DOKEZO Serikali imuangalie upya Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, Ayoub Rioba

DOKEZO Serikali imuangalie upya Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, Ayoub Rioba

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

UKWELI24

New Member
Joined
May 9, 2024
Posts
2
Reaction score
1
Awali ya yote ni vyema kutambua juu ya umuhimu wa Shirika la Utangazaji la Taifa duniani kote, kwa kawaida tunapozungumzia sehemu nyeti za kitaifa kama vile makambi ya Jeshi, Jengo la Taifa (Ikulu), vituo vya kuzalisha Umeme, vituo vya kuzalisha Gesi ghafi au asilia, Miundombinu ya kitaifa kama vile Reli pamoja na matangi ya kuhifadhi maji yanayotumiwa na jamii kwa ujumla wake hizi ni baadhi ya sehemu ambazo nyeti kwa usalama taifa.

Sasa turudi kwa mlengwa ambaye ni Shirika la Utangazaji la Taifa, Kiukweli shirika la hilo nalo ni sehemu nyeti kwa usalama wa Taifa yaani kuanzia ngazi ya chini mpaka ngazi ya juu kabisa zote hizo zinahitaji umakini wa hali ya juu hasa katika ushirikiano, uzingativu wa eneo lote, mahusiano mema kwa kila mtumishi wa shirika, uwazi na uwajibikaji usio na matabaka, fitina, kutishana, kunyanyasana au uhasama wa aina yoyote ile. Uzingativu mwingine ni juu uendeshaji wa mifumo ya utangazaji yaani mifumo ya ndani.

Hivi karibuni serikali ilimuongezea Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt. Ayub Rioba miaka miwili ya kulisimamia Shirika la Taifa, tukumbuke tu kuwa Ayub aliteuliwa rasmi machi 19, 2016 na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ambapo alichukua nafasi ya Mzee Clement Mshana alipostaafu utumishi wa Umma.

Kwa kipindi kirefu cha uongozi wa Ayub Rioba umekuwa na mashaka sana, kinachonishangaza mamlaka husika za uteuzi zimeshindwa kufuatilia na kujua matatizo ya kiutendaji yaliyopo ndani shirika hilo, huyu bwana kwa mda mrefu amekuwa na sifa ambazo hazina ufanisi kiutumishi hasa kwa nafasi nyeti kama hiyo, endapo mamlaka zitataka kujua basi zifanye uchunguzi kwa namna yoyote ile ndani ya shirika hilo zitapata kujua nini kinaendelea.

Watumishi wengi ndani ya TBC wananyanyasika na wananyanyaswa na Ayub Rioba, huyu bwana amekuwa akifanya mambo ya kulidumaza shirika kwa kuwafanya watumishi kuwa watumwa katika uongozi wake, amekuwa na sifa za kuwafanyia fitina watumishi pindi wanapoonesha ubunifu ktk utendaji yaani chuki binafsi inayoendana na kuwapa makosa yasio ya ukweli kwa watumishi ambao hawakubali, amekuwa akitumia ofisi ya Umma kama chumba chake binafsi cha nyumbani.

Rushwa ya ngono imekithiri ndani ya shirika iwe usiku au mchana , endapo mtumishi asipo mkubali Ayub basi huyo atakwenda na maji aidha kwa kuhamishwa kwa kutupwa mbali au kutengenezewa mazingira ya kufukuzwa kazi, Ayub ni bingwa wa kutoa bahasha za rushwa kwa mtu ambaye atakuwa anamkosoa kwa utendaji wake yaani katengeneza mazingira ndani ya shirika kuwa yoyote atayemsema basi arekodiwe na apelekewe hiyo audio kisha yeye anatoa bahasha kubwa ya asante, kiutuimishi hii ni rushwa ya kiutndaji, ni vyema TAKUKURU mkafuatilia hilo.

Katika kipindi hiki cha Digital Era ya Broadcasting and Management ulimwenguni kote ikiendelea kufanyiaka kila siku kwa TBC itakuwa ngumu sana kufanyika endapo Serikali itaendelea kusubiri akili za Ayub zifanye mageuzi kama mashirika mengine ya kitaifa yanavyofanya tuchukulie mfano kwa KBC , UBC. SABC.

Maadili ya Utumishi wa Umma yanajulikana bila kujali wewe ni kiongozi wa ngazi gani lakini cha kujiuliza kiongozi mkuu wa shirika kwanini uingie ofisini na silaha ya moto? Kwanini kiongozi utumie maneno ya matusi kwa mtumishi mwenzako? Kwanini ufungie watu ofisi angali unajua hii ni ofisi ya umma? Kama kiongozi ambaye ni kioo kwa wasaidizi wako kwanini utengeneze makosa ya makusudi kwa msaidizi wako angali unajua kabisa kuna ugeni mkubwa wa kitaifa unakuja kwako? Kwanini utafute mtu asie na sifa kwa maslahi yako umtoe mwenye sifa wakati unajua kabisa hilo ni shirika la Umma /Taifa lengo lako ni nini? Na kwanini wewe Ayubu ulazimishe ngono kwa mtumishi bila ridhaa yake? Zote hizo ni sifa mbaya sana kwa kiongozi mwenye kuongoza Shirika nyeti kwa maslahi ya Taifa.

Mwenye masikio na asikie na Mwenye Macho atizame , ....................

9/5/2024
 
Back
Top Bottom