Serikali inaagiza sukari nje karibu kila mwaka wakati Tanzania inaweza kuwa inaongoza kwa uzalishaji wa muwa unaoachwa ufie shambani

Duh! Tatizo letu sio upungufu bali ni kushindwa kuwa na mipango inayohimili misimu yote. Ya miwa mingi na ya miwa kidogo.

Ndiyo maana zikinyesha mvua umeme unakatika kisa maji yamezidi na zikipungua pia umeme unakata kwamba maji hayatoshi.

Kwa watu wenye akili tatizo linabidi libakie moja tu au yasiwepo yote. Kuwepo kwa matatizo yote ni upungufu wa akili tu ya kuyatawala mazingira


Hiyo miwa kama vipi ikizidi tuzalishie pombe tupunguze utegemezi wa petroli kutika nje. Mambo ya kufanya ni mengi tu tukiweka akili hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…