Ndata
JF-Expert Member
- Mar 2, 2017
- 226
- 329
Serikali inaagiza sukari nje karibu kila mwaka wakati Tanzania inaweza kuwa inaongoza kwa uzalishaji wa muwa unaoachwa ufie shambani kwa maslahi ya wachache.
Mwaka 2022 nimechoma zaidi ya tani elfu moja kwa kigezo cha muwa umepitiliza muda wa kutengeneza sukari. Tani elfu moja ni tunaongelea million 40 baada ya makato yote.
Huu ni mchezo unaofanywa na Kagera Sugar wakishirikiana na vyama vya ushirika kumuumiza mkulima aachane na muwa ili Kagera Sugar aendelee kwa kutumia muwa anaolima mwenyewe.
Mwaka huu ratiba inaonyesha nilitakiwa kuvuniwa tar 30 june ila mpaka sasa July inaenda mwishoni sijaona navuniwa wala kupewa habari yoyote.
Bashe na wizara yake wapo kimya, serikali ya Ccm ipo kimya mkulima akiendelea kunyanyaswa.
Ni kwanini wakulima wa muwa wasipewe vibali kuuza muwa nje ya nchi kama mazao mengine?
Wakati wakulima wa Morogoro wakilipwa 108000 kwa Tani Kagera bado tani inalipwa elfu 70 na bado mkulima havuniwi mpaka muwa unachomwa moto kuteketezwa.
Wana jamii forum nawaomba tuutembeze huu uzi mpaka uwafikie wahusika.