Serikali ina wajibu wa kuzuia matangazo ya kibiashara ya kidini/imani kwenye vyombo vya habari kulinda raia wake

Upo sahihi mno mno. Na pia maisha yanapokuwa magumu wananchi wanapumbazwa kuwa ni ''kazi ya shetani'' hataki maendeleo yao. Magonjwa nayo tunaambiwa ni mapepo na wanga hivyo suluhisho ni kuombewa na siyo kwenda hospital. Bado huweka ''unabii'' wa kusema wameoteshwa fulani ndiye rais bora.
 
Je, ulishawahi kufikiria hao wananchi wenye matatizo mbalimbali wakiamua kuacha kwenda kwa manabii na madhehebu yao na kuamua kutafuta suluhisho kupitia serikali au watawala ni nini kitatokea?

Tutafakari kwa pamoja.
 
Mkuu hili swali la msingi sana likitafakariwa kwa kina!
 
Hata waganga wa kienyeji hujitangaza kwenye vyombo vya habari kwa uhuru kabisa.
.......sisi kama serekali rumetenga fungus la Tsh. Billion kadhaa mwaka... Kwa ajiri ya utafiti, Ili kubaini kwanini jamii haipaendi kutumia huduma za hospitali, na wanaoenda hospital huwa wamechelewa...............
 
Je, ulishawahi kufikiria hao wananchi wenye matatizo mbalimbali wakiamua kuacha kwenda kwa manabii na madhehebu yao na kuamua kutafuta suluhisho kupitia serikali au watawala ni nini kitatokea?

Tutafakari kwa pamoja.
Huduma hazitatosha!
Pia tunazo emotion induced sicknesses nyingi ktk jamii zikitokana na changamoto za kiuchumi na kijamii.
 
Je, ulishawahi kufikiria hao wananchi wenye matatizo mbalimbali wakiamua kuacha kwenda kwa manabii na madhehebu yao na kuamua kutafuta suluhisho kupitia serikali au watawala ni nini kitatokea?

Tutafakari kwa pamoja.
Yatatokea mabadiliko ya kweli na viongozi watabadilika na kuwajibika kwa wananchi.
 
Je, ulishawahi kufikiria hao wananchi wenye matatizo mbalimbali wakiamua kuacha kwenda kwa manabii na madhehebu yao na kuamua kutafuta suluhisho kupitia serikali au watawala ni nini kitatokea?

Tutafakari kwa pamoja.
Watakosa wateja(wafuasi ) hivyo biashara (kanisa)litakufa na hivyo matangazo nayo yatoweka
 
Jumuiya za makanisa na misikiti nazo hulipa Kodi na zinatambulika kama 'legal persons' - zinaweza kushtaki na kushtakiwa. Hivyo, zina haki ya kunufaika na huduma zinazotolewa nchini. Ili zizuiwe ni lazima kuwe na uthibitisho wa huo utapeli. Sasa utathibitishaje kuwa hayo matangazo yanayotolewa ni ya kitapeli?
 
Hapana, taasisi za kidini hazilipi kodi.
Pia kuzuiwa kwao kutangaza ni kwa sababu za kimaadili(ethics) zaidi kama vile hospitali na law firms zinavyobanwa kufanya commercial marketing.
 
Mbona matangazo ya kubeti yanaendelea bila shida? Mwisho wa siku, raia si anapigwa tu kama anavyopigwa huko kwenye dini?
 
Mbona matangazo ya kubeti yanaendelea bila shida? Mwisho wa siku, raia si anapigwa tu kama anavyopigwa huko kwenye dini?
Matangazo ya betting huwa yana angalizo "bet kistaarabu", nchi nyingi duniani pia zinazuia matangazo ya kamari.
 
Hapana, taasisi za kidini hazilipi kodi.
Pia kuzuiwa kwao kutangaza ni kwa sababu za kimaadili(ethics) zaidi kama vile hospitali na law firms zinavyobanwa kufanya commercial marketing.
Nani kakwambia kwamba hazilipi kodi? Kusajiliwa wanalipia. Kununua kiwanja sehemu ya kujenga kanisa, shule, chuo, hospitali, benki etc wanalipia, vifaa vya ujenzi wanalipia, etc. Zimesamehewa tu kwa baadhi ya huduma zinazotoa. Ngoja niseme kwa upande wa Kanisa Katoliki kwa vile na mimi ni Mkatoliki. Kanisa Katoliki linatoa huduma mbalimbali. Mfano, lina shule mbalimbali na vyuo, benki na limeajiri watu wanaoendesha hizo shule, nyuo, benki na wanalipwa mshahara na wako entitled kwa mafao mbalimbali kama vile bima ya afya/maisha, NSSF na pension etc, unadhani nani anachangia hizo gharama? Labda niachie hapa kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…