuwa na msisitizo mkubwa sana wa amani katika taifa letu lakini watu wakasahau haki. Amani ni macho, haki ni nuru. Ukiwa na macho hakuna nuru huwezi kuona kwaiyo hakuna amani unayoweza kuizungumzia bila kuwa na haki. Kwaiyo lazima uanze na haki. Haki ndo inazaa matunda kama amani, furaha, mshikamano, umoja vyote vinatokana na haki.
Kwaiyo msisitizo wetu tulikua tunataka tuuangalie uchaguzi wetu kwenye mfumo wa haki, amani na utulivi. Na katika hili tuwapongeze wataalamu na kamati yetu ya kitaalamu wa TLS ya mabo ya sheria na katiba ilichambua sheria zote, kwaiyo tulikuwa hatufanyi kazi ya kubahatisha , tulisikiliza malalamiko anayesema nilishafanya marekebisho yamekamilika oktoba tunatiki, anayesema no refoems no election kwa nini na anayesema piga kura linda kura kwa nini.
Maeneo yote haya tuliyapitia, tuliyaangalia tuka identify na kupitia mijadala hii tuli identify maeneo 21 makubwa ya kikanuni lakini katika hayo maeneo 21 kuna maeneo 6 muhimu sana ya kikanuni ambayo tulifikiri kwa muda huu mchache uliobaki yakifanyiwa kazi tutaingia kwenye zoezi la uchaguzi tukiwa pamoja.
Lakini vilevile tuliangalia suala ala utulivu, haki na equitable participation kwenye democratic space, hatukufumbia macho kwa sababu tulikuwa tunaangalia kwa ukweli na usawa na mpja ya maeneo tuliyoangalia katika mkutano mkuu wa amani na maazimio na kupitia maazimio ya mkutano huo uliofanyika Agosti 19, 2025 jijini Dodoma tuliwakutanisha wadau wote wanaohusiana na masula ya uchaguzi, masula ya demokrasia na tukajadili kwa kina na tukaona kwa dhati kwamba lipo tatizo.
Tusikatae tuliona siyo vyema kupuuza malalamiko yanayotolewa na watu. Kwaiyo katika kikao cha wadau wote waliona ni muhimu kuunda kwa kamati shirikishi yenye uwakilishi mpana wa makundi yote ya kijamii ili kuainisha hatua za dharura za muda mfupi, muda wa wakati na muda mrefu kwa ajili ya kuhakikisha haki, amani na utawala bora unadumishwa nchini na kuhakikisha changamoto za zoezi la uchaguzi zinapatiwa ufumbuzi kwa njia ya mazungumzo na maridhiano. Kwaiyo kilicho zungumzika ni kwamba tatizo lipo na marekebisho yalifanyika lakini kuna maeneo muhimu ambayo yaliyotakiwa kufanyiwa marekebisho na yaliyokuwa na changamoto za kweli hayakuguswa kabisa na marekebisho.
Kwaiyo hoja ya CHADEMA kwamba kuna changamoto katika reforms ni halali huwezi kulipuuza kwa sababu uchaguzi una maeneo mawili, Qualitative na quantitave process na unapoona haki imekiukwa kuna taratibu za kufuata kisheria. Kama unalalmika kuliuwa na mgogoro ndani ya chumba Uonyeshe fomu namba 14 &15 iko wapi, uonyeshe barua ya uteuzi wa uwakala, uonyeshe fomu yako ya matokeo., sasa ukienda kwenye kanuni vyote hivi vimeonekana kwamba ni hiari kwamba unaweza ukapewa au usipewe lakini kwenye sheria imeachwa vilevile proof beyond reasonable doubt lakini kanuni inakunyanganya vidhibitisho vyote na kuweka ni hiari, na ndilo eneo lenye tatizo, huku ndiko watu wanakimbia na masanduku ya kura, huku ndiko zinakoletwa kura feki. sasa ukiwa na kanuni ambazo zinasaidia uhalifu yaani haziwork strictly adherance kazi ya kanuni ni kuipa nguvu sheria kuhakikisha ufanisi katika kufanikisha lengo.
“Sasa hivi kuna mashauri yanaendelea Mahakamani ni kauli za kisiasa kabisa, huyu ametoa kauli za aina hiyohiyo yupo uraiani hajaguswa, huyu katoa kauli ya namna ileile mwingine Mhaini, ni maoni ya Wadau suala la Lissu, tunaishauri Serikali liondoke Mahakamani, DPP anajua cha kufanya aliondoe Mahakamani Lissu aondoke”
“Kama Taifa tukitaka kupona lazima tuache unafiki, Lissu hakuongea gizani aliongea hadharani na wote tunajua kuna kauli kali zaidi zilitoka kuliko za Lissu lakini zile ni kauli za kisiasa, Mimi wakati nagombea sehemu fulani Mtu mmoja alisema mtamchaguaje Mwabukusi ana sura mbaya vile sikuchukulia upande hasi nilichofanya nikamleta Mke wangu nikampandisha jukwaani nikamwambia waambie Wapiga kura sura yangu unaionaje?, Mke wangu akasema nina sura nzuri nikawaambia Wapiga kura kama Mke wangu ameridhika wewe unayelalamika ni nani?, ni siasa”
“Kwahiyo kwenye siasa tuna lugha zetu za kuongea, ukianza kujinaisha kauli na mazingira ya kisiasa moja kwa moja lile ni shambulio dhidi ya demokrasia, Serikali imuachie Lissu, nimerudia Mahakama isitumike kama kokoro la kuvulia samaki na kuharibu matumbawe na tunasema hivi ili kuliponya Taifa”