HOJA Serikali ina mpango gani wa kumsaidia Mkulima wa Mahindi nchini?

HOJA Serikali ina mpango gani wa kumsaidia Mkulima wa Mahindi nchini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
SERIKALI INA MPANGO GANI WA KUMSAIDIA MKULIMA WA MAHINDI?

Tanzania kwa sasa ina uzalishaji mkubwa wa mahindi, lakini NFRA imetangaza kununua mahindi kwa Sh 450 kwa kilo, wakati mwaka jana (2025) bei ilifika karibu Sh 700 kwa kilo.

Wakati huo huo, gharama za uzalishaji zimekuwa zikiongezeka kila mwaka.

Kwa mfano, mwaka jana mfuko mmoja wa mbolea ulikuwa takribani Sh 78,000. Kwa mkulima anayehitaji mifuko 4 kwa ekari moja, mbolea pekee inagharimu takribani Sh 312,000 kwa ekari, bila kuhesabu mbegu, kulima, kupanda, kupalilia, dawa, kuvuna na kusafirisha.

Ikiwa ekari moja inazalisha takribani tani 2 za mahindi, kwa bei ya Sh 450 kwa kilo, mkulima anapata takribani Sh 900,000 kwa mavuno yote kabla ya kutoa gharama nyingine zote kwa bei ya sasa. Hapo, achana na gharama za kuandaa mahindi ili yaweze kukidhi vigezo vya kuuza NFRA, kama kupepeta na kuchagua magunzi na mahindi mabovu.

Swali ni hili:

Tunapomhamasisha mkulima azalishe zaidi, Serikali ina mpango gani kuhakikisha uzalishaji huo unamletea mkulima kipato na si hasara?

Kenya imekuwa moja ya masoko muhimu ya mahindi yetu. Lakini sasa Kenya imeingia makubaliano ya kununua mahindi kutoka Zambia kwa kiwango kikubwa.

Kwa hiyo wakulima tunaomba mlengo wa wazi wa serikali kuhusu:

  • Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha mkulima anapata bei inayolingana na gharama za uzalishaji?
  • Serikali ina mpango gani wa kutafuta na kulinda masoko ya mahindi ndani na nje ya Tanzania?
  • Wakati uzalishaji unapokuwa mkubwa kuliko mahitaji ya ndani, Serikali itafanya nini ili mkulima asiuze kwa hasara?
  • Je, kuna mpango wa kupunguza zaidi gharama za pembejeo, hasa mbolea na mbegu?
  • Je, sera ya kudhibiti mipaka na wafanyabiashara kusafirisha mahindi nje ya nchi inamsaidiaje mkulima anaelima kwa ajili ya chakula na ziada ya biashara. Tukumbuke kuna baadhi ya mikoa, mahindi ndio zao mama.
  • Na muhimu zaidi, Tanzania ina mpango gani wa muda mrefu wa kuhakikisha kuongeza uzalishaji wa kilimo kunaongeza kipato cha mkulima, badala ya kushusha bei ya mazao yake?

Mkulima akizalisha kwa hasara, kesho atapunguza uzalishaji. Na akipunguza uzalishaji, nchi yetu itarudi kwenye tatizo la upungufu wa chakula.

Hivyo, suala la bei ya mahindi si suala la mkulima wa mahindi pekee. Ni suala la kipato cha mkulima, usalama wa chakula na uchumi wa nchi, na ustawi wa familia zao iliwa kumudu gharama za maisha ya kila siku pamoja na ada za watoto wao.

Tunaomba kusikia mkakati wa Serikali wa kumlinda na kumuinua mkulima wa mahindi.

Asante.
 
Mkuu kiukweli kabisa viongozi tulionao siku zote huwa nasema wana akili kisoda mno...kwanza hata wao wenyewe hawajui hata jinsi ya kumkomboa mkulima zaidi ya janjajanja za kitapeli za kicccm
watu wanazidi kupoteza matumaini
 
Fikiria mkulima wa korosho,mbaazi na ufuta anabeba mazao yake na kuyapeleka kwenye maghala ya vyama vya ushirika bila kujua bei dira
stakabadhi ghalani ni kama mchezo wa bahati nasibu
 
Back
Top Bottom