Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Niliwahi kuambiwa hospitali na zahanati huwa zinabanwa kufanya matangazo ya kibiashara kuvutia wateja kwenye vyombo vya habari kwa sababu za kimaadili ya afya, sina uhakika kama kuna sheria au kanuni rasmi katika kuratibu matangazo yao lakini huu ni utaratibu ambao ungefaa zaidi kwa "huduma za kidini"
Vyombo vingi vya habari(radio na TV) siku hizi vina matangazo ya kibiashara ya makanisa mbalimbali hasa haya ya manabii wa kisasa yakihamasisha watu kufika katika makanisani au katika mikutano yao kupata utatuzi wa shida zao na kubarakiwa. Pia kuna masheikh mbalimbali wamekuwa kwenye vyombo vya habari wakitangaza huduma zao.
Serikali izuie matangazo yote ya aina hiyo kwa sababu madai ya hayo makanisa na ma-sheikh ni mambo yasiyoweza kuthibitishwa kwa aina yoyote ile na serikali yenyewe. Yanaweza kuwa na mambo ya hadaa na utapeli tu au vinginevyo na serikali inao wajibu wa kuzuia raia wake kuingiziwa kwenye aina yoyote ile ya utapeli.