carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Serikali ya Tanzania imesema inaendelea kutathmini ufanisi, muda wa kinga na gharama za chanjo ya malaria kabla ya kuamua matumizi yake nchini, ikilenga kuhakikisha chanjo itakayochaguliwa inatoa kinga inayokidhi mahitaji ya wananchi na kuendana na uwezo wa mfumo wa afya.
Hata hivyo, Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoshiriki katika tafiti za kisayansi zilizochangia maendeleo na tathmini ya chanjo za malaria ambazo tayari zimeidhinishwa na kuanza kutumika katika baadhi ya nchi duniani.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu, Novemba 2, 2026 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Grace Magembe, wakati akizindua mkutano wa wataalamu wa kuandaa Taarifa ya Maendeleo ya Mapambano dhidi ya Malaria ya Umoja wa Afrika (AU), unaofanyika Dar es Salaam Novemba 2 na 3, 2026.
Dk Magembe amesema Tanzania inaendelea kushiriki katika tafiti za chanjo mbalimbali ili kubaini zile zenye ufanisi unaokidhi mahitaji ya wananchi. Amesema tathmini hizo zinazingatia muda wa kinga, gharama, uhifadhi na usafirishaji wa chanjo hizo.
Amesema ni muhimu kuhakikisha chanjo itakayochaguliwa inaweza kutolewa kwa ufanisi na kuendana na mazingira na uwezo wa mfumo wa afya nchini.