Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi ili kukuza uchumi

Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi ili kukuza uchumi

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Katibu Mkuu Wizara ya UItamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi hatua inayosaidia kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu ambayo ndio msingi wa maendeleo ya sekta
nyingine.

Katibu Mkuu Bw. Yakubu amesema hayo Juni 17, 2023 wakati wa Mahafali ya 13 ya Shule za Kimataifa za Feza

“Tunapaswa kutambua vipaji vya watoto na vijana katika michezo na utamaduni, hivyo tulilazimika kuwa na programu zinazojumuisha utendaji wa kitaaluma na kukuza vipaji kwa wanafunzi wetu kwa manufaa ya kijamii na kiuchumi” amesema Bw. Yakubu.

Aidha, amewasihi Viongozi na walimu wa Shule za Kimataifa za Feza kuendelea kuthamini na kutekeleza moja ya haki za Mtoto zinazohusiana na Michezo na Utamaduni ambayo inafafanua haki ya Watoto kucheza na kushiriki katika shughuli za michezo na kitamaduni kwa manufaa ya kimwili, kiakili na kiafya.

Michezo inatoa ajira kwa vijana wengi Tanzania, Afrika na duniani kote na ni moja kati ya shughuli muhimu zinazopaswa kutekelezwa kwa kuzingatia azimio la mkutano wa Umoja wa Vijana wa Utamaduni na Michezo wa Umoja wa Afrika wa mwaka 2016.​
 
Katibu Mkuu Wizara ya UItamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi hatua inayosaidia kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu ambayo ndio msingi wa maendeleo ya sekta nyingine.

Katibu Mkuu Bw. Yakubu amesema hayo Juni 17, 2023 wakati wa Mahafali ya 13 ya Shule za Kimataifa za Feza kwa manufaa ambapo wanafunzi wa shule ya msingi darasa la sita, sekondari darasa la 11 na 13 wamehitimu masomo yao.

“Tunapaswa kutambua vipaji vya watoto na vijana katika michezo na utamaduni, hivyo tulilazimika kuwa na programu zinazojumuisha utendaji wa kitaaluma na kukuza vipaji kwa wanafunzi wetu kwa manufaa ya kijamii na kiuchumi” amesema Bw. Yakubu.

Aidha, amewasihi Viongozi na walimu wa Shule za Kimataifa za Feza kuendelea kuthamini na kutekeleza moja ya haki za Mtoto zinazohusiana na Michezo na Utamaduni ambayo inafafanua haki ya Watoto kucheza na kushiriki katika shughuli za michezo na kitamaduni kwa manufaa ya kimwili, kiakili na kiafya.

Michezo inatoa ajira kwa vijana wengi Tanzania, Afrika na duniani kote na ni moja kati ya shughuli muhimu zinazopaswa kutekelezwa kwa kuzingatia azimio la mkutano wa Umoja wa Vijana wa Utamaduni na Michezo wa Umoja wa Afrika wa mwaka 2016.View attachment 2661438View attachment 2661440View attachment 2661443View attachment 2661442View attachment 2661439View attachment 2661444View attachment 2661441
IMG-20230618-WA0303.jpg
View attachment 2661445
 
Back
Top Bottom