Serikali imuandae Mbwana Samatta kuja kuwa kocha wa timu ya taifa

Serikali imuandae Mbwana Samatta kuja kuwa kocha wa timu ya taifa

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
15,692
Reaction score
23,038
Taifa Stars imetolewa kwenye mashindano ya fainali za OFCON za mwaka 2019, kwa kushindwa mechi zote tatu za awali.

Lakini kufukuzwa kwa Emanuel Amunike kuwe ni kigezo cha kuanza kuwatayarisha wachezaji wenye elimu ya mpira kutoka katika nchi zilizoendelea.

Katika nchi zilizostua wengi kwenye fainali za mwaka huu ni timu ya Madagascar au kwa jina la utani la Barea.

Madagascar inafundishwa na kocha mfaransa Nicolas Dupuls ambae aliwahi kuwa mchezaji aliecheza nafasi ya beki wa kushoto wa timu ya FC Souvigny.

Pia amewahi kuchezea timu ya FC Beaumont ya Marekani na baadae kuanza kufundisha mpira kweyne timu ya AS Yzeure ya Ufaransa.

Mwaka 2017 Dupuls aliteuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa Madagascar na kama Tanzania mwaka 2018 timu hiyo ikafuzu kucheza fainali za AFCON za mwaka huu nchini Misri.

Dupils bado ni mkurugenzi wa ufundi wa timu ya FC Fleury 91 ya Ufaransa na pia anaifundisha Madagascar.

Nchi nyingi sasa hivi zinatumia wachezaji wake wa kimataifa kufundisha timu za taifa za nchi zao au kuwa wachezaji wanafunzi yaani "understudy" kwa makocha wa kigeni ambao huja kwa mikataba maalum.

Tatizo kuwa nililoliona kwa wachezaji wetu na timu nzima ya taifa ni kuwepo kwa lugha- gongana inayofanya kazi ya ufundishaji kuwa ngumu na pia mawasiliano baina ya kocha na wachezaji kuwa si sahihi.

Tanzania kwa sasa ina wachezaji watatu tu wanaocheza mpira barani Ulaya ambako hata iwe ni timu ya daraja la tatu bado viwango vya mpira vipo juu kuliko Tanzania.

Pia mbinu za ufundishaji kutoka kwenye vitalu vya soka hadi kwenye timu za ligi mbalimbali pamoja na timu ya taifa ni za hali ya juu.

Mwaka huu tumeshuhudia fainali za kombe la dunia la wanawake ambapo timu za wanawake pamoja na waamuzi wameonyesha viwango vya juu vya uchezaji na usimamizi wa mpira wa miguu.

Kama taifa tukae chini tutafakari na tuje na uamuzi wa kuanza kuundeleza mpira wa miguu na michezo kwa ujumla.

Litakuwa ni jambo la busara na mbolea iwapo Bwana Samatta ataandaliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Tanzania kwa miaka michache ijayo pindi atakapoacha kucheza soka.

Huko aliko barani Ulaya kuna kozi maalum ambazo wachezaji wa zamani husomea na mwisho hupewa leseni maalum za kuanza kufundisha mpira wa kisasa kwa kutumia usomi na mbinu za kisasa za ufundishaji.

Kwenye mpira kuna vitu vitatu muhimu ambavyo timu ikikosa basi hushindwa kiujumla.

!. Mawasiliano baina ya kocha, jopo la ufundi na wachezaji ambalo wanapaswa kuongea lugha moja.

Madagascar wanatumia lugha ya kifaransa na hivyo kufanya kazi ya ufundishaji kwa wachezaji kuwa rahisi na tumeona matunda yake.

2. Mbinu za uchezaji - Timu kama haina mbnu za uchezaji basi huishia kufngwa mapema na kukata tamaa. Mbinu hizo ni pamoja na kuangalia kama mnacheza na timu kubwa au ngumu na kujaribu kwenda mapumziko mkiwa sare ya 0-0.

Mwisho mnajarbu kutafuta goli moja tu , na kuhaikisha mnalinda hilo goli kwa hali na mali.

3. Udhibiti wa mchezo yaani "Game Management" yaani kuhakikisha kila mchezaji anakuwa na nidhamu katika uchezaji bila kucheza rafu nyingi zisizo na maana na kuhakikisha wachezaji wote uwanjani wanawasiliana na kumsikiliza nahodha.

Hivyo basi serikali ifikirie kuwagharamia wachezaji khasa wale walio nje ya nchi barani Ulaya na iwe tayari kuwandaa khasa Bwana Samatta ambae anaonekana na uwezo mkubwa wa kuhamasisha timu hivyo kuifanya kazi ya ufundishaji kuwa rahisi.

Bila hivyo tutaendelea kushangaa timu kama Madagascra ikicheza robo fainali za AFCON 2019 na hata kufikia fainali.
 
Ushauri mzuri tatizo hakuna wazizi au kiongozi anaeharibu kuweka misingi ya mafanikio ya timu kwa hapo baadae

Wanachojali ni kuanagalia miaka mitano inakaribia kuisha nitateuliwa tena?
 
Naunga mkono hoja,ila hii tff na siasa

TFF inatakiwa ijitegemee kimawazo.

Yaani itafute washirika, wafadhili na wadau wengi wa michezo na iwashirikishe kikamilifu.

Wizara mtazamaji na kutoa ushauri.
 
Ukocha sio kusoma tu, ni charismatic. Ni lazima uwe na interest kwanza na kipaji cha kufundisha. Kwa nafasi yake pia hawezi kuwa kocha mzuri, labda umpe kazi ya kufundisha safu ya ushambuliaji tu kama ilivyokuwa kwa Kruvert pale Ajax.
 
Ukocha sio kusoma tu, ni charismatic. Ni lazima uwe na interest kwanza na kipaji cha kufundisha. Kwa nafasi yake pia hawezi kuwa kocha mzuri, labda umpe kazi ya kufundisha safu ya ushambuliaji tu kama ilivyokuwa kwa Kruvert pale Ajax.

Kwahio wadhani hata unahodha pia haumfai kwa kuwa sio charismatic?

Najaribu kukuelewa.
 
Mkuu ukocha ni suala jingine anaweza kuja kuwa kocha mzuri ama asiwe mzuri pia, Pele na mwenzie maradona wameshindwa kuwa makocha wazuri, plus wachezaji wazuri kibao..

Kikubwa sisi turekebishe mfumo wetu wa soka, wachezaji bora hawakurupuki tu wanaandaliwa!! Ukihesabu academy za maana kwa mchezo wa soka hakuna, wachezaji wanaocheza mbali pia hakuna...
Tusitegemee maajabu hata kama timu atapewa guardiola.
 
Guardiola ni mmoja was wachezaji wa zamani kufanikiwa kuwa kocha mzuri. Wengi wamechemsha.
Tusilazimishe. Anaweza kutokea ambaye hakucheza mpira kwa kiwango hicho.
 
Football ina Makocha wachache sana waliofanikiwa wakiwa na histroria ya kuwa wachezaji zamani!
 
Guardiola ni mmoja was wachezaji wa zamani kufanikiwa kuwa kocha mzuri. Wengi wamechemsha.
Tusilazimishe. Anaweza kutokea ambaye hakucheza mpira kwa kiwango hicho.

PEP ni charismatic sio elimu tu ya ukocha,
 
Guardiola ni mmoja was wachezaji wa zamani kufanikiwa kuwa kocha mzuri. Wengi wamechemsha.
Tusilazimishe. Anaweza kutokea ambaye hakucheza mpira kwa kiwango hicho.
👍
 
Write your reply....
kula sio sawa na kunywa ilhali vyote vinakaa sehemu moja.
kucheza na kufundisha ni tofauti kabisa.
umemuona huyo seedorf wa cameroon? ulimuona henry na monaco? ulimuona gary neville na valencia? usidhani kuwa kocha ni simple
 
Back
Top Bottom