Serikali inafahamu juu ya Huu Uhuni/Wizi unaoendelea hapa Shekilango/Urafiki??

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,988
Reaction score
30,183
Wakuu Kwema?

Niende Kwenye Mada, Shemeji yenu ni mtu wa kutoka Mikoa ya kaskazini, na kama mnavyojua kila ikifika tarehe kama hizi basi Pilika pilika za kueleke maeneo/mikoa hiyo hua zinakua nyingi sana. Mimi kwa kujua hilo ulipoanza huu mwezi tu nikaenda hapo Ubungo kwa ajili ya kumkatia shemeji yenu ticket, yeye antarajia kusafiri tarehe 22 ndo likizo yake inaanza.

Sasa siku hiyo nilipoenda tarehe 1 hiyo nikaambiwa utaratibu ni kua Tickets za tarehe yoyote huanza kukatwa/booked siku zisizozidi 5 kabla ya safari. Ndo kusema kua kwa taerehe hiyo 1, ticket pekee nayoweza kukata ni kuanzia tarehe 01 mpaka 05, sio zaidi ya hapo. Na nikitaka ya tarehe 25 basi nije kuanzia tarehe 20. Nikasema ngoja nizunguke kwenye makampuni mengine pengine wako na utaratibu tofauti. Eneo hilila Shekilango lina Kampuni za Mabas za nazozikumbuka za Kidia One, Marangu Coach, Esther, Kilimanjaro, Dar Express, Dar Lux, Happy Nation, BM Coach. Kote nilikopita utaratibu ulikua ni huu huu. Hakuna alienikubalia kukata ya tarehe 22.

Nikaondoka huku nikipiga hesabu kua nikienda kuanzia tarehe 18 December (Leo) nitapata ticket nayoitaka. Nimeenda leo hapo Urafiki kwa ticket ya tarehe 22 nkakosa. Kampuni moja nkaambiwa zimeisha toka juzi, nkawauliza kwani walishaanza kuziuza toka juzi, wakasema ndiyo. Nkazunguka tena kutafuta hata ya tarehe 23 nkakosa, zilizoko ni za tarehe 25. Wakati tuko kwa folen wanakuja watu kama wanafahamiana hivi na wahudumu wa haya makampuni, sababu wanasalimiana vizur tu kisha wanachaniwa tickets wanaenda kuwapa wateja wao pembeni kidogo na hapo. Nikatoka kidogo nikamfuata yule jamaa mmpjawapo alieingia hapo nkamwambia nataka tiketi na nina mgonjwa namuwahi, sitaki kukaa foleni, akaniambia nimpe 38,000 nimsubir, kweli akaja na ticket ya tarehe 22.

Kumbe ticket zipo, ila ndo wanauziwa/wanapewa Vishoka/Madalali. Inawezekana ni mpango wa Wafanyakazi au hata Wamiliki wanahusika. Tunajua hiki ni kipindi chenu cha kupiga hela lakini oigeni kihalali basi. Mbona abiria ni wengi tu hata mkifanya bei za halali bado mnapata hela za kutosha tu? Serikali si ilishapiga marufuku upandishwaji holela wa nauli msimu wa sikukuu kama huu? Au hii ndo sababu wenye makampuni haya ya mabas hawataki mfumo wa ki-electronic sababu utakua unawapuguzia huu upigaji unaofanyika??

Hivi serikali imeshawaza hata kupeleka makachero wake eneo hili ili hata iweze kujua kama kuna michezo michafu??
 
POLE SANA MKUU

KINACHOUMIZA ZAIDI HAKUNA SEHEMU YA KUSEMEA HAYA YAKATAFUTIWA UFUMBUZI.

NAKUMBUKA MIAKA HIYO TUNATOKA SHULE TABORA KURUDI DSM,WENYE MABASI WALIKUWA NA UTAMADUNI WA PANDISHA GHARAMA ZA NAULI WATAKAVYO.
NASI KUONDOA HASIRA NA UCHUNGU TUNA HAKIKISHA TUNACHANA CHANA VITI/SITI.
MARA KADHAA TULIJARIBU KUNYA HUMO HUMO BILA MAFANIKIO
 
Wakuu Kwema?

Niende Kwenye Mada, Shemeji yenu ni mtu wa kutoka Mikoa ya kaskazini, na kama mnavyojua kila ikifika tarehe kama hizi basi Pilika pilika za kueleke maeneo/mikoa hiyo hua zinakua nyingi sana. Mimi kwa kujua hilo ulipoanza huu mwezi tu nikaenda hapo Ubungo kwa ajili ya kumkatia shemeji yenu ticket, yeye antarajia kusafiri tarehe 22 ndo likizo yake inaanza.

Sasa siku hiyo nilipoenda tarehe 1 hiyo nikaambiwa utaratibu ni kua Tickets za tarehe yoyote huanza kukatwa/booked siku zisizozidi 5 kabla ya safari. Ndo kusema kua kwa taerehe hiyo 1, ticket pekee nayoweza kukata ni kuanzia tarehe 01 mpaka 05, sio zaidi ya hapo. Na nikitaka ya tarehe 25 basi nije kuanzia tarehe 20. Nikasema ngoja nizunguke kwenye makampuni mengine pengine wako na utaratibu tofauti. Eneo hilila Shekilango lina Kampuni za Mabas za nazozikumbuka za Kidia One, Marangu Coach, Esther, Kilimanjaro, Dar Express, Dar Lux, Happy Nation, BM Coach. Kote nilikopita utaratibu ulikua ni huu huu. Hakuna alienikubalia kukata ya tarehe 22.

Nikaondoka huku nikipiga hesabu kua nikienda kuanzia tarehe 18 December (Leo) nitapata ticket nayoitaka. Nimeenda leo hapo Urafiki kwa ticket ya tarehe 22 nkakosa. Kampuni moja nkaambiwa zimeisha toka juzi, nkawauliza kwani walishaanza kuziuza toka juzi, wakasema ndiyo. Nkazunguka tena kutafuta hata ya tarehe 23 nkakosa, zilizoko ni za tarehe 25. Wakati tuko kwa folen wanakuja watu kama wanafahamiana hivi na wahudumu wa haya makampuni, sababu wanasalimiana vizur tu kisha wanachaniwa tickets wanaenda kuwapa wateja wao pembeni kidogo na hapo. Nikatoka kidogo nikamfuata yule jamaa mmpjawapo alieingia hapo nkamwambia nataka tiketi na nina mgonjwa namuwahi, sitaki kukaa foleni, akaniambia nimpe 38,000 nimsubir, kweli akaja na ticket ya tarehe 22.

Kumbe ticket zipo, ila ndo wanauziwa/wanapewa Vishoka/Madalali. Inawezekana ni mpango wa Wafanyakazi au hata Wamiliki wanahusika. Tunajua hiki ni kipindi chenu cha kupiga hela lakini oigeni kihalali basi. Mbona abiria ni wengi tu hata mkifanya bei za halali bado mnapata hela za kutosha tu? Serikali si ilishapiga marufuku upandishwaji holela wa nauli msimu wa sikukuu kama huu? Au hii ndo sababu wenye makampuni haya ya mabas hawataki mfumo wa ki-electronic sababu utakua unawapuguzia huu upigaji unaofanyika??

Hivi serikali imeshawaza hata kupeleka makachero wake eneo hili ili hata iweze kujua kama kuna michezo michafu??
Serikali sidhani kama itakusaidia, pandeni treni
 
In principle kupanda huku kwa bei za usafiri wakati huu wa sikukuu ndio huo huo unaotumika na madalali wa COMMODODITIES kuwanyonya wakulima wa mazao kama KOROSHO NA SUKARI!!! Hawa madalali ndio wanaofaidika at the detriment of wakulima na wasafiri!!!
Serikali inaelekea haina uelewa wa operations za CARTELS namna hii especially kwenye biashara ya MAZAO YA WAKULIMA [COMMODIDITIES]!!!
 
-Kuna mabasi yako very smart huwezi kuwakumbusha tiketi ya kielectronic wanakuwekea,na tiketi zao pamoja.
-Nachukia sana kupigwa/kuibiwa na madalali wa mabasi,mengi yamejaa wahuni.Ukiwa mgeni unaweza kutamani kulia...SUMATRA sioni wakilinda watumiaji usafiri huenda Wana wasimamiaji wachache sana.
-Abiria Bado tunasafari ndefu ya kuibiwa
 
Mkuu mbona unatokwa na povu sana ni simple nunua gar yako mpeleke over
 
Back
Top Bottom