Serikali imulike tatizo la wapiga debe nchini

Serikali imulike tatizo la wapiga debe nchini

narogo

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2021
Posts
2,765
Reaction score
2,707
Kwa muda mrefu hawa wapiga debe wamekuwa sio tu kero bali pia wanaongeza kupanda kwa nauli za mabasi.

Yaani hata wenye vyombo vya usafiri twawaogopa. Hata ukiwa na gari yako binafsi huwezi kuchukua abiria au hata kumpa lifti jamaa yako kwa kuwa tu wao huwa wanajimilikisha hao abiria na ukithubutu kuchukua abiria wako tayari kupasua vioo vya gari lako.

Pendekezo la suluhisho:
SUMATRA wapitie upya nauli za mabasi, wapunguze ili kupunguza nguvu ya wenye mabasi kuwapa cha juu wapiga debe,
Ni kwa wenye mabasi hutoza nauli halali kama ilivyopangwa na SUMATRA, lkn wao wanachukua kama 80% na inayobaki huwa
ya wapiga debe.

Nimekuwa ikisafiri na gari yangu nnapotaka kuchukua abiria ni lazima mpiga debe aingilie kati. Anakupangia nauli, yeye anakusanya
kutoka kwa abiria halafu anakata karibia Nusu! Inauma sana kwa kweli!!
Gari langu,
Mafuta yangu
Abiria nimewaona mwenyewe Barabarani,
Wamekuja kwa hiari yao,
Halafu wahuni fulani wananini nini sijui.. Ah!!
 
Acha kilialia lia niko hapa Kibo nauli ninelf 40 kwenda Mosh tu ..na hakina anayelalamika
 
Nauli Mwanza-Kigoma ni 20k lakini wapiga debe wameipandisha mpaka 31k, hiyo 11k wanakula wao
 
Kata leseni ya kubeba abiria awatokusumbua wapiga debe
 
Hivyo ni vinasaba vya watu wote hii nchi, ndio maana hata viongozi wanapenda 10%.

Hili tatizo la wizi na udalali ni changamoto na tujitafakari kama taifa usiwanyoshee kidole hao tu.
 
Nauli mwanza-kigoma ni 20k lakini wapiga debe wameipandisha mpaka 31k, hiyo 11k wanakula wao
Katia kwenye basi stand asubui wakati wa kuondoka utalipa hio 20,bado mnakata tiketi vijiweni
 
Binafsi ninawachukia sana wapiga debe. Mimi sioni tija yao katika jamii licha ya kuwaibia abiria na kupata fedha za bure.
 
Kwa muda mrefu hawa wapiga debe wamekuwa sio tu kero bali pia wanaongeza kupanda kwa nauli za mabasi.

Yaani hata wenye vyombo vya usafiri twawaogopa. Hata ukiwa na gari yako binafsi huwezi kuchukua abiria au hata kumpa lifti
jamaa yako kwa kuwa tu wao huwa wanajimilikisha hao abiria na ukithubutu kuchukua abiria wako tayari kupasua vioo vya gari lako.

Pendekezo la suluhisho:
SUMATRA wapitie upya nauli za mabasi, wapunguze ili kupunguza nguvu ya wenye mabasi kuwapa cha juu wapiga debe,
Ni kwa wenye mabasi hutoza nauli halali kama ilivyopangwa na SUMATRA, lkn wao wanachukua kama 80% na inayobaki huwa
ya wapiga debe.

Nimekuwa ikisafiri na gari yangu nnapotaka kuchukua abiria ni lazima mpiga debe aingilie kati. Anakupangia nauli, yeye anakusanya
kutoka kwa abiria halafu anakata karibia Nusu! Inauma sana kwa kweli!!
Gari langu,
Mafuta yangu
Abiria nimewaona mwenyewe Barabarani,
Wamekuja kwa hiari yao,
Halafu wahuni fulani wananini nini sijui.. Ah!!
Yaani unasimamisha gari yako mwenyew bila appointment na mpiga debe ,halafu anakuja mpga debe na sigara yake mkonon na kikombe cha kahawa kavaa mlegezo hataree anakuulza bro unaelekea wapi?

Unamwambie huku abria wameanza kusogea halafu anawambia " leteni nauli hyo faster wenye halaka choma ndani wew mama njoo ukae huku mbele nipe kabsa nauli yako" Ina kera sana jamani. Pale Nzega njia panda
 
Wapiga debe ni tatizo la uchumi, kazi nyingi za vijana kwa sasa ni bodaboda, umachinga, udalali na kupiga debe.
 
Yaani unasimamisha gari yako mwenyew bila appointment na mpiga debe ,halafu anakuja mpga debe na sigara yake mkonon na kikombe cha kahawa kavaa mlegezo hataree anakuulza bro unaelekea wapi? Unamwambie huku abria wameanza kusogea halafu anawambia " leteni nauli hyo faster wenye halaka choma ndani wew mama njoo ukae huku mbele nipe kabsa nauli yako" Ina kera sana jamani. Pale Nzega njia panda
Nimekutana nayo hiyo Uyole Mbeya Na Ipogolo Iringa...
 
Hili ni tatizo la kitaifa na ni bomu kubwa kuliko hata la wamachinga,maana machinga hawana sifa mbaya kama hizi za wapiga debe.

Mfano
kubwia unga,unywaji holela wa pombe bila kuzingatia muda,uchafuzi wa mazingira kwa kukojoa ovyo kwenye vichochoro vya stand za nabasi, uchomozi na wizi kwa mizigo ya abiria.

Serikali inapaswa kuliangalia hili tatizo na kulitafutia ufumbuzi wa kina na wa kudumu.
Kadri inavyozidi kulipuuza ndivyo litakavyokuja kusumbua kuliko tunavyofikiria,maana kila uchao idadi yao inazidi kuongezeka.
 
Back
Top Bottom