macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Upo sahihi mno mno. Na pia maisha yanapokuwa magumu wananchi wanapumbazwa kuwa ni ''kazi ya shetani'' hataki maendeleo yao. Magonjwa nayo tunaambiwa ni mapepo na wanga hivyo suluhisho ni kuombewa na siyo kwenda hospital. Bado huweka ''unabii'' wa kusema wameoteshwa fulani ndiye rais bora.Je, unafahamu kwamba serikali ni mnufaika mkubwa wa uwepo wa hizo dini na madhehebu yake kuliko wananchi wenyewe?
Uwepo wa hayo madhehebu na dini unasaidia kuwapumbaza na kufubaza fikra pevu za wananchi, na kupelekea wananchi kuamini katika uchawi, ushirikina au miujiza inayopatikana kwenye dini au kwenye Imani.
Ukitaka kuamini angalia jinsi hao viongozi wa dini wanavyopewa promo na kusapotiwa na serikali.