Ndugu wana JF, kila mmoja amesoma tamko la hasira la Marekani juu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ndugu Paul Makonda.
Kwa desturi za USA, mlengwa mkuu hapo ni Rais Magufuli na serikali yake, walichofanya ni kuipima serikali yetu itamfanya nini Makonda baada ya wao kutangazia Dunia kuwa hawataki akanyage Marekani.
Makonda asipoondolewa, tujiandae kususiwa na Dunia nzima, maana Marekani ndio taifa lenye nguvu za kila aina Duniani.
Hata mataifa yanayojitegemea Kiuchumi yana ufyata kwa Marekani, sembuse sisi tunaojitegemea kwa asilimia 56%? Huku 44% tukitegemea kusaidiwa na Mabeberu?
Kama unajua trend reading, Ubalozi Marekani walikuwa wanatoa taarifa inayofanana na balozi nyingine kama ubalozi wa Ulaya, Uingereza nk.
Usishangae ndani ya siku chache ukawasikia washirika wa Marekani nao wakimpiga marufuku Makonda kukanyaga huko.
Kama serikali ikizembea kumfukuza Kazi Makonda ili kujisafisha, usishangae likatoka tamko la kuzuia misaada kwa Tanzania, halafu tuwekewe na vikwazo ikiwa ni pamoja na kuzuia watalii wasije Tanzania kwakuwa ni nchi hatari kiusalama.
Wazungu wanaweza kutukumia vyovyote, hambo la msingi na haraka ni kumuondoa Makonda ofisini na kuteua mtu mwingine atakaefanya tofauti.
Chonde Chonde washauri wa Rais Magufuli, tunawapenda sana na tunaipenda serikali yetu, Makonda Mmoja asiingize nchi kwenye mgogoro wa Kidiplomasia.
Sent using Jamii Forums mobile app