PostGE2025 Serikali inaandaa mpango wa kuwarejesha kazini waandishi wakongwe waliokosa vigezo vya ithibati. Kwanini baada ya Uchaguzi?

PostGE2025 Serikali inaandaa mpango wa kuwarejesha kazini waandishi wakongwe waliokosa vigezo vya ithibati. Kwanini baada ya Uchaguzi?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
Wakuu,

Baada ya wananchi kuwakataa waandishi wa habari sasa relikali inakuja na mbinu ya kuwarudisha wakongwe ili kurudisha imani na kuendeleza uchawa? Miaka tu ya wao kuwa kazini inatosha wao kupewa ithibati? Hii ina athari gani kwenye sekta ya habari? Kwanini baada ya uchaguzi? Tukirudi kwenye mzizi wa tatizo, hivi JAB inatakiwa kweli kuwasimamia waandishi? Inawasimamia au inawadhibiti?

======


"Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuandaa mpango maalumu utakaolenga kuwawezesha waandishi wa habari wakongwe ambao, kwa sababu moja au nyingine, wamekosa sifa za kuwa na ithibati ya kuwa waandishi wa habari. Huu ni utekelezaji wa Sheria yetu ya Huduma za Habari ya mwaka 2016, Sura namba 229.

"Hiyo ni moja ya programu ambazo tunakusudia kuzifanya katika mwaka 2025, 2026, na 2027. Kama ambavyo Mheshimiwa Waziri, Paul Christian Makonda, alisema katika uwasilishaji wa bajeti, Bodi ya Ithibati inakamilisha mwongozo ambao tunatarajia uanze kutumika mwezi Julai mwaka huu.


Pia soma GE2025 - Waandishi ambao hawajasajiliwa JAB marufuku kuripoti Uchaguzi Mkuu

"Kuonekana kwa mwongozo huu hakutoi nafasi ya moja kwa moja kwa kila ambaye amekosa sifa kuruhusiwa kupata ithibati na kufanya kazi za uandishi wa habari. Huu ni mwongozo ambao utatoa fursa kwa watu ambao wamekosa sifa lakini wamekuwa wakifanya kazi ya uandishi wa habari kwa miaka mingi ili waweze kuruhusiwa kufanya kazi ya habari.

"Pia, mwongozo huu utatoa fursa kwa wale wanaoweza kujiendeleza, wajiendeleze. Lengo kuu la kuwa na ithibati kwa waandishi wa habari ni kuifanya kazi hii kuwa ya kitaaluma zaidi. Hatutaki kuwa na watu wanaofanya kazi ya uandishi wa habari wakati hawajasomea, hawajui misingi yake, maadili yake, wala miiko yake.

"Tunataka mwandishi akishika maikrofoni au akiwa studio, asiweze kuleta madhara kwa chombo chake cha habari kwa kutangaza vitu visivyozingatia misingi ya uandishi wa habari. Serikali inatambua kuwa wapo watu ambao, pamoja na kwamba hawakuwa na sifa za kitaaluma, walifanya kazi zao vizuri kwa muda mrefu sana. Hivyo, tutaweka utaratibu mzuri wa namna gani wataendelea kufanya kazi."
 
Na ukikaribia uchaguzi ujao wanaenda bench tena 😀 Ila washkaji kwanini wasisome, siku hizi elimu kila mahali hadi inakufata ulipo kupitia online. Utumwa mdogo mdogo wa wanasiasa unaepukika..
 
Waandishi waliowekwa bench kwa hiyo idhibati watakaorudi ni wale wasio na ujanja nje ya huo uandishi wa habari. Yaani wabunge wanaotunga sheria wanapatikana bila kujali elimu, ila watangazaji wanatakiwa wawe na vyeti? Ile idhibati lengo lake lilikuwa ni kuwapiga stop waandishi kadhaa waliokuwa wanajitahidi kuongea ukweli.
 
Back
Top Bottom